Sababu ya watu kuogopa kutoa ushahidi kwenye baadhi ya matukio aliyo shuhudia live na wengine baadhi hukimbia kabisa

Awali ya yote nikupe pongezi mkuu.
Mm hio naita utu na asilimia kubwa ya watu wa mijini hasa dar hawana tena utu ndo maana kelele za watoto zilikuwa nyingi ila kutokana na ubinafsi wao wakaona ni sawa tu wao kukaa ndani

Mkuu issue si ushahid kama mtoa mada alivyosema ila ni ubinafsi na kujiona smart na kutotaka kuingilia maisha ya watu

Ila hao hao ambao walisikia sauti kama kungekuwa na kifo wao ndo wakwanza kupiga story nying mtaan kama wale ambao eneo la tukio hukinbilia kupiga picha na simu pasipo kukumbilia kutoa msaada
 
UBINAFSI NA UMWINYI NDIO SABABU YA VIFO VYA WATU WENGI SEHEMU ZA AJALI
mfano kisa cha yule kijana aliyepata ajali hapo tegeta alikufa kizembe kutokana na ubinafsi na kukosa kwa utu kwa baadhi ya watu.

Laiti ndugu yake angekuwepo pale labda leo tungekuwa hatuna msiba maana naamin angemchukua na kumkimbiza hospitali ila wale wapiga picha na watu wa kutaka kuonekana walishuhudia wao walibaki kupga kelele tu.

Niliwahi ona kisa cha nyumba za wapangaji zaid ya 13 zikivunjwa na vibaka wasiofika kumi na wakiingia chumba kimoja kimoja hadi kumaliza vyumba vyote.
Wapangaji hawakuwa na lakufanya zaid ya kungo nao wafikiwe.

Kukosekana kwa upendo
Kukosekana kwa huruma
Ubinafsi
Ndio chanzo cha yote haya. Hivi ndugu yako akifanyiwa baya hutomsaidia kisa hizo sababu za polisi.
Tupendane
 
Mm nilipata ajali pia wasamalia wema walinisaidia nikafika hosptal mm sijali police walete huo ujinga wao ila km naweza msaidia binadam mwenzangu akihangaika kuutete uhai wake lazima nitamsaidia.
Mkuu hakuna kitu kinauma kama kuona mtu anakufa na uliweza toa msaada.
Mm nasaidia yoyote nikiona naweza toa msaada. Utu na uhai n zaid ya issue za polisi na mahakama
 
Jeshi lilioundwa ili kumtumikia mkoloni bado sera ni hizo hizo utegemee mabadiriko?? Si bora kidogo hata Kenya kwa sasa kuna unafuu!! Jeshi linaloamini vitisho zaidi
Polisi jau sana.... Nilitoaga msaada Kwa mdada nilimkuta njiani amepasuliwa kichwani yupo Kando ya barabara.... kufika polisi apate pf3 maana ni jirani tu na polisi na hospital ya Wilaya sio mbali ....nikawekwa Mimi ndani.... Sitosahau mabwege sana wale jamaaa...... Mpaka yule dada alipopata fahamu na kuchukuliwa maelezo nimeshakaa ndani usiku kucha ....
 
Mtu kugomea kutoa ushirikiano ni kumzulumu mtu hasa mhanga haki yake
 
Ili kipigo kimuingie vizuri...

Ila hao watoto wali fanya u-snitch sana kwa mzee wao. Yani mama anachinjwa kumbe ndio baba ananyongwaa..

Au watoto walikuwa wanapiga kelele kwa code..
Watoto ni smart, unaweza kuta walijua wakisema mama anampa kipondo baba labda watu wange puuzia au walikua wana maintain masculine status ya dingi yao.
 
Mambo mengine ni ujinga tu uliojilimbikiza kwa jamii,kama hili halihusiani kabisa na matatizo ya police.

Nikupe mazingira tofauti uone namna gani ujinga wa wa jamii nzima unavyosababisha wanashindwa kutatua kero zinazowahusu wenyewe??
Mtu anaweza akakwapuliwa simu aliyeibiwa na waliomkamata ni watu tofauti,waliomkamata wanakabidhi simu kwa mwenye nayo kisha wakiwa wanataka kuua kwa moto wanatokea polisi na kumchukua kibaka husika kumpeleka kituoni,hatatokea aliyeibiwa wala walioshuhudia tukio kuhakikisha jamaa anafungwa,mwisho kibaka anaachiwa kwa dhamana,zinaanza kelele kwamba polisi wamekula rushwa kibaka karudi mtaani.

Swala la shahidi kuhusishwa kwenye case sio rahisi kama kupakwa sukari ionekane uliramba,kuna mambo mengi ya kiupelelezi yanaangaliwa.
 
Pf3 ikitokea hospital haitakuwa PF3,labda itaitwa HF3,hii ni kama ila barua ya mwenyekiti wa serikaliya mtaa unapoishi kukutambua.
Inatokea polisi ili hospital kujiridhisha kwamba mhanga hahitajiki kujibu tuhuma zozote baada ya kupona,isijekuwa unatibu mtu kumbe kachoropoka ktk mikono ya wenye nchi baada ya kukutwa anabaka mtoto,hivyo anatakiwa atibiwe na pingu ktk kitanda.ndio sababu hata utokaji wake unaambatana na maswali mengi sana ambayo ni kero kwa msamalia aliyejitolea kama wewe.

Ni hakika mlolongo huo una changamoto kubwa lakini ulirenga jambo muhimu pia,labda tubadili mfumo iwe kila hospital kunakuwa na pingu kwa ajili ya wagonjwa wa dharula,ukija hujitambui unapigwa bangiri matibabu yanaendelea mpaka polisi waje kuhakiki huna shida ndipo uachiwe.
 
