Sadaka zimekuwa nyingi sana, dini imekuwa biashara

Unakuja na mihasira asubuhi
 
[emoji91][emoji16][emoji28][emoji23] Sema yote mkuu.

Wenzio Kanisa tumeamishia Nyumbani. Kristo tupo nae.
Bora hivyo mkuu, mimi kwa kweli la lunch na Bwana Yesu liliniacha hoi(KKKT hawa) RC lile la kusema sadaka irudiwe mpaka laki saba zipatikane na hapo mnaamka benchi kwa bench, na kumbuka huo /hiyo ni sadaka ya mwisho na zimeshapita kama tatu nyuma.
 
Hizi sadaka zinachanganya sana, misaa masaa 3, lkn masaa 2 zinazungumziwa hela tuu. Ukitaka mchungaji akuguse, toa sadaka. ya kueleweka, ili uende mbele akuombee kwa kukugusa Wasio na hela hawana nafasi. Wachungaji wa Nigeria wamejitajirisha mpaka wanatembelea private jets.
 
Ila hizi imani hizi, eti wale mitume na manabii wote hakuna Mwafrika hata mmoja, then unakuta mwafrika yuko bize anaimba "Ningekuwa na mabawa ningepaa niende nyumbani kwa bwana nikamwone Ayubu, Ibrahim na the rest.."
Wakati Gwajiboy yuko hapa ila hataki kwenda kumwona (Joke).
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ni kweli sadaka zimekuwa nyingi sana..makanisa Yesu anawaona na siku ya hukumu mutajibu
Sadaka ya ukombozi
Sadaka ya fungu la kumi
Sadaka ya ujenzi
Sadaka ya nabii
Sadaka ya upebdo
Sadaka ya shukuranj
Sadaka ya kumtegemeza mchungaji
 
Unaposema Wakristu ni weupe kichwani, unamaanisha Waislamu wako vizuri kichwani?
Huu utani sasa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hakuna kanisa takatifu, makanisa yote ni utapeli kama kawaida. Kumbuka zamani roma walikua wanatoza hela kuondoa dhambi, imagine 😂.
 
Sa
Sadaka inahusiana na Imani yako mbele za Mungu, sadaka ni Ibada. Unapojandaa kwenda kanisan ombea kabisa sadaka mbele za MUNGU kisha jongea nyumba ya Ibada. Hata ukute vikapu mia toa ile ulijiandaa nayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…