Saa ishirini na nne za Nusrat Hanje kutia doa Mihimili mitatu ya Nchi

Saa ishirini na nne za Nusrat Hanje kutia doa Mihimili mitatu ya Nchi

Hahahah Siasa za Tanzania Kiboko.

Waliokuwa wanamtetea Nusrat awe huru wanasikitika kutoka Mahabusu japo wamejificha kwny kichaka cha sheria

Halima Mdee imekuaje kalifyeka jina Kongwe la Viti Maalum la Joyce Mukya?
Hahahahahah.......kila zama na kitabu chake bwashe.
 
1. Tarehe 23/11/2020 Mtuhumiwa Nusrati aliyekuwa mahabusu bila dhamana alitolewa gerezani. Muhimili uliotumika kumtoa gerezani ulikua ni Inasikitisha mhimili wa serikali kwa kile kilichoelezwa kwamba Jamhuri ambayo ni Mimi na wewe hatuna haja ya kuendelea na kesi yake.

2. Mahakama kwa Tarehe hiyohiyo ilikimbizwa mchamchaka na dola ikabariki atolewe na baada ya kutoka akakabidhiwa kwa serikali ambayo ndiyo iliyomtuhumu.

3. Baada ya kupindua mhimili wa serikali na mahakama, Nusrat akisaidiwa na Tume ya uchaguzi (serikali) Tarehe 24/11/2020 akatinga kwenye viunga vya Bunge na kukutana na spika kisha spika akamwapisha kuwa Mbunge wa viti maalumu. Ikumbukwe Mbunge huyu anatakiwa apitishe fomu zake za Ubunge mahakamani hivyo yawezekana mahakama ilitumika pia kubariki kilichotokea bungeni. Bunge nalo likabeba mapungufu ya serikali na kuyapiga mhuri, Nusrat leo ni mbunge siyo mahabusu Tena.

Nusrat anatukumbusha kwamba unapodai haki yako na ukaamini katika kuwatetea wananchi movu huibuka na kuvunja misingi yote ya sheria na kukuinua.

Nusrat Mtuhumiwa amefanya miujiza mikubwa inayopaswa kuandikwa kwenye mbao mbalimbali, ndani ya saa ishirini na nne amekuwa na hadhi tatu muhimu ambazo ni binadamu wachache wamewahi kuzipata Duniani. Hadhi hizo Ni;
1. Hadi tarehe 23/11/2020 jioni alikuwa Mtuhumiwa wa makosa yasiyo na dhamana akiishi mahabusu.

2. Tarehe 23/11/2020 usiku akatoka gerezani akiwa Mwananchi huru asiye na hatia na kuelekea nyumbani kuoga na kuchagua nguo ya kuvaa siku iliyofuata. Natumai hakulala.

3. Tarehe 24/11/2020 asubuhi akaibuka kwenye viunga vya Bunge na kushika msahafu kisha kuapishwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano ya Tanzania yaani Mheshimiwa huku akiwa na kinga ya kibunge.

Haya yanatokea ulimwenguni ambapo kila Jumapili tunashinda nyumba za ibada kumwabudu muumba, haya yanafanywa na binadamu walewale ambao wanaomba Mungu atuepushe na balaa. Haya yanafanywa na binadamu wakitumia vitabu vitakatifu kuapa mbele ya vyombo vya habari.

Nadhani Nusrat anatuonesha kwamba adui yetu siyo Beberu bali adui yetu ni mtu mweusi anayelipwa fedha na watanzania kufanya maigizo ndani ya Tanzania kwa kutumia ofisi za umma na kutumia vitabu na misaafu tunayoamini ni mitikatifu.

Tunajiombea adhabu kwa Mungu, nadhani adhabu ipo mbioni kuwapata wanaowatendea Hawa viumbe haya. Si utashi wa Nusrat kuapa bali ameapa kuinusuru familia yake na ya mahabusu wengine waliokua hawana hatia. Ipo siku Nusrat atakua huru, ipo siku atapata nguvu yakusimamia anachokiamini.

Pole Nusrat na hongera kwa kuteuliwa kuwa Mbunge ukitokea Mahabusu. Wameona unafaa, wameona una kitu cha ziada kwa Taifa, usilipize tenda kwa nafasi uliyopewa.

