Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Umeongea kwa mhemuko sana hapa. Umtembeze mtoto 5Km ili tu ku prove kwamba humdekezi? Hizo ni akili kweli
Kabla ya kuhemka kumjibu mtu unapaswa kumwelewa kwanza.Unaelewa maana ya sentensi yenye maneno 'chini ya 5KM' ?
 
Tatizo kodi ikiondolewa gari litakuja ila matumizi yake yanakuwa tofauti
Kwenye shule mnaweka Model tofauti na Raia wengine hawaruhusiwi mbona Nchi zingine wameweza maisha sio magumu hivyo bandari haitusaidii kitu unakuta shule ya msingi ina hadi basi kama hayo ya mikoani...wakisema Coaster za 2018 aina fulani ni za shule tuu mwingine huwezj kuleta na muundo unakua tofauti nani hapa kwa sasa hivi anaagiza miaka ya 2018 kwa ajili ya abiria...sema kama 2023 tunazungumzia madawati na mbao zinaenda nje hilo swala kweli halitawezekana,
 
Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Nimeumia sana moyoni!

Hujasema ni wapi umemkuta huyo mtoto. Kama ni kijijini inawezekana ikawa shule iko mbali. Lakini kama ni mjini ni suala la ujinga na ushamba wa wazazi pia kudhani kuwa shule ndo inafaulisha.

Wazazi wengi hawafahamu kuwa mwalimu wa kwanza ni mzazi. Wazazi wengi hawatekelezi jukumu lao la ualimu na hivyo kujikuta wanahangaika kutafuta shule zinazofaulisha.

Wazazi hawajiulizi je wale wanaopata A kwenye shule za kata na shule za msingi za serikali huwa wanafanyeje.

Ndo unakuta mtoto anatoka Kimara Kilungule B au Bonyokwa anaenda kusoma Shule ya Msingi Bunge, Posta. Hapo ni lazima mtoto aamke usiku usiku na kuondoka kabla jua halijachomoza. Shule ya palepale jirani mzazi haitaki anakwambia haifaulishi.
 
Siku hizi tabu tupu.

1.vitoto vya primary vinapelekwa bweni , vinakosa malezi ya wazazi, vinafundishwa tabia mbaya huko.

2. Walio day wanaansha saa Tisa usiku saa 10/11 wako barabarani kwenda shule kurudi saa 11 jioni

Huyo mtoto atapata wapi muda wa kumpumzika na kucheza na wenzake wa mtaani kwake. atakuwa Hana socialization na wenzake. Ndio mwanzo wa jamii kuwa na ma introvertd kibao.

Huko shuleni anarundikwa ma homework kibao wengine wanakaririshwa wakapate A Ili shule ipate wanafunzi wengi.

3. LYK haijulikani ni ipi mara kiswahili mara kiingereza.

Elimu yetu Ina changamoto kubwa sana

Huko serikalini ndio usiseme walimu wanalia njaa serikali inawaangalia tu. Huyo mtoto Wa masikini anajiendendea tu sababu mwalimu Hana mzuka wa kufundisha tokana na kipato na maslahi duni..

Tumerogwa
 
Wenzetu kwa mfano Finland, watoto waanaanza kujifunza kusoma na.kuandika wakiwa na miaka 7. Chini ya hapo wanaenda kujifunza mambo mengine mpaka akili zikomae. Sasa huku kwetu yalaa, chekecheq mtoto anasoma mambo makubwa kuliko uwezo wake.
Chekechea mtu anasoma mambo chungunzima..
hapo unakuta katoto kana miaka mi3
 
Serikali iingilie kati hili suala, watoto hasa shule tokea ya awali, msingi wawe wanaingia darasani saa 2:30 kwa Dar, ili watoto wasiamke usiku sana, imagine 4 yrs kid kaamka saa 10 asubuhi anaondoka kila siku saa 10:40 asubuhi kwenda shule akiwa njiani au kwenye bus kalala hata hajui nini kinaendelea, mashuleni wanasinzia tu sbb bado wadogo mno mnoooo
 
Ungeona au kusikia watoto wa kichina wanateswa kiasi gani usingesema haya,tho sifurahishwi na watoto kutendewa hivi..China mtoto akipata 90 out of 100 anagombezwa..mtoto wa madarasa ya chini anasoma vitabu vingi kama mtu mzima
UONGOooooo
 
Kipindi nasoma hayo madarasa ya chini,kutoka ilikua saa 5 asubuhi,na tulikua tuna enjoy kinoma noma,hakukua na story za darasa la 7 watoke saa 12,kutoka mwisho saa 8 mchana.
O'level ikawa hvo hvo kutok mwisho saa 8 unaingia kitaa kukichafua mambo ya soka,wadau wa kilimo kumwagilia bustani jion safi kabisa.Naona hizi sifa za kutafuta ma A zinawapeleka watoto kubaya
A zenyewe basi ziwasaidie wanatafuta sifa tuu
 
Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Nimeumia sana moyoni!
Maeneo gani hayo ili tufuatilie kama ni mzazi ama mwalimu ndiye anayesababisha mtoto awe barabarani muda huo.

Nimeumia mno moyoni kusikia hivyo.
 
Mama anamwamsha mtoto yeye anarudi kulala katoto saa kumi na mbili na nusu kapo kwenye gari sijui kameamshwa saa ngapi?
Kaamshwe kavalishwe kapewe chai lazima ni kaliamshwa saa kumi usiku
..!!!
 
balaa sana mtoto wa nursery kaunta buku 10 vitabu kama vyote sijui ndio wanasomeaga upulofeseli mimi hata siwaelewagi kwa kweli, na cha kushangaza hizo shule wana ratiba ya kila siku kiasi kwamba anaweza kubeba vitu vinavyohusika na siku hiyo tu, kuna mahali tunakosesa sana .
 
balaa sana mtoto wa nursery kaunta buku 10 vitabu kama vyote sijui ndio wanasomeaga upulofeseli mimi hata siwaelewagi kwa kweli, na cha kushangaza hizo shule wana ratiba ya kila siku kiasi kwamba anaweza kubeba vitu vinavyohusika na siku hiyo tu, kuna mahali tunakosesa sana .
Hiyo nursery ya kauta book ni ya wapi hiyo, mbona balaa sasa. Huwa wanasoma nini huko loh
 
A zenyewe basi ziwasaidie wanatafuta sifa tuu
Kabisa ndugu,kuna madogo unakuta ana A flat,ila ukikaa kuongea nae unamuona ni mweupe kwenye mambo ambayo tulitegemea awe na ufahamu nayo....Lakini hizo A's kazipata kwa kukaririshwa na kuamshwa saa 11 asubuhi na kurudi saa 2...
Kingine nachoona wazazi au walezi wahitahid kupeleka watoto shule za karibu itasaidia sana
 
Saa kumi asubuhi nimepishana na katoto kadogo kana begi kubwa mgongoni, hivi shule za namna gani hizi?

Nimeumia sana moyoni!
Hii kitu imenikumbusha mbali sana,miaka hyo kijijini huko tunaamshwa saa kumi tunaondoka wengi kwa pamoja kwenda Shule,shule ilikuwa mbali sana alafu giza totoro mapori kibao,ile kitu imenifanya kuwa jasiri sana mpaka leo hii katika maisha yangu.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom