Sadaka zimekuwa nyingi sana, dini imekuwa biashara

Sadaka zimekuwa nyingi sana, dini imekuwa biashara

Hivi vitu vya kijamii,ukiamua kuwa Bandidu, ufahamu consequences na repercussions zake...
Ni vizuri kutambua mbeleni,kwa kuchukua uamuzi huo, athari zake kwangu na familia yangu ikoje..
Kuna watu wanakuwa na misimamo dhaifu,huduma za kanisa anahitaji,ushiriki wake hafifu,alafu utegemee mteremko, lazima either wewe mwenyewe au familia yako itaadhirika kwa namna moja au nyingine.



Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Navyozidi kutumia logic.. naona mapungufu mengi sana makanisani na mazuri mengi sana dini ya wenzetu waislamu..

Sadaka kwenye ukrito imekaa kipigaji pigaji sana hasa fungu la kumi na sadaka zingine kibao. Angalau waislam sadaka inasisitizwa itolewe kama zaka kwa maskini, wajane, wagonjwa, na makundi mengine yenye shida ,,katika nguzo zao za uislam.

Nimeshauguza sana mama yangu muhimbili na moi.. kila mara akilazwa nikienda asubuhi kumuona naona makundi ya waislam wanatembelea wagonjwa waliolazwa na kuwapa uji na vyakula asubuhi .. sio ndugu zao bali ni utaratibu wa dini yao wanasaidia wagonjwa ambao hawana wa kuwapa vyakula.. mimi ni mkristo sijawai kuona kundi la wakristo likifanya hivyo hata siku 1 katika siku zote nilizokuwa naenda moi na muhimbili kumuona mama.

Makanisani mahubiri yanasisitiza sadaka tu na hizo sadaka hazijulikani zinaenda wapi? Maana hata shule za kanisa zilizojengwa kwa sadaka zetu bila kulipa ada mwanao anafukuzwa
💯
 
Watu wa Mungu mnasoma maandiko?

K/TOLATI 4:22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.

MALAKI 3:10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

Watu wa Mungu toeni pesa asee, hizo ni roho za uchoyo asee, kama unafanikiwa na unapata pesa toa sana ili uweze kupata sana na kadiri unavyofupisha mkono wako ndivyo hivyo hivyo pesa iliyo karibu nawe inavyozidi kusogezwa mbali nawe.
 
Dini sahihi na ya kweli ni Waislamu tu hawana makuu kbs.. haya mengine na hizi kanisa za mabati ndio balaaa. Mshika pesa ni mke wa mchungaji. Kuna siku niliwafuma wazee wa kanisa wakigawana mpunga Mwambao restaurant Dom.

Duu umetishaa[emoji23][emoji23]
 
Lazima mtoe povu kama mnaviela vyenu vya mawazo, kingine mnasali makanisa gani nyie, mfano luther sadaka sio lazima na fungu la kumi ukipeleka hata 5000 kutoa tena inaweza kupita hata miiezi, katika ukristo kuna fundisha watu kufanya kazi na kutafuta pesa ndio maana ukiona michango ujue unaamshwa upambane ndio maana matajiri wengi ni wakristo duniani hao wengine ni mmoja moja fanya utafiti uone waislam wengi ni masikini kinomaa coz din yao kila kitu ni simple sasa hapo inafundisha utafutaji kuwa chini mfano angalia nchi za kiislam africa ni masikin zakutupa, angalia sasa za wakristo wengi mfano south africa au nigeria pande za lagos matajiri kibao nenda kule kaskazin kwa waislam masikin kibao so kama vp hamieni huko kwenye usimple mnakotaka
Unaongea nini wewe mbona sikuelewi! We ulisikia wapi waislam wengi maskini!
 
Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
Matendo ya Mitume 10 :4

Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.
Waebrania 11 :4



  • Malaki 3 :8_11 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
  • Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
    10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha,
  • Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
    Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya..
 
Jumapili iliyopita kulikuwa na michango minne..eti kapu la mama la redio maria,mara kusomesha wamisionari..yaani full mizengwe.

Kilichoniacha hoi zaidi ni kutaja jumuia zilizotoa fedha kidogo kwenye zaka/fungu la kumi na exactly kiasi walichotoa..huku tukiambiwa kutoa unatoa ulichonacho,vipi kama hao wanajumuia hawana?

RC mizengwe imezidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kanisani kwetu viongozi wa jumuia waliitwa mbele mmoja mmoja kueleza kiasi walichotoa na kilichobaki waeleze watamalizia lini!! Ilikuwa ni mchango wa ukarabati wa paa la kanisa, hapo hapo kulikuwa na michango ya sijui kapu la mama, kuchangia watoto wanaoenda kujifunza rozali na michango mingine mingi mpaka nimeisahau!
 
