Kama Benki imeuza nyumba kwa mnada kimakosa, baada ya mahakama kubatilisha mauzo. SH Amon yeye hana kosa.
Kwa vile uamuzi huu ni wa Mahakama ya Rufaa
waliokaa majaji watatu,
Hamisi Bushiri Pazi & Others vs Saul Henry Amon & Others (Civil Appeal 166 of 2019) [2022] TZCA 186 (13 April 2022); | Tanzlii, bado anaweza kuomba rufaa nyingine, Mahakama wakakaa majaji watano, Half Bench
kupinga uamuzi wa mahakama ya Rufaa kumpora ghorofa lake alilojenga baada ya kununua kihalali nyumba iliyokuwepo kabla kwa mnada halali wa Benki.
Rufaa hiyo ya half bench ikishindikana, then, anakata Rufaa ya mwisho kabisa, kwa Mahakama kukaa Full Bench, Majaji 7, wakiongozwa na Jaji Mkuu, CJ mwenyewe in person, ambapo sasa uamuzi wa Full Bench ndio uamuzi wa mwisho, final and conclusive, Kwa mfumo wetu wa sheria, hivyo kilichobaki ni Kwa SH Amon anaifungulia benki kesi ya madai kudai fidia na anashinda straight away.
P