Sadaka kumpa mzazi ni bora kuliko kuipeleka kwenye nyumba za ibada

Watu walioanzisha makanisa watakanusha hoja yako . Mimi nakuunga mkono , ukishawapa wazazi , angalia majirani wenye shida uwasaidie kuliko kuwapelekea mchwa waliojificha makanisani. Wengi wakiitikia wito wako makanisa mengi yatafungwa. Hawa watu wanakula kilaini Sana , eti kitendo Cha kunikumbusha Mungu anakupenda umpe sadaka ! Mimi ninajua Mungu anakupenda .
 
Kama una laki moja yako usiipeleke msikitini/kanisani kwanza fikiria mama yako hana shida binafsi ambazo anaweza kutatua kwa pesa hiyo?

Baba je?

Ndugu wengine wa karibu?

Kuna watu wazazi wao wanahangaika kutafuta ugali wa siku mtu ile package ya kula wiki hana lakini mtu huyu anachukua pesa anapeleka kwenye nyumba ya ibada.

Mungu anakuona aisee, hautaadhibiwa na Mungu kwa nini pesa yako ulimpa mzazi akatatue shida zake wakati nyumba ya ibada haijapigwa rangi n.k

Lakini Mungu anaweza kukutia adabu kwa nini mzazi wako alilala njaa wakati wewe ulipeleka pesa kwingine.

Lengo la sadaka ni kuwasaidia wasiojiweza, sasa kama mzazi wako naye hajiwezi msapoti.

Kuna kitabu nilikichungulia kinasema toa walau 10% ya kipato chako ukatoe sadaka.

Niliamua tu sadaka yangu hiyo 10% nawapa wazazi. Sina maana ya kukosoa sadaka lakini nakumbusha tu wazee wetu wana dhiki nyingi, tusijifanye wema sana kwenye nyumba za ibada wakati wazee wetu hilo salio lingewasaidia.

Wema, sadaka huanzia nyumbani kwa watu wako wa karibu.

NB ; Kama wazazi wako wanajiweza hii mada haikugusi

Uzuri ni kwamba imani zetu zinatufundisha kila kitu. Katika kutoa ili sadaka yako ipokelewe kitu cha kwanza kabisa unatakiwa kutoa kwa imani huku ukiwa na upendo na watu wako

Kumbukumbu la torati 14: 22-24
22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi (10%) katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka. 24 Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako; 25 ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako;

Hagai 1: 5-10
"5 Basi sasa, Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu. 6 Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka. 7 Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu. 8 Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema Bwana. 9 Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha. Ni kwa sababu gani? Asema Bwana wa majeshi. Ni kwa sababu ya nyumba yangu inayokaa hali ya kuharibika, wakati ambapo ninyi mnakimbilia kila mtu nyumbani kwake. 10 Basi, kwa ajili yenu mbingu zimezuiliwa zisitoe umande, nayo nchi imezuiliwa isitoe matunda yake."

Mungu wetu ni Mungu wa kiasi, na aliweka taratibu katika kutoa.....

Marko 12:17 anatuambia​

"Yesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu. Wakamstaajabia sana."

Ukitoa sadaka vibaya Mungu hapokei ni kujichosha tuu

1 Timotheo 5:8 anatuambia​

"Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.

Hakuna anayeweza sema ametoa sadaka hadi kushindwa kumtunza mzazi wake au kusaidia watu wa nyumba yake na wahitaji"

Tusimtafute Mungu sababu ya kutuwahudumia wazazi
 
Na wazazi wahakikishe shida zote za watoto na wanandugu nyumbani zimetatuliwa tayari ndipo waanze kujazia vipato kina gwaji boy.
 
Sadaka kanisani(unapo weka imani yako hata kama ni kwa mganga)
msaada kwa wasio huwez
a
Matumizi kwa familia (wazazi ndugu jamaa na marafiki)

Usichanganye
 
Watu walioanzisha makanisa watakanusha hoja yako . Mimi nakuunga mkono , ukishawapa wazazi , angalia majirani wenye shida uwasaidie kuliko kuwapelekea mchwa waliojificha makanisani. Wengi wakiitikia wito wako makanisa mengi yatafungwa. Hawa watu wanakula kilaini Sana , eti kitendo Cha kunikumbusha Mungu anakupenda umpe sadaka ! Mimi ninajua Mungu anakupenda .
Majirani unawajua vizuri wewe!

