SACP Wambura: Jeshi la Polisi Dar lakamata Majambazi, Wauaji, Wezi wa Magari na Pikipiki, na Uvunjaji

SACP Wambura: Jeshi la Polisi Dar lakamata Majambazi, Wauaji, Wezi wa Magari na Pikipiki, na Uvunjaji

Wangewafanyia ile kitu ya "walipigwa risasi walivojaribu kutoroka wakati wanaenda kuonesha maaskari walipoficha silaha"
Naunga mkono hoja.
Hii tabia ya kutumia demokrasia kupambana na watu wanao tumia silaha za moto haitofanikiwa kamwe kamwe ni lazima tuwe wawazi hawa watu wanapaswa kuchapwa risasi tuu kama ilivyokuwa kipindi cha Magu..

Hawa wapumbavu kuwakamata kama vile ni wezi wa vijiko ni ujinga na tunao teseka ni wakazi wa dares-salaam yani watu wanavamia hadi suma jk halafu unawakamata kidemokrasi hivi halafu useme uhalifu utakwisha kweli?

Lazima tuseme ukweli dawa ya moto ni moto sasa hivi dar kuna hofu kubwa ya ujambazi na njia ya kuumaliza ni kuwapa taarifa wenzao wameuwawa wakiwa wanapambana na jeshi la polisi.
Hawa wanapaswa kutwanga risasi tuu sio kuleta story za kuwakamata
 
Natamani kusikia huyo mkurya (wambura) anavyoongea 😂😂

Wanapendaga dana kutumia R badala ya L, rara chini, utanenda kujiereza kituoni, ntarara nikira..😂😂

Ila hawa jamaa kwenye ishu za usalama nawaaminia,

Naona hata simon Sirro ni wa kule kule Mara, Mura eeeh 😂😂
 
Ila Tanzania bana. Yan mpaka leo suala la CCTV cameras linaonekana halina msingi. badala ya polisi na mamlaka kusisitiza kila ofisi, eneo la biashara nk lazima liwe na hizi camera wao wanachukulia simpo tu. kazi kufanya jambo (uchunguzi kizamani sana).

Kuna matukio watuhumiwa wanadakwa n kujulishwa umma dk 0 tu. Kutaja majina Omar said sijui mkazi wa kimara hiyo ni kizamani. Mtu kaiba, kavunja kaonekana ktk camera mwekeni hewani kila.mmoja amuone na.amjue ni mwizi, mvunjaji PERIOD

Sent from my PBAT00 using JamiiForums mobile app
 
Polisi Kanda Maalum ya DSM inawashikilia Watu watano ambao ni Issa Karim maarufu Mdaka Bomu (33) wa Mbezi, Mohamed Juma maarufu (Miaka 31) wa Mbezi Mwisho, Selemani Seif maarufu Dullah Kishandu (34) wa Mbezi Mwisho, Samsoni Joseph maarufu Mjeuri (32) wa Mbezi na Ezekiel Kennedy maarufu Simba MC wa Mbezi kwa tuhuma za mauaji.

“May 08, 2021 majira ya mbili usiku Mikocheni A Watuhumiwa walivamia Bar iitwayo Imbizo na kumshambulia kwa mapanga na marungu Mlinzi (Regan Sylivester) na kusababisha kufariki dunia papo hapo, pia wanatuhumiwa kuhusika na tukio la unyan’ganyi wa kutumia silaha huko Mabwepande May 07, 2021 saa tatu usiku walipovamia Petrol station ya MEXONS na kuwashambulia Walinzi, Wahudumu na Wateja na kupora Tsh 2,440,000/= na kisha kupora silaha ya Walinzi aina ya short gun”———Polisi DSM
 
Kipindi cha JPM utasikia tu kuwa jeshi la police limeuwa majambazi waliojaribu kurushianana risasi na police wanamalizwa kimya kimyaa bill kutoa taarifaa huku.
 
Hongera Jeshi la Polisi. Kila mmoja anapenda maisha salama.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea na Operesheni Maalum ya kupambana na vitendo vya kihalifu Katika maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam katika dhima nzima ya Usalama wa Raia na Mali zao na limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 20 na vielelezo mbalimbali kama ifuatavyo:
Majambazi wengine huwa hawakamatwi, wanakamatwa vijambazi vidogo vidogo.
Doto james aliiba mabilioni yetu, akishirikiana na Bashiru, Philip Mpango na majambazi wenzao ambao tunawaita eti 'waheshimiwa'.

Ngoja siku JW waamue kufanya yao kama huko Afrika magharibi
 
Back
Top Bottom