Saa 12 alfajri hadi saa 12 jioni, mtoto wa shule ya msingi anasoma nini kikubwa hivyo huko shuleni?

Kwani zamani ilikuwaje kipindi tukitoka shule saa 8:30 mchana . Je tulikuwa hatufaulu?
Hili swali ndilo nalojiuliza...

Ila nishaelewa...hii ni kwa sababu WALIMU HAWA NI WALE WALIOPATA DIV 3 MPAKA 4...Kwahiyo tuseme hawana mbinu za ufaulu wenye tija...
 
Nawashangas sana ma afisa elimu wa wilaya, sijui kazi yao nini, yaani watoto wadogo wa darasa la nne wana amshwa saa kumi za usiku, wanakalilishwa adi saa nne za usiku, jumatatu adi jumamosi, hata university tulikuwa hatusomi hivyo
 
INASIKITISHA SERIKALI NDIYO INASHIRIKI KUTUHARIBIA KIZAZI...ALAFU BAADAE WANAKILAUMU HICHO HICHO...
 
Yaani hata hiyo position haisaidii kitu...ni sifa tu za kijinga...
 
Mbona saivi tunafundisha kwa kufuata kalenda ambayo lengo lake mtoto asome kwa kurelax.Serikali ishaona na tumeelimishwa pia
 
Nawashangas sana ma afisa elimu wa wilaya, sijui kazi yao nini, yaani watoto wadogo wa darasa la nne wana amshwa saa kumi za usiku, wanakalilishwa adi saa nne za usiku, jumatatu adi jumamosi, hata university tulikuwa hatusomi hivyo
YAANI ELIMU YA UNIVERSITY AMBAYO INA MAANA KULIKO HIYO PRIMARY HATUKUSOMA HIVYO...
 
YAANI ELIMU YA UNIVERSITY AMBAYO INA MAANA KULIKO HIYO PRIMARY HATUKUSOMA HIVYO...
Shida ipo kuanzia wizara ya elimu yenyewe, sijui ni kwanini hawatoi mwongozo juu ya hii kelo, hizi ‘english medium’ zina uwa watoto wetu kimya kimya……..
 
Umenena vyema, naunga mkono hoja. Hili jambo halina afya kwa watoto, Maisha sio kusoma tu, na ahwataishi kwa kusoma tu, bali kwa kila jambo jema linalotendeka katika jamii. Hayo mambo ya kijamii watajifunza saa ngapi kama muda wote wapo shule au darasani. By the way nia sio kuwasaidia wanafunzi bali ni mbinu ya walimu kujiongezea kipato
 
Kweli...
 
Ukiacha hili la muda Kuna hili la idadi ya masomo wanaosoma hawa watoto, unakuta kitoto cha darasa la 3 Kina lumbesa la madaftar hili nalo ni tatizo .
 
Wewe ulikuwa unatoka saa ngapi shule?
Kitendo cha kuwa shuleni tu ni shule tosha kwani kuna social interaction, watoto wametoka katika malezi tofauti mengine ya wazazi wa hovyo kabisa, hivyo wanapokuwa shuleni waalimu wanawanyoosha ili waweze kuendana na jamii wskikuwa
 
Aisee Hili Tatizo kubwa Sana yaani ujue ulichosoma shule ya msingi Kwa Miaka Saba Kwa kiswahili,unaenda kukirudia Secondary Kwa kingereza,ukifika chuo uaply kozi ni Mbingu na ardhi Kwa uliyosoma Shule ya msingi na Secondary
Yaani Kiufupi elimu yetu Haina muunganiko kabisa Kila kitu kinajiendea tu bila mpangilio

Hizi nchi za kiafrika shida kweli kweli!
 
Advance Pcm chuo mtu anasomea uhasibu
 
Acha woga pamoja unatumia ID fake bado umeogopa kutaja shule uliyonayo karibu
 
Hili swali ndilo nalojiuliza...

Ila nishaelewa...hii ni kwa sababu WALIMU HAWA NI WALE WALIOPATA DIV 3 MPAKA 4...Kwahiyo tuseme hawana mbinu za ufaulu wenye tija...
Japo sample space yangu ni ndogo ila hapa tusiwasingizie walimu wasio na vyeo. Mchezo huu unachezwa na viongozi wa elimu kushirikiana na walimu wakuu (japo pia kuna walimu wachache wapumbavu wanaolishangilia hili na hawa ni wale wasiokuwa na njia nyingine ya kujiongezea kipato).