Hongera Mtuhumiwa, hongera mtu huru, hongera Mbunge, hongera mpiganaji. Umeandika historia.
Sasa ametoka mnalalamika, mlitaka aendelee kusota rupango😲!? Nusrat anahitaji kuwafahamu adui zake wasiomtakia mema!
 
Kukata rufaa,? Kesi ya ngedere unampelekea nyani
Hauko serious! Kulalamika ndio ujuacho! Kama unao ushahidi lete mahakamani! Vinginevyo acha utoto! Si umeona wenye ukweli wamewahi kuingia bungeni maana wanajua mapichapicha yaliyochezeshwa!
 
Hata mimi naweza kulaumu shetani kanipitia kumbe kuna wanadamu,majini,wanga,vibwengu na wote wapo kwenye utawala wa mwenyemungu ila kwa kuwa yesu alisema ya mungu mpe mungu na ya muhandishi mpe JF
Hahahahahahahahahaaaaaa.Yamuandisi???
 
Ili mtu ateuliwe kuwa Mbunge Viti Maalum anatakiwa kujaza fomu za NEC namba 8D ambazo sehemu C Inatakiwa kujazwa na Katibu Mkuu wa Chama, na kiapo mbele ya Hakimu. Kama NEC imepokea hizo fomu, Mnyika alizijaza?

Kama Mnyika anatuambia akuzijaza, Nani alizijaza?

Je, NEC wanamjua Katibu Mkuu wa Chadema? Ndiye huyo aliyejaza?

Nusrat alikuwa Mahabusu, je, Nani alimjazia hizo fomu na alimjazia akiwa wapi na kuzirejesha Chadema? Je, mahakamani Nani alikwenda kuapa au Nusrati alitolewa akapelekwa mahakamani kimyakimya?

Je, sheria inaruhusu mtu kumjazia fomu za Ubunge mteule ambaye hayupo?Hakimu gani alimuapisha mtu asiyekuwepo?

Kama huu mchakato haukufuatwa Kuna umuhimu wa kuwa na taratibu na sheria?

Nasrati na wenzake walifutiwa mashtaka wakati gani na mbele ya hakimu Nani?

Kama lengo ni kuiua CHADEMA je tunaamini tunaiua au tunaua imani ya wananchi kwa vyombo vilivyopewa dhamana ya kusimamia haki?

Endapo mahakama ilimnyima Nusrat na wenzake dhamana, then over suddenly Jamhuri inajitokeza na kuwatoa ndani kisha bila kusita anatinga bungeni hatuoni Kama mahakama inatumika kuwaweka Mahabusu watu wasio na hatia kinyume kabisa na misingi ya uwepo wa chombo hiki?

Kama moja ya kazi ya Mahakama nikutenda haki, ni wakati gani Mahakama inapaswa kutenda haki? Ni baada ya kumnyima mtu Uhuru kwa miezi au miaka wakimtia Mahabusu? Au ni pale tu Mtuhumiwa anapofikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ndipo mahakama inapaswa kutenda haki?

Je, mahakama huru inaona ni haki kuendelea kupokea chaji zisizo na mashiko chini ya amri ya kiapo Cha DPP kuwatia watu ndani?

Kwanini tuendelee kuamini mahakama ni chombo Cha haki Kama binadamu wanaopaswa kusimia haki hawapo tayari kuisimamia?
Mkuu hi ndio Tanzania nchiyangu yenye burudani zakila ainaa
 
Zetu dua. Ila nalifuatilia hili suala kwa ukaribu kabla ya kustaafu kufatilia siasa zetu hizi.
Hahaahahhaahhaahaahhahaaaa msistafu.jomon badomnahitajika.Kwamustakbali wataifaletu.hv mnavyosema ndiomnatupunguzia sumu huku .Mtaani
 
Ushauri wa bure kwa mtoa mada

1. Achana na siasa za Tanzania. Kwa usalama wa afya yako, NEVER TAKE TANZANIAN POLITICS SERIOUSLY

2. Tumia muda wako kula vizuri, kunywa maji mengi, kula matunda na fanya mazoezi.

3. Hakikisha unatafuta future ya watoto wako na wewe mwenyewe kwa njia zingine zozote nje ya siasa.

4. Sio kila unaemuona kanisani kavaa koti kafunga mikono kifuani anasali kwa unyenyekevu anakuwa ana maanisha.

Sent from my SM-G973F using JamiiForums mobile app
Unachosahau ni kuwa siasa ndiyo maisha yako ya kila siku!

