Safari za Kikwete hugharamiwa na nani?!

Safari za Kikwete hugharamiwa na nani?!

Hizo safari za kila uchwao za Kikwete toka alipo staafu u Rais hugharamiwa na nani?
Kikwete yupo kwenye mashirika mbalimbali ya kijamii na pia mara nyingine Serikali humtuma kuiwakilisha kwenye makongamano na dhifa mbalimbali So safari zake hugaramiwa na serikali au Tasisi anazoziwakilisha.Akisafiri for medical checkup - Serikali kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi wanamgaramia yeye na watu wake muhimu kumsindikiza akiwemo Bodguard wake
 
Muulizeni Dada yake maana wote wana mizuka ya kusafirisafiri.Lakini kama naisikia sauti ya ndani inaniambia ni Lake Oil au GSM na wakati mwingine Dada yake wa Chamwino!
 
Huyu Mheshimiwa kama angepewa nafasi ya kuchagua mahali pa kuishi kati ya Msoga Tanzania na Maryland Marekani, nadhani faster angechagua kwenda kuishi kwa Joe Biden!

Na wakati swali la aina hiyohiyo ungemuuliza Mwalimu kati ya Butiama na Maryland, basi jibu lake lingeshangaza American babies na wabeba maboksi wengi.
 
Hizo safari za kila uchwao za Kikwete toka alipo staafu u Rais hugharamiwa na nani?
Kikubwa unatakiwa kufahamu kwamba kikwete sio ngumbaru kama wewe..

Kwa taarifa yako JK ni Mwenyekiti wa Global Education Partnership,Ni board member wa Agra,Ni mjumbe wa Jopo la Amani Kusini Mwa Afrika na ndio maana huwa unaona anakuwa muangalizi wa uchaguzi mara kadhaa na bado ni mwanadiplomasia mashuhuri tuu..

Hivyo ni Kati ya nafsi chache nazozofahamu so wanaogharamia hizo safari ni hao wahusika..

Kama umepewa umepewa tuu na kama huna komaa na ulichonacho.
 
Back
Top Bottom