Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imechangamka ile mbaya, mambo yako moto fire, marais wa nchi wanachama wapo busy hapa na pale.
Lakini ukweli mchungu ni kuwa kuna marais wa nchi majirani wanaopiga hatua za kiwango cha dunia huku wengine tukibaki kuwa watazamaji wa mechi za wenzetu.
Ukiangalia jumuiya yetu hivi sasa, mataifa ya Kenya na Rwanda ndio GOATS wa maono haswa kwenye jukwaa la kimataifa. Huku wenzetu wakipanga mipango ya matukio ya kuvuna pesa nyingi tunazungumzia mabilioni ya fedha, sisi huku watanzania tumebaki mabingwa wa kupanga mikakati isiyotekelezeka na kuimba mapambio ya kusifu viongozi masaa 24/7 mwaka mzma.
Hebu mtazame jirani yetu Rwanda. Nchi ndogo kijiografia, lakini yenye akili za ukubwa wa bara zima. Kagame yule mwanaume ni Genius, kwani Rwanda imefanya kweli kwa kusaini mkataba wa miaka 10 wa kuleta mashindano ya mbio za magari za Formula 1 (African Grand Prix) pale mjini Bugesera kuanzia miaka ya mapema ya 2030.
Yaani wakati sisi bado tunagombania bodaboda zisipaki katikati ya mji na kuanzisha vikao vya kutafakari jinsi ya kupunguza foleni za magari Dar es Salaam, wao Rwanda wanajiandaa kutandaza lami za kiwango cha FIA Grade 1 ili akina Lewis Hamilton waje kukunja kona kwa speed ya km 350 kwa saa! Wenzetu wametambua kuwa michezo ni biashara ya diplomasia na utalii wa kiwango cha juu.
Ukivuka tu Namanga kuna jamaa wana akili tofauti kabsa na sisi, Wakenya hawajabaki nyuma. Kuna moto unakwenda kuwaka ndani ya Jiji la Nairobi, Januari 5, 2027, uwanja mpya wa Raila Odinga International Stadium pale Talanta Sports City utafunguliwa kwa mechi ya kihistoria kati ya miamba ya soka duniani: Bayern Munich dhidi ya Ajax Amsterdam!
Hapa hatuongelei timu za mchangani au mechi za ndondo cup; tunazungumzia miamba iliyotwaa Mataji ya Klabu Bingwa Ulaya! Uwanja huo wenye uwezo wa kubeba watu takribani 60,000 utazinduliwa kwa kishindo kikubwa kikienda kuonesha taswira ya Kenya kuelekea AFCON 2027. Bila shaka game ya fainali itapigiwq hapo.
Sasa keti kitako utazame upande wetu wa Bongo! Sisi tuko busy na nini? Tuko busy kupanga miradi ya majaribio isiyo na matokeo ya msingi, huku redio na runinga zetu zikijazwa na makofi na nyimbo za sifa kwa viongozi wa serikali kwa kutengeneza barabara ya lami ya kilomita mbili!
Media zinapiga kelele kuwa Makonda kaenda Barcelona, halafu anapiga picha na Laporta akiwa na jezi mamba 10 ya Samia. Aisee, wakati Wanyarwanda wakitangaza taifa lao kupitia Jezi ya Visit Rwanda, sisi tunatangaza taifa letu kupitia jezi za Makonda na Samia.
Badala ya kuweka mikakati ya kuvuta matukio makubwa yatakayowaleta watalii na wawekezaji wa maana duniani, sisi tunajipiga kifua kwa kukamilisha mambo ya msingi ambayo kisheria ni wajibu wa serikali.
Ukipita kwenye mikutano yetu, utasikia hotuba ndefu za "tuko kwenye mchakato wa kufanya upembuzi yakinifu." Hivi huyo "upembuzi yakinifu" wetu huwa unaisha lini ili na sisi turudie kuwaalika angalabu Real Sociedad au Arsenal pale Benjamin Mkapa kama tulivyofanya kwa Sevilla?
Kenya na Rwanda zimetufundisha somo moja kuu: dunia ya bhana haisubiri porojo wala mapambio. Unapowekeza kwenye miundombinu yenye malengo ya kimataifa na kufungua milango kwa majina makubwa, unaleta fursa halisi za kiuchumi na ajira.
Sisi tukizidi kukumbatia unafiki na kuridhika na mambo madogo huku tukipiga makofi, tutabaki kuwa mashabiki wa kusafiri kwenda Nairobi kuwatazama kina Harry Kane wakiwa na kikosi cha Bayern Munich au kwenda Kigali kushuhudia Formula 1!