Saa 12 alfajri hadi saa 12 jioni, mtoto wa shule ya msingi anasoma nini kikubwa hivyo huko shuleni?

kukaririshwa tu. wanasiasa wanawapa waalimu presha kubwa mno hasa kwa haya madarasa mapya mambo yameharibika zaidi,kila mmoja anataka matokeo mazuri
 
Wanakwambia eti watoto wa siku hizi sio kama zamani...sijui vitoto tunavyozaa siku hizi ni vingedere ...?
 
Chakushangaza sijasikia wale wazee wa haki za binadamu wakipwayuka kuhusu ili ila sula la mtu mzima na akili zake kuzibuliwa chemba wanapwayuka. Useless individuals.

Huu utaratibu ni kiwakosesha watoto haki yao ya kiwa watoto. Mtoto hapati ata muda wakuruka sarakasi au kucheza kula tumbakishie baba...inakera kwa kweli
 
Huu upupu ukemewe kabisa Kuna shule wanajiita Montessori ya hapo town daslam,wanafunzi inakupasa ufike saa kumi na mbili mapema ikifika saa Moja au saa mbili mtoto haruhusiwi kuingia darasani,
Kuna dogo yupo std seven anatoka chanika saa kumi,anapambana na daladala mpka city siku akipitisha tu akifika kule saa 2 haloo
Yule mkuu wao ambaye ni sister ana roho mbayaaaaa huingii shule unaishia getini,yule dogo anahenya Sana
Hawa watawa Wana roho Mbaya sana Aisee Yaani hajali Wala Nini halafu watoto wanarudi saa Moja jioni dogo kufika chanika saa 4 usiku analala masaa ma 4 tu
Daaa hata kama elimu hii too much wadau
Mamlaka shughulikieni mbona huko Nchi za Scandinavian watoto wanatimba skulii saa tatu asubuhi bila presha na wametuzidi mbali wajameni?
Tafakari!
 
Siku hizi wanawang'ang'ania wake boarding😂!
 
Mikoa ya kanda ya ziwa,wanafunzi kuanzia darasa la tatu na kuendelea wanatoka saa 6:30 hadi saa 7 mchana,wanarud majumbani kula,then wanarud shuleni,huko shuleni hakuna la maana,misimu kama hii ya mavuno ni kazi kwenda mbele,wanageuzwa vibarua wa mashamba ya walimu/shule. Basi ni heri shule zingekua na upungufu wa madarasa,tungesema kuna session ( wa asbh na wa mchana),ukiuliza walimu wanakwambia ni mpango wa mkoa[emoji24]
Sekondari (kutwa/day) nako mwendo ni ule ule,kutoka saa 8:10 mchana,kurudi saa 10 jioni,kutoka shule ni jioni saa 12,mpk afike anapoishi ni saa 1 uck na kuendelea,kesho anaamka na ratiba ile ile.
Kwa tathmini ya mchana,mwendo wa kutoka shuleni mpaka afike nyumbani,ale chakula,apumzike kwa hayo masaa mawili hautoshi,tunawafanya wanafunzi waone shule kama adhabu,shule ina madarasa ya kutosha na walimu wa kutosha tu,kuna haja gani ya kumrudisha mwanafunzi jioni ilhali alishatumia masaa 8 kujifunza?
Sioni sababu ya mwanafunzi kurudishwa shuleni mara mbili mbili ilhali alishatumia masaa 8 ya asbh na mchana kujifunza,Unless shule iwe na shift,mfano form 1&2 asbh,form 3&4 mchana kwa shule zenye upungufu wa madarasa (ambazo now sidhani kama zipo)
Ushauri wangu,kurudi jioni iwe ni kwa siku maalum ya michezo tu,sherehe(graduations/welcome form 1,Clubs events au etc) au km kutakua na maandalizi ya matukio maalum mf. Mapokezi ya viongozi,mwenge na matukio ya kufanana na hayo.
Vinginevyo,tuwape watoto muda mwingi pia wa kupumzika,kuwa karibu na wazazi/walezi (now maadili yanashuka sababu mtoto hapat mda wa kutosha wa kukaa na wazazi,shule imechukua muda mwingi wa mtoto kuliko mzazi) na kufundishwa majukumu mengine nje ya masomo ya shuleni.
 
Maisha ya sas mtoto akishajua kusoma na kuandika inatosha,
la ziada labda akasomee lugha za kimataifa kwa msaada wa hapo mbelen napo kama kuna ulazima.

Hakuna mtoto atakaekula bata shuleni kama mwanangu/wanangu.

