Sababu gani zitakufanya usipige Kura zoezi la Uchaguzi litakapofika?

Sababu gani zitakufanya usipige Kura zoezi la Uchaguzi litakapofika?

Binafsi sio uchaguzi huu ujao tu, sitokaa nipige kura tena maisha yangu yote kama mambo yatabaki kuwa hivihivi na sheria zao mbovu za uchaguzi.

Kitu pekee nitafanya ni kujiandikisha nipate kitambulisho basi maana kinasaidia sometimes.
 
Hebu leo tushirikishane

Kwanini wengi wanaona kwenda kupiga kura ni kupoteza Muda?
Tanzania hakuna uchaguzi, bali Kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura. Ni mtu mjinga tu atapanga mstari kwenye box la kura huku Kuna kigenge kinajiita system kinapanga nani atangazwe mshindi. Kwa jinsi wapinzani wanavyoumizwa, kubambikiwa kesi, kura kuchezewa, ni ujinga wa dhahiri kuendelea kushiriki uchaguzi ambao mwenyekiti wa ccm asiye na maadili, ndio muamuzi wa matokeo.
 
Kupiga kura kwa nchi za kiafrika hasa Tanzania ni kupoteza muda na pia ni dhambi kubwa sana maana ni kama kushiriki Maovu yanayoleta laana maana mchakato wake ni dhalimu na usio fuata misingi ya haki.

Tunaweza jiuliza kwa nini watanzania tuna maisha magumu kumbe huwa tuna shiriki katika maovu bila kujua .. moja wapo ni kushiriki katika chaguzi kama hizi.
 
Mkuu Nifah sasa yule jamaa yetu atapitaje......chini ya katiba hii yenye viraka kila mahali nami nitabaki nyumbani....
 
Hebu leo tushirikishane

Kwanini wengi wanaona kwenda kupiga kura ni kupoteza Muda?
Kwa upande wangu sitokuja kushiriki hilo zoezi kwa sababu kuu zifuatazo:-

1) Tume ya uchaguzi haina uhuru kwa sababu inateuliwa na Mwenyekiti wa chama tawala.

2) Wakurugenzi wa Halmashauri/Miji/ Manispaa, nk wote ni Makada wa CCM na wanayeuliwa na Mwenyekiti wa CCM! Halafu wamepewa jukumu la kuwa wasimamizi ngazi ya Wilaya.

3) Matokeo ya Rais yakishatangazwa, hata yawe feki au yawe na dosari! Bado hayawezi kupingwa mahali popote pale mfano Mahakamani, nk.

4) Vyombo vya dola mfano polisi na usalama wa Taifa wamekuwa wakitumiwa waziwazi kwenye kukinufaisha chama tawala kwa kuwatisha wapiga kura na wagombea wake, kuwalinda Wakurugenzi wanaowatangaza wagombea ambao hawakushinda kihalali, nk.

5) Mara nyingi mshindi wa uchaguzi amekuwa akijulikana hata kabla ya matokeo. Kwa mfano mgombea wa Urais kupitia CCM akishapitishwa na chama chake; tayari huyo anatambulika kuwa Rais mtarajiwa hata kabla ya zoezi la uchaguzi kufanyika.

Kutokana na hizi sababu zangu hapo juu; aisee kupiga kura ni majaliwa. Ni mpaka hapo nitakapo jiridhisha kura yangu itaheshimiwa.
 
Sina mpango tena wa kuidhinisha ufisadi wa kitaasisi kupitia sanduku la kura.
Nitashiriki kupiga kura baada ya nchi hii kupata uhuru kamili kutoka kwa wakoloni weusi.
 
Back
Top Bottom