Sababu ya watu kuogopa kutoa ushahidi kwenye baadhi ya matukio aliyo shuhudia live na wengine baadhi hukimbia kabisa

Mkuu ni kweli kabisa hii hali

Mi ilikua hivi
Mida ya usiku kama sa mbili kuna bodaboda alikua mbele yangu mi nna kibajaji sasa mbele kuna Lori lilikua bovu halina reflecta wala halijawasha taa sas yule boda hakuliona akaligonga kwa nyuma akaanguk hp hp na kupoteza faham watu walikuj wengi kushuhudia ila hawakutaka kumbeba bahT nzuri mm nikajitolea kumplek hospital ila baada ya jamaa kupandushwa kweny bajaj kila mtu akpita na njia zake hawatki ushahid bahat akatokea jamaa tu muokt kopo tukaend nae hospt na mgonjwa

Tumefk hospital wakagom kumtib had tuend polis kuchukua pf3. Tumefika polisi wanaanz kutuuliza jamaa anaitwa nani anakaa wap na maswali personal kibao na sis hatumjui ...tukajieleza tumerudi tena hospital nao wanatak hela za kufungua file na matibabu ..kiukwel polisi na mahospitali inabidi suala la ajali liangaliww uppya watu wanaacha kusaidia watu kwa kukwepa kubeba mizigo juu ya mizigo labda kama jamaa angekata moto naona kabisa mimi na muokta kopo tungewekwa ndani kwa ajili ya ushahidi

Tunaomba sheria au sera za majanga au ajali ziangaliwe upya ..pia ikiwezekqna pf3 ziwepo hospital na sio polisi

Asante
 
Inasikitisha sana,. Kuna jamaa yangu alienda kuripoti kituoni kuwa ameibiwa simu akaandikiwa RB kisha akaambiwa kesho urudi,. Kweli siku iliyofuata jamaa alienda tena kituoni cha ajabu akaishia kuulizwa " umefikia wapi kutafuta simu yako." yani kiufupi yeye ndo akageuka kuwa mpelelezi.
 

Sasa hapa ndio tunapata picha kamili jinsi haya matendo yanavo athiri jamii kwa ujumla
 
Bongo hamna mahakama mkuu, kama jaji anateuliwa na Raisi utegemee mhimili kuwa huru!
 
Hili kwakweli lipo aisee .
Hata mimi kuna tukio ilibidi tu nicheze part ya kumfikisha mtu kwenye sehemu salama na nikimbie nikabaki mtazamaji wa mbali tu aisee . Polisi siwaamini kabisa .
Muhimu kama unaweza kuokoa maisha jitahidi okoa maisha

Kama unaona kuna mtu anaenda kuonewa kwa wewe kutotoa ushahidi unaoweza kumpa haki zake jitahidi tu basi tu

Ila polisi hawaaminiki na haswa kama hujiamini na sio mwongeaji mzuri ni shughuli
 
Mm juzi nimerudi kwetu hapo tanga niliko zaliwa nikamuulizia jamaa mmoja ivii anaitwa Asumani ni chiz kidogo namjuwa toka udogoni kwangu chaajabu yule tunaambiwa alitoweka siku nyingi ila sio yeye kuna Chekse pia huyu nae chenga kidogo nae pia alitoweka[emoji25][emoji25] nilimuuliza asumani kwakuwa nilikuwa namtania lila nikimuona yote kwa yote nawaombea huko waliko [emoji29][emoji29]
 

Tatizo ni namna wanavyo kuchallenge na kukutisha unaweza ukijichanya ukakosea katika kuropoka basi watashikilia hiyo hiyo point na kukuhoji maswali kwa lengo la kukubananisha mwenyewe kwahiyo hapa tatizo sio kutokujiamini tatizo ni mindset za polisi shahidi anatakiwa aandaliwe mazingira mazuri ya kuelezea ushuhuda wake lkn wao wanatumia vitisho na maswali yasiyo jibika
 
Unaona WANAWAKE WALIVYO. Yaani hayo matoto yameshasetiwa kitambo kuwa mkiona ugomvi semeni baba anamuua mama.
Wanawake!!!! MUNGU ANAWAONA
 
Mambo mengi sana yako ovyo.Ile tume ya haki jinai ilitoa ripori nzuri sana ila kwa bongo jinsi ilivyo itatuchukua karne nyingi kuishi kulingana na ile ripori.Kwa ujumla jeshi la polisi na mahakama ni shida sana.Na hiyo inapelekea wananchi kuchoka na badae watakua wanajichukulia sheria mkononi.Tukifika uko hakuna hatakayekua salama.kwasasa wacha tu tusifiane bila mambo ya msingi muda utatoa majibu.
 
Ifike mahali jeshi la polisi na sheria pia ziangaliwe upya. Hivi inashindikana kabisa kutumia hekima?
Sheria zetu zinatutengeneza tuwe na roho mbaya.
 
Fanya ujinga Wote ktk Maisha yako, lakini sio kuwaeleza Polisi Taarifa ya Muarifu, Polisi WATANZANIA Ni Waajabu, Wakimpata mwalifu wanamwambia ukweli Wote kua we ndo umechomeshwa mpaka akamatwe.
Pia kutoa ushirikiano kwa Polisi Ni kujitafutia shida.

Ni hatari kwa afya 😂
 
Kuna kusumba kwa baadhi ya wazazi wanawaonya vikali sana watoto wao kuwa wasiwe na kiherehere kwenye matukio mabaya hatakama anafahamu A to Z utasikia mzazi anamwambia nyamaza kama hujaona chochote lakn nadhani kosa halipo kwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…