Sababu gani zitakufanya usipige Kura zoezi la Uchaguzi litakapofika?

Sababu gani zitakufanya usipige Kura zoezi la Uchaguzi litakapofika?

Halafu nikapigwe jua kutwa nzima , my last vote ilikua kwa hayati Magufuli na nashukuru kura yangu haikupotea, na kule kuungua na jua hakukua kwa bure tu walao tuna la kuwaambia wajukuu zetu alikuwepo Magufuli wakati fulani.
Tuliwazidi kete tukamuua
 
Hebu leo tushirikishane

Kwanini wengi wanaona kwenda kupiga kura ni kupoteza Muda?
Unaenda kupiga Kura wakati wenzio walishaandaa na matokeo tayari.

Hivi tunavyoongea CCM wameshajipangia na asilimia za ushindi.

Hata mtakayemchagua hatatangazwa.

KITUKO:
Mmoja wa wagombea (CCM) ndiye anayeteua wasimamizi wa uchaguzi/wajumbe wa tume ya uchaguzi.

Katika kuteua anateua kimkakati, watu watakaolinda maslahi yake.

Mahakamani utawakuta majaji walioteliwa na mgombea (CCM)mmoja wapo.

KWANINI KUPOTEZA MUDA? SIONI HAJA YA U HAGUZI.

Akishinda mpinzani simu zinapigwa ngazi za juu km atangazwe au la na Lazima wananchi washinikize na hata fujo ndiyo pinzania atangazwe.

NILISHAACHA HUO UPUUZI WA KUOIGA KURA. SIDHANI KM KUNA WA KUNISHAWISHI!
 
Tanzania kuleana kumezidi inatakiwa zikiibiwa kura wapinzani waseme bhasi liwalo na liwe .
 
Hebu leo tushirikishane

Kwanini wengi wanaona kwenda kupiga kura ni kupoteza Muda?
1.Kiongozi anakuwa "selected" by the establishment,kwa hiyo wanayemtaka wananchi hawezi kupita.
2.Kuna ballot fraud sana, ili kuhakikisha kwamba aliyekusudiwa na establishment ndiye anayepita.
3.Hakuna tume huru.
Wasimamia uchaguzi ni waajiriwa serikalini, kwa hiyo it is impossible kuwa impartial,kwa kuwa lazima watampendelea muajiri wao.

Simply put it,uchaguzi is a sham,kwa hiyo a waste of resources.
 
Tukae kimya kwa sababu yenu nyie majizi ya kura?!
Sasa ukiropoka "sioigi kura, sipigi kura" inanizuia mimi nisipige? Mligomea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019, imewazuia Wenyeviti waliopo kufanya kazi? Na mwakani susieni muone kama Serikali itashindwa kuwepo na kufanya kazi zake! Alaaah!!!
 
Nlipokua advance ku mwanangu aligombea uongozi wa bweni, mim sikuepo bwenin mda wa kupiga kura, si kwamba sikua na taarifa bali nliamini kwa namna yotote uwepo au kutokuwepo kwangu hakuwezi kua na madhara,

Nmerudi ktoka kitaa nakuta mwenyekiti wa uchaguzi anatangaza matokeo, na ktk matokeo yale yamaa angu alishindwa kwa kura 1, nliumia sana maake mwamba alikua na uwezo wa kuvusha msosi kweny chamber yetu.

nlichojifunza, hasira za kutoshiriki kabisa uchaguzi zinaweza kua na impact hasi ktk maisha kwa ujumla.
Hebu leo tushirikishane

Kwanini wengi wanaona kwenda kupiga kura ni kupoteza Muda?
 
Sasa ukiropoka "sioigi kura, sipigi kura" inanizuia mimi nisipige? Mligomea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019, imewazuia Wenyeviti waliopo kufanya kazi? Na mwakani susieni muone kama Serikali itashindwa kuwepo na kufanya kazi zake! Alaaah!!!
Serekali hata kwenye nchi zilizopinduliwa zipo, sasa sijui unaongea Nini. Tunazungumzia serekali zenye uhalali wa umma, sio Bora serekali.
 
Serekali hata kwenye nchi zilizopinduliwa zipo, sasa sijui unaongea Nini. Tunazungumzia serekali zenye uhalali wa umma, sio Bora serekali.
Kwa Tanzania p, hilo la "kioinduliwa" hata wajukuu zako watapata wajukuu bila kutoka Tanzania, labda apinduliwe Mbowe! Ahahahahaha!
 
Kwa Tanzania p, hilo la "kioinduliwa" hata wajukuu zako watapata wajukuu bila kutoka Tanzania, labda apinduliwe Mbowe! Ahahahahaha!
Nyerere mwenyewe aliyekaa madarakani Hadi katiba ikatungwa kumfurahisha alitaka kupinduliwa, ndio itakuwa haya majizi?
 
Na mwisho utasikia
Huyu ni chaguo la Mungu
Kura yako ishapuuzwa tayari,
Sasa kama ni chaguo la Mungu kupiga kura Kuna faida gani sasa?
 
CCM tunashinda uchaguzi asubuhi maana wapiga kura wa vyama vya upinzani wanajificha siku ya kupiga kura sisi tunajitokeza,
 
Sitopiga kura, kwakuwa nimekosa imani kwa mchakato mzima wa kupatikana kwa tume, wasimamizi wa vituo, utangazaji wa matokeo, na kadhalika.
 
Nyerere mwenyewe aliyekaa madarakani Hadi katiba ikatungwa kumfurahisha alitaka kupinduliwa, ndio itakuwa haya majizi?
Sina hakika kama unajua unachoandika. Au una stress za CCM kutawala nchi hii? Si utakufa mapema, maana CCM ipo Jana, leo, kesho, kesho kutwa na mtondogoo!!
 
Sina hakika kama unajua unachoandika. Au una stress za CCM kutawala nchi hii? Si utakufa mapema, maana CCM ipo Jana, leo, kesho, kesho kutwa na mtondogoo!!
Sijui, kwakuwa ww umekuja na marking scheme unaweza kusahihisha kutokana na maelezo uyatakayo.
 
Back
Top Bottom