Sababu ya watu kuogopa kutoa ushahidi kwenye baadhi ya matukio aliyo shuhudia live na wengine baadhi hukimbia kabisa

Sababu ya watu kuogopa kutoa ushahidi kwenye baadhi ya matukio aliyo shuhudia live na wengine baadhi hukimbia kabisa

Natumaini wote mko poa ndg wana JF,, lakini poleni sana kwale wote wenye changamoto yoyote ya kiafya au maisha kwa ujumla poleni sana Mungu awasaidie mkae sawa [emoji120]

Ndg zangu nimeamua kuandika uzi huu kutokana na mambo yanayo fanyika kwenye jamii zetu haya mambo yanaumiza sana[emoji24] mitaani kumekuwa na vifo vingi sana vya watu baadhi vinaeleweka vizuri na wana jamii huku vingine vikiwa ni vya kuhisiwa tu kuwa huenda amefanywa hivi au

Lakini la kusikitisha zaidi kuna kuwa na watu wanao shuhudia kabisa mwanzo wa tukio mpaka mwisho lakini wanakausha kama vile hawajaona chochote ila mtu ndio tyr kafa hivo inabaki tu minong'ono ya chini chini wakifika polisi hao watu hujitenga kabisa tena wengine huondoka kabisa eneo la tukio,,, haya yote hutokea kwa sababu ya sheria na mifumo kwa askari walio wengi, shahidi akijitokeza kutoa ushahidi wake wana shughulika zaidi na huyo shahidi kuliko kushughulikia tukio zima yani yanageuka kuwa majuto kwa mtoa ushahidi hawafikirii kuwa huyo mtu ameguswa na matukio yanayo fanywa na baadhi ya watu wao hufikiria mtoa taarifa kuwa ana kiherehere kwahiyo wanakula sahani moja na shahidi tumeshuhudia watu wengi walio jaribu kusaidiana na askari kushughulikia waharifu lakini mwisho wa siku shahidi ndio anakuwa mwaharifu yaani,, yani askari badala ya kumpongeza mtoa ushahidi lakini wao wana mchallenge kupita kawaida hadi mwisho wa siku shahidi anashindwa anakuwa mtuhumiwa mwenyewe

Kwa kifupi hiyo ndio taswira tu ya mambo yanayo endelea kwenye jamii hadi kwenye suala la vifo kutoa ushahidi inakuwa ni kiherehere

Kuna siku moja nilipita barabara flani hivi nilikuta mtu amegongwa na gari gari lililo mgonga huyo bwana lilikuwa limepitiliza haraka kwahiyo halikueleweka kuwa ni gari gani japo kuna wengine walilitambua hilo gari lakini walikausha, huyo bwana alikuwa liye gongwa alikuwa amebaki pale barabarani hakuna mtu aliye msogelea wala kumgusa na vyombo vingine vya usafiri viliendelea kumkwepa akiwa pale pale,, mimi nilivoona watu wanashangaa tu hawataki kuenda kumsaidia nilijaribu kuwa hamasisha "jamani tuendeni tumsaidie mwenzetu..." watu walisema wanaogopa wakimgusa yule bwana eti wataacha alama za vidole itaonekana wao ndio wameua [emoji24][emoji24] kwahiyo tuliendelea kumshangaa pale huku wengine wakihangaika kuwaita polisi mwisho mimi uvumilivu ulinishinda niliamua kuenda hivo hivo bahati nzuri kuna jamaa mwingine alikuwa ameguswa na hilo tukio yeye alikuwa ana bajaji kwahiyo tulimbeba yule hadi hospitalini alikuwa bado hajapoteza maisha ila alikuwa amepoteza fahamu,, lakini kitu kingine cha ajabu tulivo mfikisha hospitalini tulijielezea na kueleza hali ilivo kuwa madaktari wakasema huu msalaba tunaubeba sisi tulio mpeleka pale kwa kuna gharama tulitakiwa tulipe kwa sababu haikujulikana kama ana bima au la! hivo sisi tulitakiwa kuullipia gharama zinazo husika kwenye ufunguaji wa faili bahati mbaya sana hiyo siku mimi na mwenzangu hatukuwa na hela za kutosha kulipia pale kwahiyo mgonjwa aliwekwa kando kwa muda 🥲 tukisubiri ndg zake waje na hii kesi siku sikia lolote mpaka sasa wala haikusemwa popote wala hakuna askari yeyote akijihusisha na hili tukio

Hii ndio hali halisi zinazo endelea kwenye jamii, watu wanaogopa kushiriki kwenye kutoa ushahidi hatakama mtu amepatika amekatwa katwa mapanga ikionekana tu uwezekano wa kupona huyo mtu ni mdogo watu wanakula kona,,

