Uchaguzi 2020 Sababu zinazofanya Magufuli apendwe na Watanzania wengi

Naomba nichukue fursa hii kujibu maswali yako kama ifuatavyo,

2. Hata marais wa miaka ya nyuma wanajua na wanamwamini Magufuli kwamba ni mchapakazi na hana mchezo katika kazi. Hivyo hiyo sababu inajibu swali lako unaloniuliza....
10: acha uwongo ninasomesha mdogo wangu juzi nimetoka kulipia ela ya ada na usajili wa mitihani kidato cha sita usionge usiyoyajua.
 
Hapo kwenye namba 10 napinga kabisa hakuna elimu ya bure, hivi mtoa post unajua maana ya neno bure basi waulize majiran zako watakumbia maana yake.
Kwani wewe unaelewaje hiyo point chief. Chief nadhani unakumbuka zamani akati tunasoma shule tulikuwa tunalipa ada na pesa ya tahadhari. Kwa shule za kataa tulikuwa tunalipa ada elfu 20 na tahadhari ilikuwa kama elfu 15 hivi.

Saivi hiyo michango haipo tena. Kwa shule za bweni tulikuwa tunalipia elfu 70 ada jumlisha na tahadhari ni kama 85 elfu hivi. Lakini saivi hiyo michango ilishaondolewa. Walimu wakuu wanaingiziwa pesa za kuendeshea shule kila mwezi
 
Hii sio hoja
Alitakiwa awalipe mafao yao wale wote aliowatumbua kwa vyeti feki ndiyo ingekuwa ubinadamu.
 
Wananchi ndio tumeamua tunamhitaji Magufuli. Tunahitaji Rais atakaye tuletea tren za umeme, ndege, atujengee miundombinu imara, na umeme wa uhakika,
Tena waambie huku jf hamuwezi kuchagua Rais, atachaguliwa na wananchi walio wengi hasa wa vijijini. Ila huku jf TL amekuwa Rais, hongereni tukutane 28 October.
 

Hizo ndege za ATCL zinapiga route ya wapi ,, hadi zinataftiwa route sijui kubeba samaki hasara tupu
 
Magufuli hategemei kura bali anategemea madaraka yake kutangazwa mshindi. Mtu anayeamini kupata kura hana jazba, na wala hawezi kutishia wapiga kura ili wampigie yeye.
unapoteza muda kumjibu hiyo hajielewi
 
Njaa itatawala pale ambapo mtashindwa kuwalipa wakulima wa korosho pesa zao,kuwalipa wakulima wa pamba pesa zao,mtashindwa kuongeza watumishi mishahara, mtashindwa kuweka mazingira mazuri ya ukuzaji wa sekta binafsi.
Endelea kusubiri, asipopita huyo unaetegemea akuboreshee maisha yako,kwenye uchaguzi huu. Endelea kulalamika humu kwenye majukwaa ya Jf, ukisubiria Miaka mitano mingine, ili Kama atapita akusaidie.
 
Hizo ndege za ATCL zinapiga route ya wapi ,, hadi zinataftiwa route sijui kubeba samaki hasara tupu
Sasa ndege zimeshanunuliwa, usipopanda wewe, tamutapanda hata sisi watu ambao uchumi wetu unaruhusu.
 
Hizo ndege za ATCL zinapiga route ya wapi ,, hadi zinataftiwa route sijui kubeba samaki hasara tupu
Kwanza ikumbukwe kwamba hizo ndege ndio zilikwenda kuchukua ndugu zetu na watanzania wenzetu waliokuwa wamekwama China na India katika kipindi cha Corona
 
Magufuli hategemei kura bali anategemea madaraka yake kutangazwa mshindi. Mtu anayeamini kupata kura hana jazba, na wala hawezi kutishia wapiga kura ili wampigie yeye.
Na wala hawezi kugawa na kuahidi vyeo wakati wa kampeni
 

Kakojoe ulale.
 
Ni kazi ngumu sana kuwaamuru watu wampende mtu asiye na upepo wa kupendwa...

Wana CCM wenyewe wanavumilia maana hawana pa kusemea!!
Sitaki kumwona wala kumsikia wala kumnusa nitatapika hadi nyongo. He is very repulsive ni wa kukwepwa kama mwenye ukoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…