Mm nilipata ajali pia wasamalia wema walinisaidia nikafika hosptal mm sijali police walete huo ujinga wao ila km naweza msaidia binadam mwenzangu akihangaika kuutete uhai wake lazima nitamsaidia.

Safi sana mkuu ubarikiwe sana
 

Ngoj nikupe mfano unaolingana na huo uliotoa hapo,, kuna mama mmoja huku mtaani alikuwa ameibiwa mbuzi yule mwizi alikamatwa alipelekwa polisi lakini polisi walimtaka yule mbuzi kwa ajili ya upelelezi πŸ˜‚ hadi leo hii yule mama hajui mbuzi wake wamempeleka wapi πŸ˜‚πŸ˜‚ sasa unadhani huyo mama siku nyingine atakubali kupeleka kesi polisi?? Yani mwizi amekamatwa tyr na mbuzi lkn wanasema wanahitaji mbuzi wafanye upelelezi

Je kwa hali hii wanasaidia watu? Hata hiyo simu lazima wangechukua tu kwa ajiri ya upelelezi sasa havirudi?? Polisi wanakuwa kama vile wanachoshwa na watu wakati huo ni wajibu wao
 
Geshi la Polisi ni big Problemas wakuu,
Yaani hayo majamaa ni majambazi yaliyopewa sale na silaha kutekeleza kazi maalumu yaani hilo jeshi msaada ni 2% zilizobaki zote ni balaa tupu,
Linahitaji kufumuliwa na kuundwa police service na Sio force!
 
Reactions: K11
Kuna kitu kinaitwa mind your own business ushahidi sio mzuri unapotezwa chap hasa ktk vitu senstive
 
Kesi=wizi wa mbuzi.
Mlalamikaji=mama mmoja.
Mtuhumiwa=amepatikana.
Wakamataji=police wa kituo fulani.

Hii case mazingira yake ni kama lalamiko la msingi la mleta mada,mtu unapata tatizo la kijinai labda kwa sababu mbali mbali unaamua kuliachia GESHI LA POLISI,ukiamini unatakiwa kusubiria haki yako,pasi na kusindikiza kujua mwenendo wa kesi.kesi yenge hints zile pale juu,ni ngumu sana kuzitemper,hata police wanajua,ila kikikosekana kimoja tu hapo,zinaanza sarakasi.

Ukute mama kwa uzito wa kujua sheria alikuwa msubirifu tu,akiwa na uhakika mbuzi na mtuhumiwa walipanda gari la police,kumbe anatakiwa police na pia mahakamani labda kila baada ya siku 5 mwezi mzima,ikaonekana mlalamikaji haonekani.
 

Kama umewahi kufatili kesi yoyote polisi au umewahi kuona mtu akifatilia kesi nafhani utakuwa unafahamu changamoto zake,, ni sawa nakupoteza time na gharama for nothing yaan utaenda then utaambiwa maneno fulani kuwa polisi wapo wanashughulikia utulie tuli
 
Reactions: K11
Yaani Polisi Tanzania HOVYO sana, ilikuwa Tarehe 9/11/2022 usiku majambazi wakabomoa kwangu wakaiba vitu vya kutosha, asubuhi nikatoa taarifa kituo cha polisi, nikaorodhesha kila kitu, la kushangaza nikawa nadaiwa pesa ya kununua karatasi, nikasema poa nikawapa... Nikamaliza kila kitu wakaniambia wanakuja eneo la tukio.... Kwa kweli sikuwaona wakija, sehemu iliyobomolewa ilibidi nirekebishe na maisha yaendelee.... Ikiwa ni tarehe 24/12/2022 majira ya Asubuh, nilisha sahau maumivu ya kuibiwa yalisha pona, simu mpya inaingia na jamaa anajitambulisha kuwa ni polisi yeye ndiye kapewa faili langu ili aje kwenye eneo la tukio aweze kufanya uchunguzi..... Zaidi akaomba nintumie pesa ya mafuta ili aweze kufika eneo la tukio..... Nilicho shangaa.... 1 yaani mwezi mmoja na umepita alafu askari anataka aje kufanya uchunguzi
2. Ina maana eneo lililo bomolewa ilipaswa nisifanye marekebisho hadi polisi wafike zaidi ya mwezi na zaidi... 3
Polisi alitaka nimpe ela ya mafuta au nauli ndipo aje kwenye eneo la tukio
4. Kituo hakina pesa ya kununua Carbonpaper na karatasi?
Mheshimiwa Rais Samia hiyo ndiyo hali halisi ya Utendaji kazi wa JESHI LA POLISI TANZANIA.
 

Now we focus on UNITED STATES OF AFRICA 🌝 huenda kutakuwa na system mpya hawa viongozi wetu haya yote wanayafahamu sababu asilimia kubwa viongozi wengi wametokea kwenye hali duni za maisha ila wanajisahaulisha kuwa kuna hizi kero huku chini ila kwasababu wao wapo kwenye good condition basi sisi wenye critical condition tupambane na hali zetu ni kawaida ya binadamu akitoka hatua moja kwenda nyingine kama aliipitia hiyo hatua kwa ugumu basi wanataka wote wapite kwa ugumu hivo hivo, wachache sana wanao kumbuka wengine like Magufuri
 
Yani nikikumbuka hawa washenzi walichonifanyia..[emoji28] yasikie tu kwa watu
 

Ni wachache sana wanao kumbuka magumu walio kumbana nayo nakutaka wengine wasikumbane nayo ni wachache sana
tulikuwa na 1. kwame Nkurumah 2. Nyerere 3. Patrice Lumumba 4.Magufuri 5. Thomas Sankara n.k
 
Polisi wabongo mtoa taarifa ndiye huwa wa kwanza kuwekwa ndani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…