Safari za Dar - Dom za Rais Samia zimekuwa nyingi, ni hatari kwa usalama wake

Safari za Dar - Dom za Rais Samia zimekuwa nyingi, ni hatari kwa usalama wake

data

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Posts
26,858
Reaction score
23,768
Kwa vile ninampenda sana Rais wangu. Napenda niwashauri hili watu wake wa karibu.

Rais amekuwa haeleweki ni wapi hasa makazi yake. Safari za Dar - Dom zimekuwa nyingi sana. Na anapaa angani, ina month anaweza fanya kama mara nne mpaka saba. This is riskier...ni hatari kwa usalama wake.

Vyombo vinavyopaa angani hakika si salama sana, hasa ukizingatia ni Rais.

USHAURI
Mama chagua sehemu moja ya kukaa. Nafahamu unaandamwa na 'guilty conscious' kwamba unatimiza legacy...ili tu eti kuwaridhisha CCM, eti 'legacy' so unalazimika kuwa Dom mara kwa mara.

Sisi ndio wananchi chagua kukaa panapo kupendeza na tutabariki. Kama ni Dar basi baki Dar...kama ni Dom basi baki Dom, kwa usalama wako.

Midege hii si ya kuamini sana Mama yetu. For your safety.

Nimemaliza.
 
Siku hizi miji ya shughuli za kiserikali naona imekuwa miwili Dar na Dodoma, japo shughuli za chama wanafanyia Dodoma zaidi, lakini uapisho na mengine yanafanyika kote Dar na Dodoma, hapa naona anatakiwa kutuliza kichwa na wasaidizi wake ajue wapi atakuwepo muda mrefu zaidi kutekeleza mahukumu yake, aachane na "legacy" nae aanze kutengeneza ya kwake.
 
Hapa cha msingi ahamie tu Dodoma ili kumuenzi Mtangulizi wake. Ikulu ya Magogoni, kama alivyotaka Mtangulizi wake, igeuzwe kuwa Jumba la Makumbusho!

Wizara na Taasisi zote za Serikali, zihamie Dodoma. Na yeye kama anataka kwenda kusalimia nyumbani (Zanzibar), basi atafute ziara za uongo na kweli, akafurahie zake harufu ya karafuu!

Na sisi humu jukwaani kama kawaida yetu, tutabweka weee! Lakini hakuna kitakacho badilika.
 
Shukrani zimuendee CHUMA JPM kwa kufufua shirika la ndege Mungu aendelee kumpa pumziko la milele.Amina.

Naona watu wanapaa tu kuna mstaafu mmoja nimemuona leo kaelekea Zambia na ATCL.

Aibu yao walipotaka kumchafua JPM wetu na ripoti yao feki ya CAG 😎
 
Hapa cha msingi ahamie tu Dodoma ili kumuenzi Mtangulizi wake. Ikulu ya Magogoni, kama alivyotaka Mtangulizi wake, igeuzwe kuwa Jumba la Makumbusho!

Wizara na Taasisi zote za Serikali, zihamie Dodoma. Na yeye kama anataka kwenda kusalimia nyumbani (Zanzibar), basi atafute ziara za uongo na kweli, akafurahie zake harufu ya karafuu!

Na sisi humu jukwaani kama kawaida yetu, tutabweka weee! Lakini hakuna kitakacho badilika.
Magu alikuwa na Makazi matatu... Dar,Dom na Chato...

Si muda Mama ataongeza kazi la tatu..Zanzibar.

Hii ndio TZ... Lakini nawaza zaidi hizo gharama...maana ni kodi zetu watanzania masikini..

Nchi ngumu sana hii.
 
Back
Top Bottom