plumber hydrogen
JF-Expert Member
- Feb 17, 2022
- 881
- 1,537
Hatari
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chali unaijua risasi wewe?Very interesting story..... Bila ya mwendelezo.
Nina mpango wa kuitembelea Congo hasa Yale maeneo ya Kivu kusini au Goma kwa ujumla, mpaka sasa naendelea kukusanya taharifa za kiintelejensia kuhusu ayo maeneo, ingawa naambiwa kuna watu makatili sana lkn Mimi uwa napenda sana awo watu makatili kwa maana ndiyo watu ambao ukiibahatika kuzoeana nao wakakubali basi utakuwa unaweza kutimiza lengo lako kiuraisi sana,Congo ni taiga ambalo limejaa rasilimali kibao unaambiwa kuna maeneo nyumba zimekandikiwa udongo wa dhaabu ukiweka Mashine kwenye kuta zao ngoma inasoma PPM za kutosha, na kwa wale wazee wa Carbon uko ndo balaa unaambiwa mkamuo moja tu wa tani moja ya Carbon unaweza toka na 1.5 kg ya gold...unaambiwa mzigo upo wa kutosha.
Vijana tupunguze uoga, twende tukapambane....
Ntajitahidi as soon as possible. Ngoja hawa wengine nao wamalizie zaoDah lini sasa????[emoji134][emoji134]
Uliivyokua unampiga mtu kachabariUmetaja gisenyi, nikakumbuka mbali sana
Harafu jamaa Wala hajibuMkuu hata kwangu hazifunguki! Sijui shida ni nini?
Hii mkulu mpaka naogopa. Tanzania kwa kweli tuitunze amani yetu.ni aherl kula ugal na chumv ila amani.huko batakula ya kongo nguvu kumayi.HII SASA NDO STORY YA KIUME. SIYO ZILE ZA KIPUUZI ZA KUTIANA NA MISUKULE.ZIMEJAA UONGO MWINGI. NJOONI MSOME STORY YA KIUME HAPA.
Mleta mada kaliweka wazi hilo alipokuwa Rwanda. Na Rwanda wanavyojisifu kuna amaniHii mkulu mpaka naogopa. Tanzania kwa kweli tuitunze amani yetu.ni aherl kula ugal na chumv ila amani.huko batakula ya kongo nguvu kumayi.
Congo nitakayoenda mimi ni ya kariakoo tu.Hii mkulu mpaka naogopa. Tanzania kwa kweli tuitunze amani yetu.ni aherl kula ugal na chumv ila amani.huko batakula ya kongo nguvu kumayi.
Nimeipenda sana. Tuletee zaidi..
Katika harakati zangu za kujikomboa na umasikini, niliamua kufanya ziara ya kusaka fursa Mpya nchini Congo. Nilikua tayari nimeshapata masimulizi mengi ya upatikanaji wa madini ya dhahabu na Rubi.
Ni mnamo mwaka Juzi mwanzoni nikiwa mji wa Uvira amabapo jilikutana najamaa Akiwa na jiwe alilo dai kuwa ni Rubi
Baada ya mazungumzo marefu jamaa alikubali kunipa jiwe Moja ambalo alisema kuwa alishawahi kulipeleka Kigali Rwanda lakini katika vipimo ilitoa majibu yanayo Changanya. Ilisoma upande Moja ni Rubi na wakati mwingine inasoma Spinel. Sasa akanionesha ndoo imekaa mawe ya Kila namna. Kazi yangu nilitakiwa kwanza kwenda Tanzania kupima jiwe hilo ili tujue ni aina Gani ya jiwe Kisha nitafute mteja wa Uhakika ambaye tutakuwa tunampa Mzigo.
Kazi hiyo nikaichukua na kuanza safari, sikuhiyo nililala Bujumbura na keshoyake nikalala Kigoma. Asubuhi nilianza safari mpaka Arusha. Pamoja na kuzongwa na matapale na kashkash nyingi nilifanikiwa kufanya vipimo na bahati mbaya jiwe lilikua feki.
Pale Arusha nilikutana na wadau wengi sana na kupewa michongo nankutiwa moyo sana. Nilianza kuiona Dunia ya dealers. Sasa kazi ilaanza kutafuta connection ili nikasake Mzigo. Hapo ndipo safari wa Kivu kaskazini ikaanza.
