Sabaya na wenzake washinda Rufaa dhidi ya Serikali kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Safi sana mahakama kwa kutenda haki, maana kuna baadhi ya wapuuzi wanataka kilichomo akilini mwao ndio kitendeke

Hivi tukiwa na sheria ya namna hiyo tutafika kweli????

Basi na kila ambae hataridhika na hii akakate rufaa ila sio kusema haki haijatendeka ilhali ushahidi upo wazi
 
Mm siyo mfuasi wa sabaya wala litakataka linaloitwa ccm, ila kwa mazingira ya kesi na jinsi mashaidi walivojichanganya sabaya hakustahili kufungwa, nilishangaa sana ile hukumu ya arusha, na kuna watu niliwaambia sabaya atashinda rufaa hata kama kesi itafika COT.
 
FB_IMG_1700279763852.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijn anaoshwa , na kjn wa mwenzake anaimuita kuja kulamba asali
 
Kuna kitu alikiongea Rostam Aziz kuna kikundi cha watu wakamkalia kooni akanushe na aombe radhi, ila ule ndio ulikua ukweli. Siku Sabaya akilamba uteuzi ndio maneno ya Rostam yatatimia.
 
Moja ya kazi ambazo niliomba maishani nisisomee ni Upolisi na uana sheria.
Ukitaka kuingia peponi kuwa daktari,mwalimu,mwanajeshi wa mabaka
Kuna usemi unasema ni aheri ukutane na jambazi mwenye silaha kuliko mwanasheria akiwa ameshika kalamu yake.
 
Kama Mahakama hazitoi HAKI tena basi msiwalaumu Watanzania watakapojichukulia Sheria mikononi.
Braza naomba nije pm kuna ishu unishauri uliwahi kunisaidia ishu fulani kitambo
 
Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imetupilia mbali Rufaa iliyokatwa na Upande wa Jamhuri, ikipinga uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha, kumuachilia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wamehukumiwa Kifungo cha miaka 30 jela.

Hukumu hiyo iliyosomwa na Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Abesiza Kalegeya, leo Ijumaa Novemba 17, 2023, imesema hakukuwepo na tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha, badala yake Mjibu rufani wa kwanza Lengai Ole Sabaya, alikuwa katika majukumu yake halali ya kufuatilia Makosa ya uhujumu uchumi kama ilivyoelezwa na Mashahidi wenyewe wa upande wa mashtaka.

Mahakama hiyo ya rufaa iliyokaa chini ya Mwenyekiti wake Jaji Jacob Mwambegele imeeleza zaidi kwamba, Mahakama ya Hakimu Mkazi iliyomtia hatiani Sabaya na wenzake, ilikosea kutochambua ushahidi unaoonyesha wazi kwamba, haiijawahi kutokea Jambazi akamate Mtuhumiwa, amnunulie Ndizi na baadae kumpeleka Polisi kama Mashahidi wenyewe walivyoelezwa kutendewa na Sabaya.

Majaji wameeleza hiyo ni aina ya kwanza ya unyang’anganyi wa Majambazi kuepeleka waliowaibia Mahakamani, na kuhitimisha kwamba Wajibu rufaa waliachiwa kihalali na Mahakama Kuu.

Mkurugenzi wa Mashtaka alikata Rufaa kupinga uamuzi wa Jaji E. Kisanya, kuwaachilia huru Lengai Ole Sabaya, Sylivester Nyegu na Daniel Mbura, waliokuwa wamehukumiwa Kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha.

Sinema zetu.
 
Ukiona wanaopandishwa kuwa Justices of Appeal unaona kabisa kuwa kuna shida sana huko CoA! Ni hao judges kutoka High court ambako ni "mavi" maupu, "mavi" hayo yanapanda kwenda kwenye apex court! Soma hata kiingereza chao, shida tupu! Linganisha hukumu za bold judges kama Mwalusanya na za hawa UPE, utaona clear intellect difference, a very big one
Hapo kwa Judge Mwalusanya ongezea na Judge Lugakingira.
 
DC anafuatilia kukamata wahujumu uchumi katika wilaya tofauti na yake!
 
Hapo kwa Judge Mwalusanya ongezea na Judge Lugakingira.
bold spirits judges: The BOLD SPIRITS within the judiciary beyond compare of this time. Their immense and exemplary contribution in protection, promotion and defence of human rights during their service is written on hard rock. They demonstrated an impressive and firm stand by judiciary in its role of dispensing justice without fear or intimidation. c&p
 
Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imetupilia mbali Rufaa iliyokatwa na Upande wa Jamhuri, ikipinga uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha, kumuachilia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wamehukumiwa Kifungo cha miaka 30 jela.

Hukumu hiyo iliyosomwa na Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Abesiza Kalegeya, leo Ijumaa Novemba 17, 2023, imesema hakukuwepo na tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha, badala yake Mjibu rufani wa kwanza Lengai Ole Sabaya, alikuwa katika majukumu yake halali ya kufuatilia Makosa ya uhujumu uchumi kama ilivyoelezwa na Mashahidi wenyewe wa upande wa mashtaka.

