Sababu za kiroho kwanini lazima ufunge Ramadhani hata kama sio muislamu

Lengo maalumu. Ili kutukumbusha turudi kwake na kuadhibu.

Ili atutahini,aone kina nani watashukuru na kina nani watakufuru.
kwa hiyo suala la binadamu kiumbe dhaifu asiyekamilika, kwake halipo kabisa!?? Atulete yeye mwenyewe, atupe mitihani yeye, na bado atuadhibu yeye kwa hiyo mitihani yake[emoji848]
Alikuwa na uwezo wa kufanya yote hayo yasiwepo kabisa na dunia ikawa sehem salama sana Kama anavyosema Kiranga

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
kwa hiyo suala la binadamu kiumbe dhaifu asiyekamilika, kwake halipo kabisa!?? Atulete yeye mwenyewe, atupe mitihani yeye, na bado atuadhibu yeye kwa hiyo mitihani yake
Huo ndiyo udhaifu wa mwanadamu,sababu Mola alipotuumba hakutuacha hivi hivi,akatupa akili,akaleta mitume wa kutupa muongozo wa Mola na akatupa uhuru,yaani ukiona unafanya kosa ujue uliweza kuliepuka.

Mitihani aliyotupa ina majibu kabisa ndiyo maana ana tadhibu kwa kuzembea.
Alikuwa na uwezo wa kufanya yote hayo yasiwepo kabisa na dunia ikawa sehem salama sana Kama anavyosema @Kiranga
Hili kwake rahisi sana,ila anafanya lililo bora zaidi na kwa malengo.
 
Malengo yapi?

Mpaka sasa.

1. Hujathibitisha Mungu yupo.

2. Hujaeleza kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea.

3. Hujatatua contradictions zilizopo kwenye vitabu vinavyoelezea uwepo wa huyo Mungu. Nimeweka contradictions kemkem zilizopo katika Quran na Biblia.

Hujatatua hata moja.
 
Safi kabisa,hali hivyo jibu maswali niliyo kuuliza.

Nimeanza na moja hiyo ya nani Muislamu wa kwanza. Ile nimeimaliza nataka niingine nyingine,ila mpaka ukiri au ukosoe jibu langu nililo toa,najua hili huwezi kufanya mpaka unakufa sababu huijui Qur'aan na kule umecopy na ku paste. Sasa unasikitisha sana,inakuwaje ukashindwa kufanya utafiti kijana ?
 
Usinieleze kuhusu Biblia mimi niulize kuhusu Qur'aan,ambacho hiki ndiyo kitabu changu cha muongozo.

Nukta ya kwanza kuhusu nani muislamu wa kwanza nimeimaliza. Nataka niingie nukta ya pili,ila ujibu maswali niliyo kuuliza kutokana na nukta hiyo. Hapa nakuonyesha ni kwa namna gani ulivyo mtupu na una copy mambo kichwa mchunga bila kufanya utafiti wa kina. Huu ni ujinga wa hali ya juu.

Hakuna nukta katika hizo tatu ambayo sijaijibu kama unao uwezo onyesha wapi sijajibu katika hizo nukta tatu,ukiweza naacha kujadili huu mjadala.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Labda nikusaidie kidogo, kwa hapa ni dhahiri unafata upepo kaka, hujasoma quraan wala kuhangaika kusoma hizo unazoita ww ni contradictions, kwa vike ww ni atheist basi kila unachokiokota ni unaamini 100%...
Tuanze na hizo contradictions chache..

Tuchukulie mfano wa ukuaji wa kipepeo..
Anaanza yai kwenye gamba chorion, kisha kiwavi, kisha pupa halafu ndio kipepeo kamili kama sijakosea,
Je mungu akisema amemuumba kipepeo kutoka kuwa chorion, yai ama buu atakuwa kakosea, hizo ni stages ambazo kipepeo anabadilikia..

Sasa mungu anaposema katuumba kwa udongo, hiyo ndio uhalisia, tumeumbwa kwa udongo, ikisha akajaalia sisi kutokana na manii, kuwa pande la damu, kisha, kijusi na kadhalika, ametaja hatua zoote hizo ni elimu kwetu tujue tulianzia wapi, na hatua zoote zimetajwa katika quraan.
Na anaposema hatukuwa chochote, kwa lugha ya tafsiri unapata tafsir mbili..
Moja, tafsiri ya cheo ama hadhi, mfano mtu anapomsaidia mtu baadae aseme nilimuokota hakuwa na chochote je hakuwa hata na nguo? Hivyo anaposema hatukua chochote kwa bimaana udongo ni dhalili mnoo kulinganisha na matokeo ya kuumbwa kwetu, anatukumbusha sisi tusijione wajanja ni dhalili mnoo na kuna aya ndani ya kuraan kazungumzia hili