Kiukweli sikuwa najua mawazo yangu ni hatari kiasi gani lakini laiti ningelijua pengine ningeanza kuungama dhambi zangu kwanza kabla ya kuanza safari katika ukanda wa damu mbichi.
Wakati ukawadia na safari ikaanza, niliambiwa nitafute biashara ya kwenda mayo ili nizugie kuingia mayo maeneo ya ndani na machimboni. Kwanza nikawaza kupeleka Nguo za kiume Jeans za masela na Viatu moka za Bakulutu na Kisha nikafikiria kupeleka Mchele. Baada tathmini jikapeleka Jeans Viatu na Samaki. Nilidhamilia kukutana na kamii ya Kila namna nanjinsia zote nilidhamilia kufa au kurudi na Mali. Militia taarifa za AWALI kujua hata mavazi ninayotakiwa kuvaa nikiwa huko. Nilihakikisha ninachukua kilataarifa Kwa uzito unao stahili.
Nilijifunza kuhisabu na kutaja pesa Kwa kifaransa, ndani ya wiki Moja nilijua kuhesabu Moja mpaka Milioni na kutaja pesa na maneno muhim ya kibiashara. Mfano Congo neno Kuuza wao linamaana ya kununua kuuu. Nipatie, kombola, mbasela na maneno mengine kama kutaja rangi na kusalimia. Bahati ni kwamba Kiswahili Cha Kivu kinafanana sana na Kiswahili Cha Tanzania Bara tofauti na hawachanganyi sana french kama wale wa Lubumbashi na Kinshasa.
View attachment 2497368
Safari ilianza Kwa kupitia Burundi Kisha kuingia mji wa Uvira. Hapo nililala na kesho nikapanda Hiache kwenda Mji wa Bukavu. Nilikua na machaguo mawili aidha kupitia Barabara ya ndani ya Congo au kupitia Rusizi Kisha Rwanda na kurudi tena Congo. Barabara ya ndani ya Congo ni mbaya sana na hatari sana, wanapita watu wahalifu na wanao ogopa ukaguzi wa Rwanda na ukifika unafanyiwa sherehe yaani makorongo na magari kuanguka sio habari tena, kutekwa na kuuwawa ni kawaida kuliko kusaliklmiana. Hii inaitwa Barabara ya Ngomo(Kaburi wazi)
Changamoto ya kupitia Rwanda, ukiwa na Visa ya Dola 50 basi ukiingia Rwanda Visa ya Congo imeisha na ukitaka tena kuingia Congo Kwa kutokea Barabara mchepuko ya Rwanda basi utalazimika kulipia Visa tena, kwahiyo kupitia njia hiyo utalipa Dola 200 kwenda na kurudi. Suluhisho ni Visa ya Dolar100 ambayo unapewa miezi mitatu na unaweza kutoka Congo na kuingia kadili uwezavyo. Hilo nilisha lifuatilia mapemaa, nikawa na Visa ya Dola100 nikapita Rwanda. Kuna mengi hapa Rwanda lakini kwakua sio mada ya Leo itoshe kusema ni Dunia tofauti sana. Tuishi bongo tu, amani inatosha.
Sasa niliingia mjini Bukavu kupitia mpaka wa Rusizi. Pale Bukavu wakati nimeingia nikakuta watu wanafunga maduka na kukimbia kujificha, nilipojaribu kuuliza wakasema Kuna vita imetangazwa M23 wanaingia Leo. Hapo nilitetemeka sana, nikawaza nirudi Rwanda lakini ukaguzi na Mahojiano ya Rwanda yalinipa hofu, maana ilifika wakati nashuhswa kwenye gari nafanyiwa Mahojiano maalum . Nilishangaa Kila yulipopita nakuta askari wanajua Kuna Mtanzani Yuko kwenye gari. Nilikua nahojiwa Kwa muda mrefu mpaka abiria wanalalamika, abiria Wote walikua Wakongo na karoko mswahili Mimi, askari wa Rwanda hawamuelewi wanashangaa Mtanzani kupitia pale.
Sasa Hali Ile ilinipa hofu ya kurudi Rwanda na nikakumbuka adhima yangu Bado, safari yangu Bado na lazima nifike.
Hapo nilisajili lakini ya Simu na kuweka vocha niajiunga mitandao yote na kupata dakika 3 Kwa Buku...