Kanisani kwetu viongozi wa jumuia waliitwa mbele mmoja mmoja kueleza kiasi walichotoa na kilichobaki waeleze watamalizia lini!! Ilikuwa ni mchango wa ukarabati wa paa la kanisa, hapo hapo kulikuwa na michango ya sijui kapu la mama, kuchangia watoto wanaoenda kujifunza rozali na michango mingine mingi mpaka nimeisahau!
Na hapo ibada na mahubiri unakuta wamelipua tu fasta..ila sasa ikifika muda wa matangazo na mihimizano ya michango hapo wanakaa sana kwa msisitizo..

I'm sick tired of this.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wa Mungu mnasoma maandiko?

K/TOLATI 4:22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.

MALAKI 3:10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

Watu wa Mungu toeni pesa asee, hizo ni roho za uchoyo asee, kama unafanikiwa na unapata pesa toa sana ili uweze kupata sana na kadiri unavyofupisha mkono wako ndivyo hivyo hivyo pesa iliyo karibu nawe inavyozidi kusogezwa mbali nawe.
Ukipigwa shavu la kushoto,geuza na shavu la kulia
 
Kuna shida mahali namna hawa wachungaji na manabii wanavyofundisha na kuhimiza kuhusu utoaji wa sadaka, aina ya maisha ya waumini wao, na aina ya maisha wanayoishi wao na familia zao, wakati mwingine sipati connection kabisa....
 
Ni bora mpungue masikin nyinyi mnapenda vya bure ndio maana waislam wengi ni masikini kinoma fanya utafiti coz ukristo unataka watu wafanye kazi yaani wajitume
Kwa hili nakupinga Sio kweli dini ya kiisilamu imehimiza sana kufanya kazi na kufanya kazi ni sehemu ya ibada ni kweli waisilamu ni maskini sababu sio wengi waliosoma sana hizo zaka zenyewe hazitolewi kihalisia lkn sio maskini kama unavyosema la muhimu ukifanya wema unajifanyia mwenyewe na ukifanya ubaya vile vile unajifanyia mwenyewe ,dini zote zimehimiza hivyo .
 
Napendekeza huu uzi ufutwe, maana unaviashiria vibaya kutoka kwa wafia dini za kigeni.

wapumbavu wanapokutana na kuanza kutukanana/kushindana kwa vigezo vya imani za kuletewa hapo kunakuwa hakuna namna zaid ya kuwashughirikia wote.

Izo sadaka zenu mnazotoa kila siku makanisan na kwenye magenge yenu ya ibada, zmewasaidia nini?

huyo Mungu wenu tangu muanze kumuomba kwa kumtolea, kawasaidia kitu gani??

enyi wajinga na wapumbv mtaibiwa mpka lin?, yaan unadanganyikaje kutoa mali yako sabbu unataka kubarikiwa,

siri ya kubarikiwa ni kufanya kazi kwa bidii, kuwa na nidhamu ya pesa, na mwisho kuwasaidia ndugu/jiran walio na uhitaji.

huyo Mungu/Allah mnae kesha kumuabudu na kumtolea sadaka anawaibia kupitia upumbv wenu, hizo sadak zilitungwa na hao washenz walioleta dini, kwa malengo ya kuongeza uchumi mkubwa wa makanisa ili yazidi kuwatawala vzur kupitia serkali zake vivuli, pia kujiimarisha zenyewe kiuchumi na kiintelejensia,

achaneni na dini, dini hazina maana kwa mtu mweusi, dini hazna ukweli wowote, ndyomaana kila siku mnatwangana wote na kupingana kwa kila kitu.

imani ya kwel ni kutenda matendo mema, kwa mujibu wa mila na desturi za kiafrika, achanen na izo imani za kishenzi.

wengine tulishatoka huko kwenye jela ya akili(dini) tupo huru, hatuna hofu ya moto wa jehanam, hatuna hofu ya kifo wala kumuogopa huyo Mungu wenu wa kusadikika, we are free to go into hell, if exist[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].., ...

FB_IMG_16366191610457395.jpg
 
Mimi nilishaacha kwenda kanisani. Nimeenda RC sadaka kama tuko kwenye Vikoba tena bora vikoba mwisho wa mwaka unapata chako wakati huko mwisho wa mwaka unatoa tena zaka. Jumuiya ndiyo usiseme, kusali ni five mnts tu then michango inaanza. Nakajaribu KKKT, huko ndiyo usiseme, eti kuna mpaka lunch na bwana Yesu. Nikajua tunapiga msosi na Bwana Yesu kumbe hakuna kitu. Niishie hapa nisiharibu imani za watu.
Nimecheka sana,lunch na Bwana Yesu tena😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom