Saa ishirini na nne za Nusrat Hanje kutia doa Mihimili mitatu ya Nchi

Saa ishirini na nne za Nusrat Hanje kutia doa Mihimili mitatu ya Nchi

Hupendi viongozi waadilifu
Sipendi viongozi wahuni ambao hawaheshimu katiba ambayo waliapa kuilinda. Marehemu Nyerere alisema "Rais asiyeheshimu katiba hatufai" abaki kuburuza familia yake nyumbani kwake na sio nchi.
 
Mkuu usihangaike na mbumbumbu wa humu JF. Wakisikia kuwa DPP amewaachia mahabusu wanafikiri anaenda yeye in person kuwatoa. Wakati utaratibu ni lazima removal order itolewe na Mahakama, kuna uwezekano removal order imetolewa mapema lakini process ya kuwatoa ndiyo ilichelewa hadi ikafika huo muda wanaousema kama ilivyokuwa kwa kina Mbowe removal order ilitoka mapema lakini walitoka Segerea jioni. Achana na hao wanasaccos uelewa wao ni mdogo sana.
Wewe umeshawahi kukaa gerezani kwa muda aliokaa Nusrat kwa makosa uchwara!? Endelea kutukuza miungu watu uchwara wanaokanyaga haki za watu.
 
HAKIKA UMEUVUA NGUO UTAWALA HUU WA KISHETAN WA AWAMU YA TANO.

Hakuna kufuata sheria wala katiba JIWE ANAUA NCHI.
 
Msimsikilize Mnyika ni muongo na mpotoshaji na siku zote hajawahi kutoa malalamiko juu ya lolote ikawa kama alivyozusha ,, hana akili timamu huyo,,, Mbowe anajua afanyacho, Nusrat kutoka maahabusu ni mchakato uliochukua zaidi ya wiki ila kutoka nje ni dakika 3 hivyo kama ni form zilijazwa akiwa maabusu na hata viwalo ni kitu rahisi na tiketi ya ndege kwenda DOM,, Msimsikilize Mnyika hayuko sawa mahali fulani,,, mbona Mbowe hajasema kitu na hao kina Mwalimu wako wapi??
Wa kwenye vigodoro wengi kweli huko
 
Imekuuma Nusrat kutoka mahabusu! Yeye ni wa kwanza kutolewa gerezani? Viongozi wa CHADEMA waliwahi kutolewa mahabusu Dar kwa teksi. Kama kuna udharura mahakama inaweza kukaa hata usiku na mahali popote.

Serikali inaweza lumfutia mashtaka mtuhumiwa wakati wowote.

Umashangaa Nusrat kuwa mbunge akitokea mahabusu, kwa taarifa yako kule Zaire wakati wa Mobutu kuna mwanasiasa aliitwa Nguza Karl Bond aliwahi kutolewa gerezani akisubiri kunyongwa na kuapishwa kuwa waziri mkuu na serikali hiyo hiyo iliyomhukumu. Mipango ya Mungu wewe mwanadamu huwezi kuijua.
Ndugu yangu, mipango ya shetani usije ukaiita ni ya Mungu. Mipango, miujiza ya Mungu hufuata haki na kweli.
 
Mbona unalilia!? Kwenye kampeni si mlikuwa mnapiga kelele watu magerezani waachiwe, bila dhamana??? Ndo kaachiwa sasa! Au ulitaka afie huko ili mzidi kujenga hoja za uzushi??? Umesema "mahakama imepelekeshwa mchakamchaka." Je unajua spidi ya utendaji wa mahakama kuwa ni "gani," kimfano!?? Ukijibu nitag, sawa? Usiponijibu nijulishe pia, sawa!?
Tangu uchafuzi uishe, yaonekana kuna wanaolipwa zaidi ya bk7, ili kuropoka ropoka. Mwenye afya njema ya akili hawezi kukubali kushushwa mpaka kiwango hiki.
 
Hauko serious! Kulalamika ndio ujuacho! Kama unao ushahidi lete mahakamani! Vinginevyo acha utoto! Si umeona wenye ukweli wamewahi kuingia bungeni maana wanajua mapichapicha yaliyochezeshwa!
Mahakama ipi? Wewe ndio hauko serious.
 
Hauko serious! Kulalamika ndio ujuacho! Kama unao ushahidi lete mahakamani! Vinginevyo acha utoto! Si umeona wenye ukweli wamewahi kuingia bungeni maana wanajua mapichapicha yaliyochezeshwa!
Mahakama ipi kwenye mfumo huu huu unaozidi kujigalagaza chini ya Mungu mtu? Wewe ndio nadhani hauko serious.
 
Back
Top Bottom