Mkuu John tatizo kubwa linalotuumiza watanzania ni UJINGA. Siku zote watu wamekuwa wakisema lakini wanaonekana wana chuki dhidi ya serikali. Ila ukweli ni kwamba sisi tulikuwa na nafasi kubwa ya kupiga hatua kubwa sana kimaendeleo kuliko ncho yoyote ile barani Afrika.
Kamati ya haki ya mtoto ya Umoja wa Afrika (African Committee on Rights and Welfare of the Child) iliwahi kuchapisha taarifa yake ya mwaka na kutaja nchi ambazo zinatoa elimu bora yenye viwango kwa watoto barani Afrika. Rwanda ndiyo ilikuwa ya kwanza, na wataalamu wengi wakapinga. Timu maalumu (Special Rapporteur) walipelekwa Rwanda kuhakikisha hili na kuthibitisha yote ndani ya ripoti.
Kila mtoto ambaye anaanza elimu ya msingi nchini Rwanda anatumia Laptop/Ipad kusoma. Binafsi sikuamini lakini nikazungumza na watu wa kwenye kamati wakathibitisha hilo. Nikashangaa tena kusikia kule nchini Rwanda ni marufuku mtoto kupelekwa kwenye shule ya bweni mpaka afikishe miaka 14. Nikasema kama Raisi Paul Kagame ataendelea kufanya hivi, kuna siku tutaiangalia Rwanda kiutofauti sana.
Rwanda iko na madhaifu mengi kiutawala na kimfumo: UKABILA umeshamiri kwenye kila eneo na kama Raisi Kagame atabadilika na kukubali kuelewana na Wahutu bila kuweka masharti (Conditions) zozote zile kwenye amani, basi Rwanda itafika mbali sana. Maana taifa lolote lile ambalo linawekeza kwenye rasilimali watu ndiyo hufanikiwa kufika juu.
Ukweli mchungu ni lazima kukubali kwamba Tanzania tulijisahau sana, na hatupendi kukubali ukweli kwamba wananchi na viongozi wetu akili zetu ziko chini ya kiwango (Below Avarage). Tumewekeza rasilimali zetu nyingi kwenye mambo ambayo siyo sahihi: Tunatumia mabilioni ya pesa kwenye siasa, ulinzi (political surveillance), matumizi yasiyo na msingi na ubadhilifu.
Tangu aondoke Mzee Nyerere madarakani hakujawahi tokea Raisi wa nchi hii ambaye aliweza kutambua nini haswa kinatakiwa kuwa kipaumbele kwa taifa. Mzee Nyerere mbali na madhaifu yake yote, aliwekeza sana kwenye ELIMU ya watu wake. Vijana wa Nyerere japo wengi waliasi falsafa na wengi wao kuwa walafi, ndiyo wameisaidia Tanzania isitumbukie korongoni kwa spidi kubwa. Hivyo tunatumbukia kidogo kidogo (Gradually Disintegrating)...
Mzee Lowassa alivyosema ELIMU, ELIMU, ELIMU hakukosea kabisa. Kuikomboa Tanzania tunahitaji watu wenye uelewa mzuri kuhusu mazingira ya nchi yetu. Nchi hii inategemea kilimo, uvuvi na ufugaji kama shughuli asilia za kiuchumi, lakini tumefanya nini kwenye kuwawezesha wananchi kwenye kilimo, uvuvi na ufugaji ??? Tuna wataalamu wangapi ambao wanaweza kutusaidia ??? Sisi tumekazania siasa na katiba mpya: Mambo ya muhimu sana, japo sidhani kama kila kitu kinaweza kutatuliwa kisiasa.
Nchi ndogo kama Uingereza na Japan ziliweza kuwa mataifa yenye nguvu sana duniani kwasababu walijua nini madhaifu yao na kufahamu vipaumbele vyao. Ingekuwa leo mtu anaenda Uingereza mwaka 1500 au Japani mwaka 1800 na akaambiwa hizi nchi zitakuja kuwa tajiri sana duniani asingeamini hata kidogo.