Wakuu nina maswali ningependa sana Mkurugenzi wa Mashitaka ayajibu. Moderators naomba msichanganye huu uzi na mwingine, kwa kuwa hapa najaribu kudadisi uwezo wa Watendaji wetu wa kufanya kazi kwa uelewevu wa sheria badala ya kukurupuka kutafuta kiki za midia.
Ukienda Tovuti ya Dar es Salaam Airport utakutana na kanuni hizi zinazohusu kuingiza fedha za kigeni nchini;;
Dar es Salaam airport : rules and customs formalities
Je, kutokana na kanuni hizi, kuna tatizo Kubenea kukutwa na USD 8000? (Naelewa kwamba kiwango cha juu cha ku-declare ni ikiwa una zaidi ya USD 10,000)
Pili, Kubenea amekamatwa akiwa Tanzania, na yeye ni Mtanzania. Ni vipi Mkurugenzi wa Mashitaka anamfungulia mashitaka Kubenea kwa kuwa nchini mwake? Na je, kuwa na risiti na hoteli nchini Kenya ni utibitisho tosha kwamba alikuwa Kenya?
Mkurugenzi wa Mashitaka Tanzania ameamua kujiajiri na kufanya kazi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Kenya?
Hivi kwa mfano, nikienda Kenya, nikagundua kuna watu wananifuatilia kutaka kuniua, nikatoroka kurudi nyumbani Tanzania bila kupitia mpakani rasmi, nikifika Tanzania nitafunguliwa mashitaka?
Kwa hiyo basi, Mkurugenzi wa Mashitaka amekurupuka kumfungulia Kubenea mashitaka kwa lengo la kupata kiki ya media na CCM dhidi ya mpinzani?