Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Elimu duni, rushwa,kukata tamaa sababu ya watawala,wizi wa kura nkHebu leo tushirikishane
Kwanini wengi wanaona kwenda kupiga kura ni kupoteza Muda?
Yupo sahihi Hundred per se %Upigaji kura wa Tanzania👇
View attachment 2840329
GwaB: Umetekwa na propaganda za chawa wa CCM. Ni sera zipi unataka uzisikie toka kwa vyama vya upinzani? Vyama vinaundwa na nani kama siyo Mimi, wewe, yule na wao? Usisubiri mwingine akufanyie na wewe shiriki ktk kufanya. Kila mmoja wetu anayo haki na wajibu wa kufanya jambo kwa taifa letu.Swali zuri sana hili. Kama wote tunaokiri kuliona tatizo tungeungana na kukubaliana kwa kauli moja kuwa 2025 tukaiondoe CCM, mimi ningekuwa wa kwanza kupanga foleni kutekeleza, Lakini sioni kwenye upinzani chama au mtu wa kumwamini kama mwenye nia ya kutenda kwa maslahi ya nchi, wengi kulingana na program zao, kauli zao na hata matendo yao hayatofautiani sana na watawala wa sasa. Itachukua muda kwa watu kuelimika zaidi kuwa hatujapata uhuru bado na kadiri tutakavyokuwa wengi walio hamasika itakuwa rahisi kulisukumia kuzimu hili gogo CCM.
Mbussi; Nikupe taarifa tu kuwa kamwe siwezi kutekwa na laghai za vyama au wanasiasa. Kama kuna chawa wa CCM wanajaribu kurubuni watu kwa propaganda nikuhakikishie tu kuwa sidanganyiki na katika maeneo ninayoishi wanafahamu kuwa sina hizo za vyama.GwaB: Umetekwa na propaganda za chawa wa CCM. Ni sera zipi unataka uzisikie toka kwa vyama vya upinzani? Vyama vinaundwa na nani kama siyo Mimi, wewe, yule na wao? Usisubiri mwingine akufanyie na wewe shiriki ktk kufanya. Kila mmoja wetu anayo haki na wajibu wa kufanya jambo kwa taifa letu.
Kwa kawaida nchi ina malengo ya muda mrefu na mfupi. vyama vya siasa utunga sera na kutafuta ridhaa ya kutimiza malengo yaliyokwisha wekwa. Serikali ya CCM ina sera mbovu sana na ndiyo maana kila Rais anapoingia madarakani uachana na mipango pamoja na miradi mikubwa ya kitaifa iliyoachwa na mtangulizi wake. Kwao wao mwenye sera ni mtu siyo chama. Chunguza, chambua na tafakari, kwasasa hivi hakuna chama cha ovyo Tanzania kama CCM, viongozi wake wapo kwa ajili ya kugawana kilichopo.
Binafsi nawashauri MSIPIGE KABISA KURA Ili CCM ishinde (maana mimi nitapiga) na iendelee kubaki madarakani ili nchi iendelee kuwa na amani na maendeleo.Hakuna namna, ni kupoteza muda tu.
CCM imekula matunda ya uhuru na kwa sasa wameamua kuula uhuru wenyewe...prof.Mbussi; Nikupe taarifa tu kuwa kamwe siwezi kutekwa na laghai za vyama au wanasiasa. Kama kuna chawa wa CCM wanajaribu kurubuni watu kwa propaganda nikuhakikishie tu kuwa sidanganyiki na katika maeneo ninayoishi wanafahamu kuwa sina hizo za vyama.
Mawazo yangu ni huru kabisa na sihitaji usaidizi katika kufanya maamuzi.
Nchi hii inakwenda mrama kwa kuwa CCM ambayo ni ya hovyo inaendelea kutesa kwa kuwa hatuna vyama mbadala wa CCM, tuna vyama na wanasiasa wanaoibuka wakati wa uchaguzi ili waiingie kwenye nafasi za maamuzi yatakayo wanufaisha wao binafsi na sio Kama taifa.
Mimi naamini kuwa safari ya kutafuta uhuru wa nchi hii bado ni ndefu sana maana CCM ndio imechukua nafasi ya wakoloni kwa miaka zaidi ya 60.
Wewe ni miongoni mwa chawa waliokaririshwa neno "amani" bila kujitambua. Amani itaenda wapi kama chama pinzani kikichukuwa dola? CCM imejiandaa kwenda msituni baada ya kupoteza? Usikariri yanayosemwa na wanasiasa majukwaaniBinafsi nawashauri MSIPIGE KABISA KURA Ili CCM ishinde (maana mimi nitapiga) na iendelee kubaki madarakani ili nchi iendelee kuwa na amani na maendeleo.
Tulianza kuona matumaini chini ya CHADEMA.Swali zuri sana hili. Kama wote tunaokiri kuliona tatizo tungeungana na kukubaliana kwa kauli moja kuwa 2025 tukaiondoe CCM, mimi ningekuwa wa kwanza kupanga foleni kutekeleza, Lakini sioni kwenye upinzani chama au mtu wa kumwamini kama mwenye nia ya kutenda kwa maslahi ya nchi, wengi kulingana na program zao, kauli zao na hata matendo yao hayatofautiani sana na watawala wa sasa. Itachukua muda kwa watu kuelimika zaidi kuwa hatujapata uhuru bado na kadiri tutakavyokuwa wengi walio hamasika itakuwa rahisi kulisukumia kuzimu hili gogo CCM.
Dogo usinitilie maneno mdomoni. Wapi nimesema wapinzani wakichukua madaraka "amani" itatoweka? Nioneshe!Wewe ni miongoni mwa chawa waliokaririshwa neno "amani" bila kujitambua. Amani itaenda wapi kama chama pinzani kikichukuwa dola? CCM imejiandaa kwenda msituni baada ya kupoteza? Usikariri yanayosemwa na wanasiasa majukwaani
Wapo waTanzania wa kutosha sana waliohamaki kutokana na matendo yanayofanywa na CCM.. Itachukua muda kwa watu kuelimika zaidi kuwa hatujapata uhuru bado na kadiri tutakavyokuwa wengi walio hamasika itakuwa rahisi kulisukumia kuzimu hili gogo CCM.
Kuzacsizo zinazoamua nani awe raisi au mbunge. Rais na tume ndo wanaamua kwa hiyo niende kupiga kura ili iweje?Hebu leo tushirikishane
Kwanini wengi wanaona kwenda kupiga kura ni kupoteza Muda?
Ccm inashinda ikishindana na nani? Watu hawana muda wa kushiriki ukhanithi, na Isitoshe sio lazima viongozi wapatikane kwa njia ya kura. Hiyo njia ya kura ya njia ya kistaarabu, ambayo mmeshindwa kuiheshimu. Itatafutwa njia nyingine bila kujali madhara yake.Binafsi nawashauri MSIPIGE KABISA KURA Ili CCM ishinde (maana mimi nitapiga) na iendelee kubaki madarakani ili nchi iendelee kuwa na amani na maendeleo.
Sasa kelele za nini? Kaeni kimya sie tukapige CCM iendelee kutawala. Period!Ccm inashinda ikishindana na nani? Watu hawana muda wa kushiriki ukhanithi, na Isitoshe sio lazima viongozi wapatikane kwa njia ya kura. Hiyo njia ya kura ya njia ya kistaarabu, ambayo mmeshindwa kuiheshimu. Itatafutwa njia nyingine bila kujali madhara yake.