Haraharaka nikapita mtu wa toroli wao wanapita shareti, nikapakia mizigo tukaelekea Bandarini. Kutoka Bukavu kwenda Guma Kuna ziwa Kivu hapo unapanda meli usiku Kucha unafika kesho Asubuhi. Lengo langu niondoka Bukavu na usiku niwe kwenye meli ili hata vita ikitokea Mimi nakua kwenye meli.
Bandarini nilikuta Meli nyingi ila nikaamua kupanda "Emanele04" waniita Emauele katre, hii Bei yake Iko juu na wanapanda watu wenye uwezo na mabishoo. Lengo langu nilitaka kuanza kukutana na watu ambao wanaweza kunipa michongo ya machimbo au kupata connection za dealer wazuri. Katika safari yangu nilikua mkimya sana kwani Kila nilipo jaribu kuongea watu waligeuka kunitazama, nikagindua Kiswahili changu kinaniumbu jambo ambalo sikulitaka hasa kulingana na treatment ya Wanyarwanda.
Usiku niliingia Club na kukaa Kwa muda Kisha nikarudi, mpaka wakati huo sikupata mtu wa kuanza mazungumzo naye. Tukiwa njiani upande Moja nchi kavu kulikuwa Giza huko ni Congo kisiwa kinaitwa Idjwi na upande mwingine Kuna mataa sana, huko ni Rwanda na mataa yale ni miji na vijiji.
Asubuhi tulifika Bandarini Goma. Hapo nilikuwa makini kuangalia watu wenye mizigo kama yangu hasa samaki ili nijue wanako wapeleka. Kuna dada Moja alikua na Samaki mwengi. Niliadhimia kujiweka karibu yake. Wakati anapakia kwenye gari kupeleka stoo ndipo nikasogea na kumuomba anipakilie Mzigo wangu nitachangia garama, dada yule alikubali na Alipo niuliza napeleka wapi nikamwambia Kuna mtu tutamkuta hapo mbele ndiye anajua stoo ilipo, lakini haikua kweli.
Tulienda mpaka nakoenda yeye, na tukiwa njiani nilikwambia ukweli kuwa sina stoo Bali nimekuja tujaribu biashara. Alipo niuliza Bei za Samaki Tanzania nilimdanganya nikamwambia Bei ya chini sana kiasi akawa anatamani nimpeleke huko chimbo. Leongo langu lilitimia na tulipo fika stoo kitu cha kwanza alimueleza mume wake kuhusu Bei za Samaki Tanzania na kuanzia hapo hao wakawa weneji wangu. Kesho yake nilizunguka mjini Goma mpaka sehem inaitwa Bireree hapo ni mjini na ndipo mpakani na Gisenyi Rwanda, yaani border Ile Iko kama ilivyoisha Tunduma na Nakonde Zambia. Nyumba zimeungana za Rwanda na Congo. Soko na mishe nyingi ziko upande wa Congo . Asubuhi Wanyarwanda wanavuka kufungua biashara zao huko Goma ni jioni kurejea kwao.
Calm down , Akifanya hivo utamlipa, ridhika na kidogo unachopata na ukizingatie,watu mnaoletaga story hakikishen mmeandika story zenu zote mmalize then msave pemben ndo mlete humu kidogo kidogo kuliko mnaanza vizur mkishaona watu wamekua wengi ndo mnajifanya na nyinyi eti mna majukumu mengine wakati masniper tukiwafatilia tunaona mnaingia mara kibao tu umu..
Me nashangaa watu hata kama jamaa yupo kwenye mabomu wanataka story iendeleeKwani amesema story inaendelea? Maana lawama zimekuwa nyingi.
Msimuliaji yupo huko uwanja Kivita alipopata muda wake mchache akaone asimulie alichokutana nacho.watu mnaoletaga story hakikishen mmeandika story zenu zote mmalize then msave pemben ndo mlete humu kidogo kidogo kuliko mnaanza vizur mkishaona watu wamekua wengi ndo mnajifanya na nyinyi eti mna majukumu mengine wakati masniper tukiwafatilia tunaona mnaingia mara kibao tu umu..
Fact!!!!Shida ukishafanya kazi za kikekike unaanza kuwa na mambo ya kikekike Hilo ndio tatizo langu kwa vijana wa kiume.
Target n kushika pesa ila kama unaipata kwa Kaz za kikekike basi hakikisha ukikutana na wanaume unaongea mambo ya kiume