Navyozidi kutumia logic.. naona mapungufu mengi sana makanisani na mazuri mengi sana dini ya wenzetu waislamu..
Sadaka kwenye ukrito imekaa kipigaji pigaji sana hasa fungu la kumi na sadaka zingine kibao. Angalau waislam sadaka inasisitizwa itolewe kama zaka kwa maskini, wajane, wagonjwa, na makundi mengine yenye shida ,,katika nguzo zao za uislam.
Nimeshauguza sana mama yangu muhimbili na moi.. kila mara akilazwa nikienda asubuhi kumuona naona makundi ya waislam wanatembelea wagonjwa waliolazwa na kuwapa uji na vyakula asubuhi .. sio ndugu zao bali ni utaratibu wa dini yao wanasaidia wagonjwa ambao hawana wa kuwapa vyakula.. mimi ni mkristo sijawai kuona kundi la wakristo likifanya hivyo hata siku 1 katika siku zote nilizokuwa naenda moi na muhimbili kumuona mama.
Makanisani mahubiri yanasisitiza sadaka tu na hizo sadaka hazijulikani zinaenda wapi? Maana hata shule za kanisa zilizojengwa kwa sadaka zetu bila kulipa ada mwanao anafukuzwa