Taarifa kutoka Mahakama ya Rufaa inaonyesha kwamba Mbunge wa Mstaafu wa ccm Mh Sauli Henry Amon , ameshindwa kesi Mahakamani baada ya Familia ya Bushiri Pazi kurejeshewa nyumba iliyouzwa kwa mnada mwaka 2001 .
Ilikuwa hivi , Kampuni ya S.H.AMON ilishinda mnada wa nyumba namba 113 , Kitalu 4 , Block 17 ambayo ilikuwa mali ya Bushiri Pazi , iliyokuwa Kariakoo , Ilala , DSM , S.H.AMON alilipa Tsh mil 105 katika mnada uliofanyika 13/5/2001 , hii ilikuwa nyumba ya kawaida tu , baada ya kuinunua Sauli akaibomoa na kuporomosha jengo la ghorofa nane .
Mnada huo ulipingwa Mahakamani na Bushiri Pazi , ambaye alidai haukuwa halali , Baada ya danadana nyingi za kisheria kwenye Mahakama mbalimbali kwa miaka 20 , Hatimaye Ndugu Bushiri Pazi amerejeshewa nyumba yake , ila sasa si ile ya chini tena , ni ghorofa 8 .
View attachment 2203933
Chanzo : KYELA FM