Uchaguzi 2020 Sababu 27 za kwanini Magufuli hafai kupewa miaka mingine 5 ya kuwa Rais

Mzalendo hawezi fika mahali, akawambia wananchi kuwa sikuleta maendeleo kwa sababu mlikosea kuchagua !! eg Moshi, Kilwa , Bunda nk .

Rais hafai kuongea hayo
Lazima ujiulize kwanini mzalendo anasema hivyo.

Uzoefu wa hao wa Moshi na Kilwa ni kwamba muda mwingi wao ni kususa bungeni na kutoka nje au ni kushinda mahakamani kisutu wakihangaishana na kesi.

Wananchi wanaowapigia kura wanakosa haki yao ya kuwa karibu na watu waliowapigia kura.

Mbunge mwenye kuwajali watu wake atajiepusha na mazingira ya kufunguliwa kesi mara kwa mara kwani atatambua thamani ya kura alizopigiwa.
 
Kesi walizo nazo hao ni za uchochezi ambazo nazo ni za kubumba .

Kiongozi wa nchi ukishaapa hutakiwi kuwa mbaguzi kwa sababu yoyote ile. Majimbo mengi yalio chini ya Ccm ni duni kuliko hata hizo zinazoongozwa na wapinzani.
 
Kesi walizo nazo hao ni za uchochezi ambazo nazo ni za kubumba .

Kiongozi wa nchi ukishaapa hutakiwi kuwa mbaguzi kwa sababu yoyote ile. Majimbo mengi yalio chini ya Ccm ni duni kuliko hata hizo zinazoongozwa na wapinzani.
Rais anataka ushirikiano na wabunge kwa faida ya mwananchi wa kawaida.

Kumbuka kuwa rais ni mtumishi mkuu wa mwananchi wa kawaida kabisa anayo haki ya kumkumbusha juu ya umuhimu wa kutopoteza kura yake.

Rais kama kiongozi mkuu wa taifa anao wajibu wa kunkumbusha kila mpiga kura kuhusu masuala yanayomcheleweshea maendeleo yake na suala la wabunge baadhi kujikita kwenye uanaharakati ni jambo ambalo mwananchi ni lazima aelezwe.
 
Kwani katiba inasemaJe kuwa multiparty system . Je halmashauri zinazoongozwa vyama vingine na si Ccm katiba inasemaJe ?!.

Nimeishi wakati wa Mwl Nyerere . Hakuwahi kuropoka . Hata kama jambo hakulipenda alitafuta lugha nzuri ya kuwakanya. Lakini si kuwabagua kwa lugha zenye ukakasi .
 
Tafsiri ya lugha za ukakasi ni ya mtu mmoja mmoja cha muhimu ni ujumbe kuweza kufikishwa na kueleweka.

Kwamba wapo wanaharakati na wapo wanasiasa makini wenye kuhangaikia maisha ya watu.
 

Kwa kuwa viongozi wa upinzani wanapenda kudai kuwa utawala wa sasa hafuati Katiba, ni dhahiri kuwa hwaijui na hivyo basi wanajidharilisha. Soma Katiba ya JMT (1977), Ibara ya 30.-(1) Haki na uhuru wa binadamu ambavyo misingi yake imeorodheshwa katika Katiba hii havitatumiwa na mtu mmoja kwa maana ambayo itasababisha kuingiliwa kati au kukatizwa kwa haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma.

Katika miaka 5 ya utawala wa Serikali ya CCM, inayomaliza muda wake, tumeshuhudia Wabunge wakisusia vikao vya bunge na kutokupitisha bajeti. Pia tumeshuhudia Wabunge na Madiwani kutokutoa ushirikiano kwa watendaji wa Serikali. Kimsingi, maana vitendo hivyo (kinyume na Katiba) vililenga kukamwisha maendeleo ili wananchi waichukie Serikali.

Serikali, pamoja na nia ovu hiyo ya kukwamisha maendeleo, bila kujali, ilitekeleza miradi ya maendeleo katika Kata na Majimbo ya upinzani. Upinzani kuona hivyo, umebadili nia yao ovu na kudai miradi ya maendeleo iliyotekelezwa ni ya "vitu" siyo ya "watu".