Pili, ndio kabla ya kuumbwa hatukuwa chochote, simu kabla ya kutengenezwa ilikiwa ni nini? Cobalt? Lithium? Copper? Gold ama silver, au tulikuwa silicon au lead? La hasha, haikuwa kitu

Umekopi baadhi ya aya hapo juu..
Hizi aya zoote ni kutuonesha hatua zetu za ukuaji, kuwa tulikuwa udongo, tulikuwa manii, kisha pande la damu, baadae kutiwa mifupa nakadhalika

96:2
2. Amemuumba binaadamu kwa tone la damu,

15:26
26. Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope meusi yaliyovunda.

3:59
59. Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa.

19:67
67. Je! Hakumbuki mwanaadamu ya kwamba tulimuumba kabla(hali yake hii), na hali hakuwa chochote?

52:35
67. Je! Hakumbuki mwanaadamu ya kwamba tulimuumba kabla, na hali hakuwa chochote?

16:4
4. Amemuumba mtu kwa tone la manii. Naye mara amekuwa mshindani dhaahiri.

Quraan 23 suratul muuminun inakujibu kama nilivyojaribu kukuelezea.. Aya ya 12 mpaka ya 14
12.Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo.
13. Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika makao yaliyohifadhika(madhubuti)
bila shaka ndio huko tumboni kwenye Uterus
14. Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji

Nyongeza ukisoma inaweza kukusaidia chief
Suratud dahr 1-3
1. Hakika kilimpitia binaadamu kipindi kirefu katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinacho tajwa.(binadamu ndio kiumbe wa mwisho kuletwa duniani) hatukuwa chochote

2. Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika(ya mwanaume na ya mwanamke) tumfanyie mtihani(kwa amri zetu na makatazo yetu) Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia na mwenye kuona.

•: hapa mungu anatuongezea kuwa sisi tulipitia katika steji ya kuchanganyika mbegu ya baba na mama

3. Hakika Sisi tumembainishia Njia(mbili, kheri na shari, Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru.

Hapo ni juu yetu kushukuru ama kufaulu juu ya akili(utambuzi) aliotupa allah

Ama katika sura al qiyama ukianzia aya ya 36-39

36. Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure?

(Yaank tusipewe makatazo, tusipewe maamrisho, kwa jinsi tulivyoumbwa ama kuwa kabla)

37. Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?(lililotonwa)

Hapa mungu anaongelea kuwa sisi tulikuwa ni bao, hatua ya kutolewa shahawa ama kukojowa vijana wanasema[emoji13]

38. Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.(mwanadamu kamili)

39. Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.

Quraan 53:45-46
45. Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike
46. Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa

Ahsante sana chief.
 
Nitaacha shughuli zangu kujibu tu maswali uliyokopi sehemu kaka, mambo ni taratibu nitakuwa nakujibu kadri nioatavyo nafasi, umekusanya vitu tofauti kwa wakati mmoja, sijui nijibu kipi niache lipii

Haya bismillah, naanza na hizi contradictions zako juu ya uumbwaji wetu..

Mungu mmoja kwa nini anasema "tulimuumba"?

"Tulimuumba" kwani Mungu alikuwa na mshirika katika uumbaji?

Unaelewa kwamba mpaka sasa hujathibitisha Mungu yupo, unahubiri tu?

Unaelewa jwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote angekuwepo, tusingehitaji kitabu kumjua?

Unaelewa kwamba Mungu huyo angekuwepo, kusingekuwa na mtu yeyote mwenye shaka wala swali kwamba yupo?
 
Himena himenes.. Upo ndugu yangu?
Umeuliza swali ambalo linafanana na alilouliza Kibukuasili ,hivyo nimekopi jibu nililomjibu yeye

Waislam Tunafunga sababu ya kiimani, lakini ndani yake kuna faida kedekede(somo oana kidogo), kwakuwa mola aliyetuumba ndio katuamrisha hivyo tunafunga kwa sababu yake yeye(kasema)tuwe wenye kufaulu kupata yale aliyotuahidi, lakini mtume anasema fungeni mtapata afya, kumbe ndani ya kufunga kuna faida moja wapo ya kupata afya, hivyo kwa asiekuwa muislam akifunga hatapata malipo kutoka kwa mola, ila anaweza pata faida za kiimani(mfano anapokaa na njaa hali anauwezo(ana mchele ndani na kila kitu/pesa ya kununulia msosi wa nguvu) wa kununua chakula lakin hanunui sababu kafunga basi anaweza kupata imani(kuwaonea huruma) wale ambao huwa hawali sio sababu wamefunga la hasha ni kwa sababu hawana chochote cha kukila, anapokamatwa na kiu na hanywi maji sio kwamba hana buku jero ya kununua Kilimanjaro la hasha ni sababu kafunga, anaweza kupata imani kuwaonea huruma wale ambao huwa wanashindwa kunywa maji sio hawana kiu ni vile hawawezi kuyapata maji(hivi ndivyo dini inataka, tuhurumiane, ndio msingi wa dini)