Mimi nimeandika tu huu uzi wala sifahamu kama unaweza kubadilisha chochote 🥲 lakini huku kwenye jamii zetu kumejaa maovu sana kama kuna mtu upo kwenye cheo fulani huko serikalini au upo kwenye harakati hizo nawaombeni mlitazame hili pia [emoji52] raia wanateseka sana watu wanapoteza ndugu zao bila sababu zozote za msingi HII AMANI INAYOSEMEKANA KUWA NCHI INA AMANI TUNATAMANI IWE NI AMANI YA KWELI KWA RAIA WOTE

Asanteni sana kwa kuvumilia kusoma huu uzi [emoji120][emoji120] naamini nimeeleweka maana yangu ni ipi
Mkuu ni kweli kabisa hii hali

Mi ilikua hivi
Mida ya usiku kama sa mbili kuna bodaboda alikua mbele yangu mi nna kibajaji sasa mbele kuna Lori lilikua bovu halina reflecta wala halijawasha taa sas yule boda hakuliona akaligonga kwa nyuma akaanguk hp hp na kupoteza faham watu walikuj wengi kushuhudia ila hawakutaka kumbeba bahT nzuri mm nikajitolea kumplek hospital ila baada ya jamaa kupandushwa kweny bajaj kila mtu akpita na njia zake hawatki ushahid bahat akatokea jamaa tu muokt kopo tukaend nae hospt na mgonjwa

Tumefk hospital wakagom kumtib had tuend polis kuchukua pf3. Tumefika polisi wanaanz kutuuliza jamaa anaitwa nani anakaa wap na maswali personal kibao na sis hatumjui ...tukajieleza tumerudi tena hospital nao wanatak hela za kufungua file na matibabu ..kiukwel polisi na mahospitali inabidi suala la ajali liangaliww uppya watu wanaacha kusaidia watu kwa kukwepa kubeba mizigo juu ya mizigo labda kama jamaa angekata moto naona kabisa mimi na muokta kopo tungewekwa ndani kwa ajili ya ushahidi

Tunaomba sheria au sera za majanga au ajali ziangaliwe upya ..pia ikiwezekqna pf3 ziwepo hospital na sio polisi

Asante
 
Inasikitisha sana,. Kuna jamaa yangu alienda kuripoti kituoni kuwa ameibiwa simu akaandikiwa RB kisha akaambiwa kesho urudi,. Kweli siku iliyofuata jamaa alienda tena kituoni cha ajabu akaishia kuulizwa " umefikia wapi kutafuta simu yako." yani kiufupi yeye ndo akageuka kuwa mpelelezi.
 
Mkuu ni kweli kabisa hii hali

Mi ilikua hivi
Mida ya usiku kama sa mbili kuna bodaboda alikua mbele yangu mi nna kibajaji sasa mbele kuna Lori lilikua bovu halina reflecta wala halijawasha taa sas yule boda hakuliona akaligonga kwa nyuma akaanguk hp hp na kupoteza faham watu walikuj wengi kushuhudia ila hawakutaka kumbeba bahT nzuri mm nikajitolea kumplek hospital ila baada ya jamaa kupandushwa kweny bajaj kila mtu akpita na njia zake hawatki ushahid bahat akatokea jamaa tu muokt kopo tukaend nae hospt na mgonjwa

Tumefk hospital wakagom kumtib had tuend polis kuchukua pf3. Tumefika polisi wanaanz kutuuliza jamaa anaitwa nani anakaa wap na maswali personal kibao na sis hatumjui ...tukajieleza tumerudi tena hospital nao wanatak hela za kufungua file na matibabu ..kiukwel polisi na mahospitali inabidi suala la ajali liangaliww uppya watu wanaacha kusaidia watu kwa kukwepa kubeba mizigo juu ya mizigo labda kama jamaa angekata moto naona kabisa mimi na muokta kopo tungewekwa ndani kwa ajili ya ushahidi

Tunaomba sheria au sera za majanga au ajali ziangaliwe upya ..pia ikiwezekqna pf3 ziwepo hospital na sio polisi

Asante

Sasa hapa ndio tunapata picha kamili jinsi haya matendo yanavo athiri jamii kwa ujumla
 
Hili kwakweli lipo aisee .
Hata mimi kuna tukio ilibidi tu nicheze part ya kumfikisha mtu kwenye sehemu salama na nikimbie nikabaki mtazamaji wa mbali tu aisee . Polisi siwaamini kabisa .
Muhimu kama unaweza kuokoa maisha jitahidi okoa maisha

Kama unaona kuna mtu anaenda kuonewa kwa wewe kutotoa ushahidi unaoweza kumpa haki zake jitahidi tu basi tu

Ila polisi hawaaminiki na haswa kama hujiamini na sio mwongeaji mzuri ni shughuli
 
Mm juzi nimerudi kwetu hapo tanga niliko zaliwa nikamuulizia jamaa mmoja ivii anaitwa Asumani ni chiz kidogo namjuwa toka udogoni kwangu chaajabu yule tunaambiwa alitoweka siku nyingi ila sio yeye kuna Chekse pia huyu nae chenga kidogo nae pia alitoweka[emoji25][emoji25] nilimuuliza asumani kwakuwa nilikuwa namtania lila nikimuona yote kwa yote nawaombea huko waliko [emoji29][emoji29]
 
