Village-in
JF-Expert Member
- Aug 30, 2022
- 2,184
- 4,517
Ccm watawachukua wanafunzi wawapangishe mistari mirefu kuhalalisha upigaji wao
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe ni mimi mtupu yani niache shughuli zangu au kupumzika nikafanye ujinga never hii nchi tumuachie mungu tu maji shida umeme shida sasa nipige kura ili isaidie nini kweliBinafsi sio uchaguzi huu ujao tu, sitokaa nipige kura tena maisha yangu yote kama mambo yatabaki kuwa hivihivi na sheria zao mbovu za uchaguzi.
Kitu pekee nitafanya ni kujiandikisha nipate kitambulisho basi maana kinasaidia sometimes.
Umejieleza vizuri sana; hata mimi katika mazingira hayo siwezi kupiga kura.Kwa upande wangu sitokuja kushiriki hilo zoezi kwa sababu kuu zifuatazo:-
1) Tume ya uchaguzi haina uhuru kwa sababu inateuliwa na Mwenyekiti wa chama tawala.
2) Wakurugenzi wa Halmashauri/Miji/ Manispaa, nk wote ni Makada wa CCM na wanayeuliwa na Mwenyekiti wa CCM! Halafu wamepewa jukumu la kuwa wasimamizi ngazi ya Wilaya.
3) Matokeo ya Rais yakishatangazwa, hata yawe feki au yawe na dosari! Bado hayawezi kupingwa mahali popote pale mfano Mahakamani, nk.
4) Vyombo vya dola mfano polisi na usalama wa Taifa wamekuwa wakitumiwa waziwazi kwenye kukinufaisha chama tawala kwa kuwatisha wapiga kura na wagombea wake, kuwalinda Wakurugenzi wanaowatangaza wagombea ambao hawakushinda kihalali, nk.
5) Mara nyingi mshindi wa uchaguzi amekuwa akijulikana hata kabla ya matokeo. Kwa mfano mgombea wa Urais kupitia CCM akishapitishwa na chama chake; tayari huyo anatambulika kuwa Rais mtarajiwa hata kabla ya zoezi la uchaguzi kufanyika.
Kutokana na hizi sababu zangu hapo juu; aisee kupiga kura ni majaliwa. Ni mpaka hapo nitakapo jiridhisha kura yangu itaheshimiwa.
Mkuu, ya Rwanda na Kagame yaache huko huko. Tunajua tumekwama chini ya CCM, lakini hizo stori za Rwanda na Kagame achana nazo. Hazitufai kabisa.Kila sekta iliyoshikwa na ccm imefeli kuanzia uchumi, biashara, barabara mbovu wakandarasi matapeli wa kichina wanajenga zinaharibika , maji hakuna pamoja na kusifiwa kote kwa awesu mkwe wa mama
umeme ndio kizungumkuti mpaka watu wanatamani magufuli JP asingekufa umeme usingechezewa na wahuni.
Nauli zimepanda ili hali mishara haitopanda na haiakisi maisha ya watu, mwendokasi tuu imewashinda.
Upo wakati tukisoma success stories za Rwanda huwa tunatamani kagame angekuwa raisi wetu tungekuwa na maisha mazuri kama 2nd world semi periphery nations. Ame attract a lot of viable investment to his country simply kwa ku set standards procedure na sio kujipeleka kwenye conferences kila siku. Angalia uwekezaji wa NBa rwanda, Volkswagen, Renault, Univeristies za maana, Business incubators, hotel ndio usiseme na sasa asylum seekers wanaokwenda UK wataishi rwanda vizuri tuu.
Na wala huna muda wa kufikiri na/au kuunga mkono juhudi za kuwaondoa CCM madarakan!Kwa katiba hii na Tume hiyo huo muda sina kwa kweli.
Umewahi kujiuliza huo "Uhuru" utapatikana kwa njia zipi?Sina mpango tena wa kuidhinisha ufisadi wa kitaasisi kupitia sanduku la kura.
Nitashiriki kupiga kura baada ya nchi hii kupata uhuru kamili kutoka kwa wakoloni weusi.
Sababu ya kwanza kabla ya kupiga kura mshindi teari anajulikana lakini pili Tanzania kuna semwa ni nchi inayofuata mfumo wa vyama vingi lakini sheria za uchaguzi zilizopo za mfumo wa chama kimoja yani kupiga kura nchi hii sawa sawa unauliza mwanamke anajinsia gani wataki ushasema mwanamke halafu unauliza jinsia gani ndio sawa sawa kwenda kupiga kura kumchagua mgombea unaemtaka halikua anetangazwa mshindi unamjuaHebu leo tushirikishane
Kwanini wengi wanaona kwenda kupiga kura ni kupoteza Muda?
Swali zuri sana hili. Kama wote tunaokiri kuliona tatizo tungeungana na kukubaliana kwa kauli moja kuwa 2025 tukaiondoe CCM, mimi ningekuwa wa kwanza kupanga foleni kutekeleza, Lakini sioni kwenye upinzani chama au mtu wa kumwamini kama mwenye nia ya kutenda kwa maslahi ya nchi, wengi kulingana na program zao, kauli zao na hata matendo yao hayatofautiani sana na watawala wa sasa. Itachukua muda kwa watu kuelimika zaidi kuwa hatujapata uhuru bado na kadiri tutakavyokuwa wengi walio hamasika itakuwa rahisi kulisukumia kuzimu hili gogo CCM.Umewahi kujiuliza huo "Uhuru" utapatikana kwa njia zipi?
Kwa nini uhalifu wanao ufanya CCM wakati wa chaguzi isiwe chachu ya kutafuta huo uhuru? Mbona hii ni sababu nzuri kabisa ya kupambania huo uhuru. Kwa nini tusiitumie hii hii.
Nifah: Unafanya kosa kubwa sana kususia hata kama kuna udanganyifu, wizi na dhuruma ktk uchaguzi. Husisusie haki bali itafute na kuipigania. Wewe kapige alafu linda kura yako lah kama uwezi ache wao waibe, ingawa hawana aibu ktk wizi wao lakini tukipiga wengi mwishowe zitawashinda kuiba. Haki itafute, ipiganie na kuilinda, lakini ukiacha au kususa, utawafanya hao wanaodhurumu wajione washindi na kuendelea kufanya watakavyo..Binafsi sio uchaguzi huu ujao tu, sitokaa nipige kura tena maisha yangu yote kama mambo yatabaki kuwa hivihivi na sheria zao mbovu za uchaguzi.
Kitu pekee nitafanya ni kujiandikisha nipate kitambulisho basi maana kinasaidia sometimes.