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Kuna Jamaa hapa ni Msabato
anafanya biashara zake
Kiukweli ana uchumi mzuri
kifupi amebarikiwa
sasa kanisani michango anatoa Malaki kwa Mamilioni
Ila ana mzazi wake wa kike
Dah mama ana hali mbaya
Kuanzia mavazi hadi chakula ni cha shida!
Chakula cha mawazo!
but Jamaa yeye kwake fresh
Kibaya zaidi wanaishi compound moja
Ila yenye fensi bora hata ingekuwa wapo mbali mbali huko hata mikoani!
Imefika hatua nikasikia mtu mmoja anasema yeye hawezi kwenda kanisani kuchanganika na watu kama huyo Jamaa, ambao ni wanafiki mbele ya kanisa waonekane ni wema wakati hata mzazi wake tu ana shida kibao!
Aisee inafikirisha sana!
Haws ndo nawakusudia mimi.

Mzazi ana hangaika huku wewe unafurahisha waumini.

Aisee Mungu hayupo hivyo bhana.
 
Kuna Jamaa hapa ni Msabato
anafanya biashara zake
Kiukweli ana uchumi mzuri
kifupi amebarikiwa
sasa kanisani michango anatoa Malaki kwa Mamilioni
Ila ana mzazi wake wa kike
Dah mama ana hali mbaya
Kuanzia mavazi hadi chakula ni cha shida!
Chakula cha mawazo!
but Jamaa yeye kwake fresh
Kibaya zaidi wanaishi compound moja
Ila yenye fensi bora hata ingekuwa wapo mbali mbali huko hata mikoani!
Imefika hatua nikasikia mtu mmoja anasema yeye hawezi kwenda kanisani kuchanganika na watu kama huyo Jamaa, ambao ni wanafiki mbele ya kanisa waonekane ni wema wakati hata mzazi wake tu ana shida kibao!
Aisee inafikirisha sana!
Haws ndo nawakusudia mimi.

Mzazi ana hangaika huku wewe unafurahisha waumini.

Aisee Mungu hayupo hivyo bhana.
 
Uzuri ni kwamba imani zetu zinatufundisha kila kitu. Katika kutoa ili sadaka yako ipokelewe kitu cha kwanza kabisa unatakiwa kutoa kwa imani huku ukiwa na upendo na watu wako

Kumbukumbu la torati 14: 22-24
22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi (10%) katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka. 24 Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako; 25 ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako;

Hagai 1: 5-10
"5 Basi sasa, Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu. 6 Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka. 7 Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu. 8 Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema Bwana. 9 Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha. Ni kwa sababu gani? Asema Bwana wa majeshi. Ni kwa sababu ya nyumba yangu inayokaa hali ya kuharibika, wakati ambapo ninyi mnakimbilia kila mtu nyumbani kwake. 10 Basi, kwa ajili yenu mbingu zimezuiliwa zisitoe umande, nayo nchi imezuiliwa isitoe matunda yake."

Mungu wetu ni Mungu wa kiasi, na aliweka taratibu katika kutoa.....

Marko 12:17 anatuambia​

"Yesu akajibu, akawaambia, Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na yaliyo ya Mungu mpeni Mungu. Wakamstaajabia sana."

Ukitoa sadaka vibaya Mungu hapokei ni kujichosha tuu

1 Timotheo 5:8 anatuambia​

"Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.

Hakuna anayeweza sema ametoa sadaka hadi kushindwa kumtunza mzazi wake au kusaidia watu wa nyumba yake na wahitaji"

Tusimtafute Mungu sababu ya kutuwahudumia wazazi
Hagai kamaliza kabisa, hawajui kila mtu ataubeba msalaba wake, mazazi hatabeba maovu ya mtoto wala mtoto hatabeba ya mzazi, kila kitu kifanyike kwa nafasi yake! Mzazi ni MUNGU wa pili hivyo wakwanza yupo pia.

Safi mkuu

Bila shaka kwa uislamu sadaka ni tofauti sana na zaka tena sana.

Sijajua katika ukristo ,ila uislamu zaka na sadaka ni tofauti,zaka wanatoa watu waliofikia kiwango fulani cha pesa kila mwaka wanatoa,hii iwe wanasaidia wazazi au laa lazima watoe.

Kwenyw uzi nimegusia sadaka sio zakka
 
Hakuna excuse kwenye kutoa. Mungu na serikali wana miongozo yao iliyo rasmi kabisaaa

Mungu alishasema Kipimo chake ni 10% ya kila tunachoingiza iwe ni pesa au bidhaa au mazao...
Serikali nayo TRA ameshaweka viwango vyake

Na kinachobaki bado kikubwaaaa ndio tuwaangalie wazazi, ndugu na wahitaji wengine
Hapa ni kujiongeza na kujiongoza mwenyewe kwa kuangalia uhitaji wa mtu
 
Safi mkuu

Bila shaka kwa uislamu sadaka ni tofauti sana na zaka tena sana.

Sijajua katika ukristo ,ila uislamu zaka na sadaka ni tofauti,zaka wanatoa watu waliofikia kiwango fulani cha pesa kila mwaka wanatoa,hii iwe wanasaidia wazazi au laa lazima watoe.