Hili kwakweli lipo aisee .
Hata mimi kuna tukio ilibidi tu nicheze part ya kumfikisha mtu kwenye sehemu salama na nikimbie nikabaki mtazamaji wa mbali tu aisee . Polisi siwaamini kabisa .
Muhimu kama unaweza kuokoa maisha jitahidi okoa maisha

Kama unaona kuna mtu anaenda kuonewa kwa wewe kutotoa ushahidi unaoweza kumpa haki zake jitahidi tu basi tu

Ila polisi hawaaminiki na haswa kama hujiamini na sio mwongeaji mzuri ni shughuli

Tatizo ni namna wanavyo kuchallenge na kukutisha unaweza ukijichanya ukakosea katika kuropoka basi watashikilia hiyo hiyo point na kukuhoji maswali kwa lengo la kukubananisha mwenyewe kwahiyo hapa tatizo sio kutokujiamini tatizo ni mindset za polisi shahidi anatakiwa aandaliwe mazingira mazuri ya kuelezea ushuhuda wake lkn wao wanatumia vitisho na maswali yasiyo jibika
 
Hii hali ni mbaya sana. Juzi uswahili kwetu huku tulisikia makelele ya watoto "Baba ana mchinja Mama" muda wa jioni tu kama saa kumi na moja kasoro.Watoto wamepiga kelele wee hadi wanaita majina ya jirani zao lakini waliotoka nje waliishia milangoni mwao tu hakuna aliyesoge

Mimi nikatoka nikasogea eneo ambalo kuna jamaa ni mafundi seremala. Nikiwaomba twende tukaamlie ugomvi watoto wamepiga kelele muda mrefu

Lengo langu na mimi ilikuwa kukwepa "kiherehere" kama mtoa mada alivyosema ili angalau tuwe wengi wengi

Ile kuingia ndani tukakuta "Hamadiii" mama wa watu yuko uchi kama alivyozaliwa kamakalia jamaa kifuani anaminya shingo jamaa katoa macho kuhema hawezi. Watoto wanalia "Baba anamchinja Mama" kumbe Mama ndo anamchinja Baba na kweli tusingeingia ndani muda ule huenda madhara makubwa yangetokea maana jamaa alikuwa kalewa hana uwezo wa kujitete na kisa cha ugomvi jamaa amerudi kalewa wakati familia kaiacha bila chakula ndani Mama hasira zikampanda akaona ampe adabu kidogo

Baada ya kuamlia ule ugomvi na kufikisha taarifa kwa mjumbe wa mtaa, jamaa alienda kuwashukuru wale fundi seremali kwa kuokoa uhai wake kwasababu ndio wanaofahamika zaidi pale kitaa. Wakamwambia wao waliogopa kuingilia ugomvi wasioujua wakasema mshukuru fulani aliyekuja kutushawishi (wakinitaja mimi) vinginevyo kwa hali tuliyoikuta ungekuwa historia sasa hivi

Ukiuliza kwanini watu hawakwenda kuamlia, ni kukwepa kutoa ushahidi tu hakuna kingine.

Kuna haja sana ya polisi na vyombo vya sheria kubadili mindset zao juu ya mashuhuda ili watu wasaidiane huku kitaa
Unaona WANAWAKE WALIVYO. Yaani hayo matoto yameshasetiwa kitambo kuwa mkiona ugomvi semeni baba anamuua mama.
Wanawake!!!! MUNGU ANAWAONA
 
Mambo mengi sana yako ovyo.Ile tume ya haki jinai ilitoa ripori nzuri sana ila kwa bongo jinsi ilivyo itatuchukua karne nyingi kuishi kulingana na ile ripori.Kwa ujumla jeshi la polisi na mahakama ni shida sana.Na hiyo inapelekea wananchi kuchoka na badae watakua wanajichukulia sheria mkononi.Tukifika uko hakuna hatakayekua salama.kwasasa wacha tu tusifiane bila mambo ya msingi muda utatoa majibu.
 
Ifike mahali jeshi la polisi na sheria pia ziangaliwe upya. Hivi inashindikana kabisa kutumia hekima?
Sheria zetu zinatutengeneza tuwe na roho mbaya.
 
Fanya ujinga Wote ktk Maisha yako, lakini sio kuwaeleza Polisi Taarifa ya Muarifu, Polisi WATANZANIA Ni Waajabu, Wakimpata mwalifu wanamwambia ukweli Wote kua we ndo umechomeshwa mpaka akamatwe.
Pia kutoa ushirikiano kwa Polisi Ni kujitafutia shida.

Ni hatari kwa afya 😂
 
Kuna kusumba kwa baadhi ya wazazi wanawaonya vikali sana watoto wao kuwa wasiwe na kiherehere kwenye matukio mabaya hatakama anafahamu A to Z utasikia mzazi anamwambia nyamaza kama hujaona chochote lakn nadhani kosa halipo kwao
 
Back
Top Bottom