Uchira 1
JF-Expert Member
- Oct 9, 2017
- 5,994
- 8,696
Awali ya yote nikupe pongezi mkuu.Hii hali ni mbaya sana. Juzi uswahili kwetu huku tulisikia makelele ya watoto "Baba ana mchinja Mama" muda wa jioni tu kama saa kumi na moja kasoro.Watoto wamepiga kelele wee hadi wanaita majina ya jirani zao lakini waliotoka nje waliishia milangoni mwao tu hakuna aliyesoge
Mimi nikatoka nikasogea eneo ambalo kuna jamaa ni mafundi seremala. Nikiwaomba twende tukaamlie ugomvi watoto wamepiga kelele muda mrefu
Lengo langu na mimi ilikuwa kukwepa "kiherehere" kama mtoa mada alivyosema ili angalau tuwe wengi wengi
Ile kuingia ndani tukakuta "Hamadiii" mama wa watu yuko uchi kama alivyozaliwa kamakalia jamaa kifuani anaminya shingo jamaa katoa macho kuhema hawezi. Watoto wanalia "Baba anamchinja Mama" kumbe Mama ndo anamchinja Baba na kweli tusingeingia ndani muda ule huenda madhara makubwa yangetokea maana jamaa alikuwa kalewa hana uwezo wa kujitete na kisa cha ugomvi jamaa amerudi kalewa wakati familia kaiacha bila chakula ndani Mama hasira zikampanda akaona ampe adabu kidogo
Baada ya kuamlia ule ugomvi na kufikisha taarifa kwa mjumbe wa mtaa, jamaa alienda kuwashukuru wale fundi seremali kwa kuokoa uhai wake kwasababu ndio wanaofahamika zaidi pale kitaa. Wakamwambia wao waliogopa kuingilia ugomvi wasioujua wakasema mshukuru fulani aliyekuja kutushawishi (wakinitaja mimi) vinginevyo kwa hali tuliyoikuta ungekuwa historia sasa hivi
Ukiuliza kwanini watu hawakwenda kuamlia, ni kukwepa kutoa ushahidi tu hakuna kingine.
Kuna haja sana ya polisi na vyombo vya sheria kubadili mindset zao juu ya mashuhuda ili watu wasaidiane huku kitaa
Mm hio naita utu na asilimia kubwa ya watu wa mijini hasa dar hawana tena utu ndo maana kelele za watoto zilikuwa nyingi ila kutokana na ubinafsi wao wakaona ni sawa tu wao kukaa ndani
Mkuu issue si ushahid kama mtoa mada alivyosema ila ni ubinafsi na kujiona smart na kutotaka kuingilia maisha ya watu
Ila hao hao ambao walisikia sauti kama kungekuwa na kifo wao ndo wakwanza kupiga story nying mtaan kama wale ambao eneo la tukio hukinbilia kupiga picha na simu pasipo kukumbilia kutoa msaada