Mahakama hiyo ya rufaa iliyokaa chini ya Mwenyekiti wake Jaji Jacob Mwambegele imeeleza zaidi kwamba, Mahakama ya Hakimu Mkazi iliyomtia hatiani Sabaya na wenzake, ilikosea kutochambua ushahidi unaoonyesha wazi kwamba, haiijawahi kutokea Jambazi akamate Mtuhumiwa, amnunulie Ndizi na baadae kumpeleka Polisi kama Mashahidi wenyewe walivyoelezwa kutendewa na Sabaya.

Majaji wameeleza hiyo ni aina ya kwanza ya unyang’anganyi wa Majambazi kuepeleka waliowaibia Mahakamani, na kuhitimisha kwamba Wajibu rufaa waliachiwa kihalali na Mahakama Kuu.

Mkurugenzi wa Mashtaka alikata Rufaa kupinga uamuzi wa Jaji E. Kisanya, kuwaachilia huru Lengai Ole Sabaya, Sylivester Nyegu na Daniel Mbura, waliokuwa wamehukumiwa Kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha.
Ilikua suala la muda tu. Aliyofanya yote alitumwa na haohao. Cheo kinamfuata soon.
 
Jamhuri ndiyo imeshindwa rufaa

The expected! Mahakama za kishenzi. Kama walitoa hukumu kuwa Wakurugenzi kusimamia kura haina shida kwa vile wameapa kutenda haki, basi ujue hakuna mahakama ni takataka tu mbona wanajeshi wanapindua serikali ingawa wamaapa? chini ya viapo vyao?
Mkuu unazionea mahakama bure, Kwa sababu mshatakiwa alikuwa ni mtumishi wa serikali, waandaa mashaka ni watumishi wa serikali, askari waliomkamata ni watumishi wa serikali na muda fulani walikuwa chini ya mshatakiwa wa serikali huyo, wapelelezi ambao ni askari ni watumishi wa serikali na mawakili wa serikali ni watumishi wa serikali!

unaona huo mnyororo???

Mkuu unlitegemea nini tofauti ukiutazama mnyororo huo???

Je, kama hao watumishi wa serikali walipeleka ushahidi hafifu kumuokoa mtumishi mwenzao wa serikali??

Mkuu Mahakama haina kosa kwa sababu huamua kutokana na ushahidi ulioletwa mbele yake.

Mkuu kunahitajika overhaul nzima na kuseparate mfumo wa mashataka, ukamataji na upelelezi. Ziwe independent entities.
 
Mahakama ya Rufaa ya Tanzania imetupilia mbali Rufaa iliyokatwa na Upande wa Jamhuri, ikipinga uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha, kumuachilia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili waliokuwa wamehukumiwa Kifungo cha miaka 30 jela.

Hukumu hiyo iliyosomwa na Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Abesiza Kalegeya, leo Ijumaa Novemba 17, 2023, imesema hakukuwepo na tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha, badala yake Mjibu rufani wa kwanza Lengai Ole Sabaya, alikuwa katika majukumu yake halali ya kufuatilia Makosa ya uhujumu uchumi kama ilivyoelezwa na Mashahidi wenyewe wa upande wa mashtaka.

Mahakama hiyo ya rufaa iliyokaa chini ya Mwenyekiti wake Jaji Jacob Mwambegele imeeleza zaidi kwamba, Mahakama ya Hakimu Mkazi iliyomtia hatiani Sabaya na wenzake, ilikosea kutochambua ushahidi unaoonyesha wazi kwamba, haiijawahi kutokea Jambazi akamate Mtuhumiwa, amnunulie Ndizi na baadae kumpeleka Polisi kama Mashahidi wenyewe walivyoelezwa kutendewa na Sabaya.

Majaji wameeleza hiyo ni aina ya kwanza ya unyang’anganyi wa Majambazi kuepeleka waliowaibia Mahakamani, na kuhitimisha kwamba Wajibu rufaa waliachiwa kihalali na Mahakama Kuu.

Mkurugenzi wa Mashtaka alikata Rufaa kupinga uamuzi wa Jaji E. Kisanya, kuwaachilia huru Lengai Ole Sabaya, Sylivester Nyegu na Daniel Mbura, waliokuwa wamehukumiwa Kifungo cha miaka 30 jela na Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha.
Ninachojua kabisa ni hiki,
Ikiwa Mungu anataka kujitukuza juu ya mtawala mwovu humfanya awe na moyo mgumu wa kufa ganzi dhidi ya haki ili ampe uwanja mzuri wa maangamizo kama ilivyokuwa kwa Farao.
Itunzeni clip hii!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya yote ni Maigizo ya ccm, kuanzia kukamatwa kwake hadi kuachiwa, ndio maana sikuwahi post chochote kuhusu Sabaya hadi Leo hii ndo nafanya hivyo, hizo zilikuwa ngonjera kuwa furahisha wapinzani waaingie Maridhiano fake , hali ya hewa ikitulia tuna mwachia Kada wetu, mwacheni Kijana aendelee na maisha yake, tatizo sio yeye ni CCM ya jenga nchi.
 
Back
Top Bottom