Na mwishoni ni huko kupata afya ya kimwili, ukifunga mchana kutwa kisha jioni, ufuturu glas ya maji, ule hata vijiko kadhaa vya tende ama chakula chochote.. Kisha aidha baadae ule daku/ama usile kisha kesho uendelee na swaumu kuna faida ya kiafya.. Hi ni kwa muislam na ambae si muislamu.

Kuna sunnah ya kupiga mswaki, kuna faida ya kiimani na ya kiafya, ukiacha utapata madhara ya kiafya na unakosa vitu fulani kiimani.. Ukipiga afya unaoata na kiimani kuna mambo yanaenda sawa sawia..

Nadhani nimejitahidi kukujibu ndugu yangu.
 
Hiyo nukta ya kwanza umeimaliza wapi?
 
Hawa jamaa Mungu wao watoto wa mjini wanasema "anajitekenya mwenyewe, halafu anacheka mwenyewe".

Anatengeneza tatizo mwenyewe, halafu analitatua mwenyewe, halafu anataka sifa eti!

Huyu Mungu yupo kweli? Au fiksi za watu tu?
 
Yani Mungu wako kashusha kitabu kigumu kueleweka kwa watu aliowaumba yeye mwenyewe na kuwapa akili mwenyewe.

Kwa akili zao, walizopewa na huyo Mungu, wengine hawawezi kukielewa hiki kitabu.

Sasa hapo wakishindwa kukielewa kitabu hiki, kwa sababu Mungu hajawapa akili za kukielea, kosa ni lao au la huyo Mungu?

Mungu anaweza kumnyima mtu akili ya kuielewa Quran, halafu akamhukumu kwa haki mtu huyo huyo kwa kukosa kuielewa Quran?

Huyu Mungu mbona anaji contradict hivyo?

Yupo kweli huyu Mungu?

Au mnatupiga fiksi tu?

Ukishaona kitabu cha Mungu kina uwezekano wa kutoeleweka hapo hapo ujue hizo habari kwamba hiki ni kitabu cha Mungu ni fiksi tu.

Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote asingeshusha kitabu ambacho kina uwezekano wa kutoeleweka kwa waja wake.

Zaidi, Mungu huyo asingeshusha kitabu kabisa.

Kwa sababu kuna watu wamezaliwa misitu ya Amazon mpaka leo hawajapata nafasi ya kuona kitabu, wanazaliwa mpaka wanakufa hawajaona kitabu.

Sasa hawa Mungu kawasahau au vipi? Mbona kawapunja kupata kujua habari zake kwenye kitabu?

Kwa nini Mungu hakuweka habari zake zote za kwenye kitabu kwenye DNA, kila mtoto anayezaliwa ajue yote kuhusu Mungu bila kuhitaji kitabu?

Huoni kwamba hizi habari za maneno ya Mungu kuwa kwenye kitabu ni utapeli wa watu tu na Mungu huyo ni biashara ya kanyaboya?
 
Naona umeanza kuelewa sasa.

Sasa jibu maswali yangu katika hito post,usipoteze muda.

Kitabu si kigumu kukielewa endapo ukisoma na ukafundishwa,sasa wewe hujasoma wala hujafundishwa,ndiyo maana tunawaambia msome. Sasa hili liko dhidi yako kijana.

Hii si hoja sababu huwezi jua jambo mpaka ujifunze au ufunzwe. Ambao hawawezi kukielewa ujue hawaja fanya juhudi ya kutaka kujua jambo husika. Mathalani wewe umecopy jambo kisa umeona Title inakuvutia pasi na kusoma,sasa hapa kosa liko wapi ? Jibu bila shaka kosa ni lako.
 
Kwa nini Mungu kashusha kitabu na hajaweka habari zake kwenye DNA watu wote wamjue tangu wanazaliwa hata wale wa misiti ya Amazon ambao kwao hakuna kitabu?

Hujajibu swlai hili.
 
Kwa nini Mungu kashusha kitabu na hajaweka habari zake kwenye DNA watu wote wamjue tangu wanazaliwa hata wale wa misiti ya Amazon ambao kwao hakuna kitabu?

Hujajibu swlai hili.
Jibu maswali niliyo kuuliza.

Hivi unajisikiaje kutokujibu maswali unayo ulizwa ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…