Four years back wakati napambana kupata kazi nilijishikiza kwenye shule moja ya English Medium. Nilisikitika sana kuona walimu wanavyopewa majukumu makubwa ya kazi kwa malipo finyu sana. Maagizo ya watoto kufaulu yanatoka kwa Afisa Elimu kuanzia ngazi ya mkoa, yanafika hadi kwa walimu wakuu. Hao maafisa elimu wanawaacha walimu wakuu wabuni mbinu zao wenyewe ili mradi watoto wafaulu tu. Na hapa ndo hili la "kuwatumikisha" watoto linaposhamiri. Ni kweli inasikitisha sana kuona watoto wanatumia nguvu kubwa kupata elimu hadi wanakosa maarifa muhimu mtaani. Watoto unawauliza wanakwambia hawajawai kukamata kuku, hawajui kotama ni nini, hawajui mila zao maana hata likizo zao wanazispend huko huko shule! Inasikitisha mno

Niseme tu hili pia linachangiwa na wazazi wenyewe tena kwa asilimia kubwa. Wengi wao wanalibariki hili ili mradi watoto wao wafaulu tu! Kwa wazazi wengi wa Dar es Salaam ubize pia unachangia wao kulibariki jambo hili. Kwenye vikao vya shule na wazazi utasikitika mno kusikia baadhi ya mitazamo ya wazazi. Kila mzazi anataka mtoto wake apate grade "A" na yupo tayari kusikiliza mbinu zitakazotolewa na shule likiwemo hilo la kubakiza watoto shuleni kwa muda mrefu.

Mfumo wenyewe wa elimu umeingiliwa. Kila kukicha kuna mabadiliko hadi walimu ambao ndo implementors wakubwa wanachanganyikiwa. Kila kukicha kuna mabadiliko ya mitaala na namna ya ufundishaji, hadi walimu wanaona ni heri waongezewe muda wa kupambana na mabadiliko hayo. Na hapa sikuwahi kuona umuhimu wa CWT, wenyewe wanakubaliana na kila jambo linaloamriwa na wakuu.

Elimu ya Tanzania ina safari bado! Tena ndefu mno! Na huu mfumo wa kupima uelewa wa mtoto kwa kutumia "mitihani" hauwezi kumaliza changamoto hizi. Yaani watoto watazidi kutumikishwa tu.
 
Nimeenda shulen kwa wamangu na kuuliza juu ya hili mwez huu mwanzoni..mwl you hakuwa na majibu akasema nimuulize mkurugenzo..mkurugenz nikamuomba waraka wa serikali unaosema watoto kwa masaa hayo..Hana....nikawaabia mnawaumiza watoto...wa kwanngu NAOMBA mda wa kurudi nyumban ukifika warud...
Nikaonekana napinga watoto wasisome..nikampa facts kuwa mtoto hafaulu kwa kusoma had saa tatu usiku..
Huu mtaala was nchi hi Nicole was kinyonge na kijinga Sana unategemea mtihan tu..
 
Wewe utakuwa na watoto vilaza na wasiopenda shule ndio maana unawachongea watoto wanaopenda shule ili wawe vilaza kama wanao. Mimi mwanangu yupo shule binafsi na wanasoma hadi saa tatu usiku, wewe unalalamikia saa 12 jioni? PUMBAVU!!!!
 
Tatizo Wazazi mnajifanya wajuaji sana..walimu wanatumia akili zao kubuni jinsi ya kuwafundisha watoto wenu wenye vichwa vigumu...mnakuja kuanzisha Uzi jf
 
Ongeza na furushi la madaftari, mtoto wa darasa la nne ana mbegi mkubwa kama mtalii, watoto wanachoka mgongo lakini bado hata ukimpa hesabu ya kutafuta mzingo wa duara hawezi. Ukimuuliza pundamilia anaitwaje kwa kingereza anaanza kuchezesha kope, yn walimu wa govt primary schools wa sasa ni mizigo. Wamebaki kukusanya vimichango ambavyo kiuhalisia vinazidi kuwafanya wawe na hali ngumu ya maisha cz ni dhuluma ile wanafanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…