Maana sitotaka wasomee shida/upumbavu kama tuliosomea wazaz wao na mababu zetu,

Elimu ya mchongo/useless, elimu inayomtaka akalili na kutofikiri nje ya box, hiyo sio elimu, bali takataka.

Elimu iliyobase kwa theories za watu wengine huko hiyo ni useless.

Technologies ambazo ziliibwa na wahuni fulani kutoka ktk jamii za kale, na kuja kutudanganya kuwa wamegundua watu wengine na kujipa majina makubwa na sifa nyingi kumbe takataka kabisa, elimu kama hiz ni takataka, hazifai kwa watoto wa kizaz kipya chenye uelewa mpana.

Histories za uongo, kuanzia stories za dunia, uongo mtupu, yaan hadi kero, kuna mambo ukiyajuwa undan wake na umeyasoma kwa zaid ya miaka15 kumbe ulkuwa uongo na uzushi, inauma sana.

Mimi mwanangu nitaruhusu shuleni ajifunze masomo 3 tuu, yaan hesabu, English na masomo ya tehama tuu, maana atleast yana uwakika& uhalisia mtaani.

Akimaliza la7 hakuna kwenda sekondary, nampeleka short coz/ shule ya lugha ya kiingereza mwaka mmoja, then akimaliza anarud mtaan tuendelee kupambania mambo ya muhimu.

Siwez poteza pesa zangu,muda wangu/wa mwanangu kuwajaza takataka kichwani
 
Umeandika mambo ya maana sana ila nasikitika kukujulisha kuwa USHAURI WAKO UTAISHIA HUMU HUMU
 
Aisee huo ni utumwa kwa mwalimu na mwanafunzi
 
mkuu na akirudi hiyo saa 12 ana homework hiyo ya kufanya masaaa mawiki na hayo maswali hajawahi kufundishwa inabadi wewe mzazi ndo uwe mwalimu
 
Watoto wengine wanakaa umbali mrefu mfano mtaani kwangu watoto wa drs la 7 wanataka saa 11alfajiri na kurudi saa 2 usiku huku wakiwa wamechoka kabisa.
anaamka sa 10 huyo kama dereva wa basi la mkoano kwenda dar [emoji23]
 
Ninachojua mimi nikuwa mfano darasa la saba wanafanya mtihani mwezi wa 9 sasa bila kuongeza muda wa kosoma hawawezi maliza topic, ambazo kikawaida huwa zinaisha mwezi wa 11.
Kwani zamani ilikuwaje kipindi tukitoka shule saa 8:30 mchana . Je tulikuwa hatufaulu?
 
Huwa nikitoka jogging jioni nakutana na vitoto vya shule za serikali ndo vinatoka shule mida hio saa moja na robo hv. Huwa nahuzunika sana rohoni coz wanawekwa kwenye hatr ya kubakwa na kujifunza tabia mbaya.

Young students may be 10% of our population but they're 100% of our future. Serikali inbidi waangalie hili kwakweli
 
KILA WIKI WASAFI WANATOA NYIMBO MPYA KAMA 5 HIV......UNATEGEMEA TUTAZIKALILI MUDA GANI????
 
Kuna kitu kizito sana kilichogandamana ktk elimu yetu ambacho kukitoa itakua ni kazi ngumuu... Nacho ni mtaala ulioegemea 'MITIHANI' ... tunahitaji mtazamo mpya.

Mateso yote haya wanayopata watoto ni shule tu zinafokasi ktk mtihani wa mwisho kugombania position, huu ni ujinga mkubwa. Hakuna maarifa yeyote zaidi ya watoto kukaririshwa mitihani. USELESS
 
Tatizo lipo kwa BARAZA LA MITIHANI/NECTA ambao wanadhamana ya kutunga mitihani haswa Darasa la saba.
wanashindwa kuelewa kuwa mtihani ni kipimo tu sio kukomoa watoto.
kwa kuwa mitihani inayo tungwa hailengi kupima uelewa wa watoto ndio matokeo yake ndio hayo ya kuwataabisha watoto.
 
Mimi mwanangu nitaruhusu shuleni ajifunze masomo 3 tuu, yaan hesabu, English na masomo ya tehama tuu, maana atleast yana uwakika& uhalisia mtaani.
Sasa utampeleka shule gani itayoruhusu mwanao peke yake ndo awe na kamtaala ka peke yake..

Ila mtizamo wako uko poa sana.

Mi nitafokasi zaidi ktk vocational training..yani wakitoka form four tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…