Ukiacha siasa ni sawa na mginjwa ambaye umemtundikia "drip" ya dawa ili a-survive, uamue kumwondolea drip hiyo!

Obviously mtu huyo atakufa
 
Mara nyingi sana huwa yanafanyika makosa ya kiufundi, kwa hilo lililotokea ni dhahiri watu wamekuwa wakifanya mambo bila kufiliria. Sasa sijui ni kwa mini?

Nilipokuwa chuo prof.wangu aliwahi kuniambia wizi upo na unaweza ukaiba ukashikwa na ukaiba usishikwe, inategemea na jinsi ulivyo weka doc. Zako na taratibu zako.

Tumeona kwenye uchaguzi,watu wameiba hadi wamepitiliza idadi ya kura, baada ya watu kuingia na kutumbukiza idadi ya kura sawa kwa wagombea wote, mtu anatumbukiza kura za rais 20,mbunge tano. Matokeo yake idadi ya kura zinatofautian

Kwenye suala la Hanje,kulikuwa na makosa makubwa ya kiufundi, haihiitaji mtu kuwa elimu ya chuo kikuu kugundua hilo. Hata mtu wa darasa la nne hapati shida kugundua .

Sasa huwa najiuliza huko juu hakuna watalaamu wa wizi, kama hawapo si wawakodi huku chini,
Hahaahahhaahhaahaahhahaaaa wangenikodisha hata mm kuu Nina diploma yawizi hukumtaani
 
Wabunge 19 wa viti maalum wa chadema ni ajira mpya inaandaliwa baada ya kufukuzwa hao wote.

Hovyo kabisa,walimu,madaktari,wauguzi,askari hali zao ngumu kimaisha halafu wao wanatumia fedha ktk mambo ya kijinga.
Ht mm najiuliza ccm wanapata wapi pesa za kuhonga watu ovyo
 
Hahaahahhaahhaahaahhahaaaa msistafu.jomon badomnahitajika.Kwamustakbali wataifaletu.hv mnavyosema ndiomnatupunguzia sumu huku .Mtaani
😂😂😂😂Bwana "mudy" hilo neno jomon limenishtua. Wewe ni Wali nazi au nazi wali. Au utakula kisha ukaoge au utaoga kisha ule?
 
CCM bhana sijui akili walishazipeleka wapi? Mahera anadai majina ya covid 19 yaliletwa na chadema ndio hayo aliyoyapeleka kwa Ndugai.

1. Mahera anadai CHADEMA iliwasilisha hayo majina tarehe 19 November 2020. Tarehe 20 Nov 2020 huyohuyo Mahera akiwa Azam tv alidai tume haijapokea majina ya viti maalumu kutokea CHADEMA. (Angalieni hizi tarehe mtaona nani muongo). Wanasema ukiwa muongo jitahidi uwe na kumbukumbu maana hii ni aibu.

2. Nusrat Hanje: tufanye basi ni kweli Mahera anasema ukweli kuwa Chadema iliwasilisha majina ya viti maalumu. Swali la kujiuliza: Nusrat Hanje alikuwa mahabusu, Chadema wana mamlaka gani nchi hii ya kuweka jina la Nusrat kwenye orodha ya viti maalumu na kuhakikisha wanamtoa mahabusu ili akaapishwe? Hapa ndio ninapowaona ccm either walishatuona watanzania hatuna akili au wao ndio hawana akili. Chadema ina mamlaka gani ya kumtoa mwanachama wake mahabusu ili awahi kuapishwa?

Ushauri wangu kwa chadema. Fungueni kesi mahakamani. Hii kesi ni rahisi sana kushinda. CCM imepanga huu mchezo kiboya sana.

Tunashukuru Nusrat Hanje ametoka mahabusu. Sasa dada wa watu yupo huru.
 
Back
Top Bottom