Kwenyw uzi nimegusia sadaka sio zakka

Zaka ni tofauti na sadaka...

Zaka ni 10% ya kipato chochote anachotakiwa kutoa mtu yoyote anayelipwa kama ujira au anachozalisha. Iwe ni mshahara, mazao, mifugo....

Sadaka inatolewa kwa kiasi unachojaaliwa.......

Ila hili ya kutokutoa huduma kwa mzazi sababu eti unamtolea Mungu limekaa upandeupande
 
Sijajua umeupokea vipi uzi wangu ama umeufahamu vipi lakini makusudio tangu kama nilivyosema ni hivi..

Jamaa anamsahau mama anaona kwa kuwa haombwi basi hatoi kwa mama,lakini ibadani ikiitajika sadaka huyo wa mwanzo kutoa ilhali wazazi wake hawana hali.

Huyu ndio niliyemkusudia,sio kwamba anasema mwenyewe kwamba anashindwa kuwapa wazazi kwa sababu ya sadaka no,bali anasahau kama wazazi wake nao wana shhida zao.

Wazazi wengi sasa hivi hawawaombi sana watoto wao kwa sababu wanajua kuwa ukiwaomba utaonekana mswahili,wengi wanakufa na tai shingoni.
 
Unajua unaweza ukamuona mtu hasaidii wazazi wake, lakini kilichopo ndani hukijui, familia hizi zina mambo mengi sana, kuna mtu alikuwa anawapa kama kawaida mpaka yeye mwenyewe anakosa au anapungukiwa, Baba kaoa mama anakusanya watoto wa ndugu lakini akiuliza anajibiwa mimi sijawabagua nyie ,siku kakosa lawama anawanyima au wakigawana kile kidogo wazazi wanalalamika na hao wazazi tuseme vipi?

Nimekuelewa safuher

Ulweso umeongea ukweli....
Wakati mwingine unakuta wazazi walifanya yao yasiyompendeza Mungu sasa wako kwenye kutumikia adhabu ya Mungu.
Mambo ya rohoni ni magumu sanaaaa, tumwombe Mungu ufahamu na hekima ya kuishi ndani ya mapenzi yake

Kutoka 34: 6-7
"Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili,

si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;
mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu,
mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi;
wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe;
mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne."
 
Lengo la sadaka ni kuwasaidia wasiojiweza, sasa kama mzazi wako naye hajiwezi msapoti.
Hilo sio lengo la sadaka. Kutoa sadaka kuna lengo la kumrudishia Mungu sehemu ya baraka alizokujalia, ambapo zinatakiwa zisaidie kueneza utukufu na ukuu wake
 
PEngine tunatofautiana imani mkuu.

mimi siamini kama lengo la sadaka ni kumrudishia MMunguMungu yeye hanufaiki na sadaka zetu na wala hadhuriki na ubakhili wetu.

pengine tunatofautiana imani.

sadaka inatolewa ili iwasaidie wengine pasi na kuangalia kipimo fulani cha pesa zako.
 
Unajua unaweza ukamuona mtu hasaidii wazazi wake, lakini kilichopo ndani hukijui,
Ni kweli ulweso,lakini mimi uzi wangu haugusii hii situation.
Mtu ataangalia mwenyewe na hali ya familia yake ijapokuwa hakuna kosa ambalo atakufanyia mzazi alafu ikawa umhukumu kwa kumnyima matumizi.
kuna mtu alikuwa anawapa kama kawaida mpaka yeye mwenyewe anakosa au anapungukiwa, Baba kaoa mama anakusanya watoto wa ndugu lakini akiuliza anajibiwa mimi sijawabagua nyie ,siku kakosa lawama anawanyima au wakigawana kile kidogo wazazi wanalalamika na hao wazazi tuseme vipi?
Bado huu sio kisingizio cha kumnyima mzazi mahitaji mkuu.

Unajua tumeamrishwa na Dini zetu kuwatendea wema wazazi,Dini haikusema kuwa umfanyie wema mzazi ambae ni mwema na usimfanyie wema au kumhudumia mzazi mbaya.

Sasa unapovunjika moyo kumsaidia mzazi ambaye unaona kuna vitu anakosea basi ujue na huyo mzazi anahitaji huduma yako pia

Kama ambavyo sisi tulihudumiwa na wao utoto wetu haina maana kuwa tulikuwa wasafi tu,tulikosea sana lakini waliendelea kutuhudumia,na sisi tuendelee na moyo huu.

Hivyo ndugu ulweso hakuna nyudhuru ya maana ambayo mtu atasema kwa hili baba namweka na njaa,no no no.
 
Back
Top Bottom