Sadaka zimekuwa nyingi sana, dini imekuwa biashara

Hivi vitu vya kijamii,ukiamua kuwa Bandidu, ufahamu consequences na repercussions zake...
Ni vizuri kutambua mbeleni,kwa kuchukua uamuzi huo, athari zake kwangu na familia yangu ikoje..
Kuna watu wanakuwa na misimamo dhaifu,huduma za kanisa anahitaji,ushiriki wake hafifu,alafu utegemee mteremko, lazima either wewe mwenyewe au familia yako itaadhirika kwa namna moja au nyingine.



Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
πŸ’―
 
Watu wa Mungu mnasoma maandiko?

K/TOLATI 4:22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.

MALAKI 3:10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

Watu wa Mungu toeni pesa asee, hizo ni roho za uchoyo asee, kama unafanikiwa na unapata pesa toa sana ili uweze kupata sana na kadiri unavyofupisha mkono wako ndivyo hivyo hivyo pesa iliyo karibu nawe inavyozidi kusogezwa mbali nawe.
 
Dini sahihi na ya kweli ni Waislamu tu hawana makuu kbs.. haya mengine na hizi kanisa za mabati ndio balaaa. Mshika pesa ni mke wa mchungaji. Kuna siku niliwafuma wazee wa kanisa wakigawana mpunga Mwambao restaurant Dom.

Duu umetishaa[emoji23][emoji23]
 
Unaongea nini wewe mbona sikuelewi! We ulisikia wapi waislam wengi maskini!
 
Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
Matendo ya Mitume 10 :4

Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.
Waebrania 11 :4



  • Malaki 3 :8_11 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
  • Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
    10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha,
  • Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
    Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya..
 
Kanisani kwetu viongozi wa jumuia waliitwa mbele mmoja mmoja kueleza kiasi walichotoa na kilichobaki waeleze watamalizia lini!! Ilikuwa ni mchango wa ukarabati wa paa la kanisa, hapo hapo kulikuwa na michango ya sijui kapu la mama, kuchangia watoto wanaoenda kujifunza rozali na michango mingine mingi mpaka nimeisahau!
 
Na hapo ibada na mahubiri unakuta wamelipua tu fasta..ila sasa ikifika muda wa matangazo na mihimizano ya michango hapo wanakaa sana kwa msisitizo..

I'm sick tired of this.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukipigwa shavu la kushoto,geuza na shavu la kulia
 
Kuna shida mahali namna hawa wachungaji na manabii wanavyofundisha na kuhimiza kuhusu utoaji wa sadaka, aina ya maisha ya waumini wao, na aina ya maisha wanayoishi wao na familia zao, wakati mwingine sipati connection kabisa....
 
Ni bora mpungue masikin nyinyi mnapenda vya bure ndio maana waislam wengi ni masikini kinoma fanya utafiti coz ukristo unataka watu wafanye kazi yaani wajitume
Kwa hili nakupinga Sio kweli dini ya kiisilamu imehimiza sana kufanya kazi na kufanya kazi ni sehemu ya ibada ni kweli waisilamu ni maskini sababu sio wengi waliosoma sana hizo zaka zenyewe hazitolewi kihalisia lkn sio maskini kama unavyosema la muhimu ukifanya wema unajifanyia mwenyewe na ukifanya ubaya vile vile unajifanyia mwenyewe ,dini zote zimehimiza hivyo .
 
Napendekeza huu uzi ufutwe, maana unaviashiria vibaya kutoka kwa wafia dini za kigeni.

wapumbavu wanapokutana na kuanza kutukanana/kushindana kwa vigezo vya imani za kuletewa hapo kunakuwa hakuna namna zaid ya kuwashughirikia wote.

Izo sadaka zenu mnazotoa kila siku makanisan na kwenye magenge yenu ya ibada, zmewasaidia nini?

huyo Mungu wenu tangu muanze kumuomba kwa kumtolea, kawasaidia kitu gani??

enyi wajinga na wapumbv mtaibiwa mpka lin?, yaan unadanganyikaje kutoa mali yako sabbu unataka kubarikiwa,

siri ya kubarikiwa ni kufanya kazi kwa bidii, kuwa na nidhamu ya pesa, na mwisho kuwasaidia ndugu/jiran walio na uhitaji.

huyo Mungu/Allah mnae kesha kumuabudu na kumtolea sadaka anawaibia kupitia upumbv wenu, hizo sadak zilitungwa na hao washenz walioleta dini, kwa malengo ya kuongeza uchumi mkubwa wa makanisa ili yazidi kuwatawala vzur kupitia serkali zake vivuli, pia kujiimarisha zenyewe kiuchumi na kiintelejensia,

achaneni na dini, dini hazina maana kwa mtu mweusi, dini hazna ukweli wowote, ndyomaana kila siku mnatwangana wote na kupingana kwa kila kitu.

imani ya kwel ni kutenda matendo mema, kwa mujibu wa mila na desturi za kiafrika, achanen na izo imani za kishenzi.

wengine tulishatoka huko kwenye jela ya akili(dini) tupo huru, hatuna hofu ya moto wa jehanam, hatuna hofu ya kifo wala kumuogopa huyo Mungu wenu wa kusadikika, we are free to go into hell, if exist[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].., ...

 
Nimecheka sana,lunch na Bwana Yesu tenaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…