Je, katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu, wameweza kueleza maendeleo ya watu ni yapi na miradi yake itakuwa ipi? Kinachoendelea katika kampeni za Lissu, Mgombea wao wa Urais, ni kumdhihaki na kumkejeli Rais aliyeko madarakani, akiamini ndiyo turufu ya yeye kuchaguliwa. Tunategemea, kama ulivyosema, kiongozi awe na lugha nzuri ya kuwasilisha hoja zake hata kama ni amri, nikinukuu Nimeishi wakati wa Mwl Nyerere . Hakuwahi kuropoka . Hata kama jambo hakulipenda alitafuta lugha nzuri ya kuwakanya.

Pasipo shaka Lissu ni punguani au msomi uchwara. Akili zake zimejaa takataka na wanaomshabikia ni Wapumbavu na Malofa
 
Mawazo mgando....

Kwani we' unaishi nchi gani kama hujayaona haya waziwazi...!?
 
Kwa Jamii ya watu walioelimika na kustaarabika asingepata hata umonita darasani Hana ethics za leadership
Hadi leo huwa nawaza sijui Mkapa na jopo lake waliwaza nini kutuletea mtu katili namna hii....

Na kwa upande wa pili wa shilingi,
Ukawa hasa Chadema hawatokaa waamini kwa kitendo cha ki-huni alichowafanyia ma-Mvi, maana pale Slaa Wilbrod alikuwa anakabidhiwa nchi.

Tulikosewa Sana wapenda mageuzi.
 
umeandika vema lakini hujatuambia badala yake tumchague nani na kwa sababu gani? vinginevyo Magufuli tano tena.
 
Duu hii ya kuishi Kama mashetani noma ndo naisikia

Bora hiyo mkuu akiwa waziri aliwahi kuulizwa ukiwa Rais utaifanyieje nchi yako.
Namnukuu alisema "Nikiwa Rais watanzania watalima kwa Meno"

Lissu alisema tuna Rais wa ajabu ajabu haijawahi kutokea tukamdharau.

Wakati ni sasa watanzania tuamke huyo mtu wa ccm hafai hafai hata kwa uvumba.
 
Umenifokea kweli Mwengeso !!. Hata umenukuu katiba mbovu lakini pia hamuifuati .
Hivi nikuulize lugha ya Kilwa ilifaa kweli ?!. Unaulizwa mkwamo wa unenzi wa stand , halafu unasema shauri yenu na Bwege wenu !!. Unaombwa maji Bunda halafu unasema mimi siwezi kuwanyima wanangu chakula nikawape wa jirani ?!. Mbona kodi zao unakusanya na kuweka kwenye kapu kubwa (hazina) ?!. Unaombwa barabara moshi halafu unasema safari nyingine mjue namna ya kuchagua ?!.

Ndiyo maana nika refer uongozi wa Mwl Nyerere . Uliwahi kufanyika uchaguzi mdogo huko Arusha , nadhani ni Karatu , pamoja na kuendako yeye kama Rais, amiri Jeshi na mwenyekiti wa Tanu . Lakini bado wananchi walimchagua mgombea binafsi Mr Sarwat . Mwl Nyerere aliwaheshimu wale wananchi na akaichukulia Ile kama challenge ndani ya chama chake na hakuwabagua. Sasa huyu wetu anayewabagua watu kwa sababu wameikataa Ccm Je ??!!.

Lugha ya Lissu ni kali kwa sababu alivyotendewa si kibinaadamu . Alipaswa kuombwa radhi hata kwa mlango wa nyuma.
 
Waache wamchague, ila mimi na nafsi yangu sintamchagua ili nisibaki na ningejua...!
 
Hizi CD zenu mmeziimba 4 five years zimesha chuja sana. Tukiwaambia maccm hamna jipya, muwe mnaelewa.
 
Media zinapiga kura? Akili zingine bana, bora hata za mbuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…