The Hunter
JF-Expert Member
- Dec 25, 2010
- 1,049
- 306
Yawezekana kadirio ulilolifanya ni dogo sana, maana kumbuka kuna kipindi ujumbe wake huzidi watu hamsini, wakati huohuo fahamu huwa wanajilipa per diem
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tanzania maskini ila ikulu ya tanzania ni tajiri kulinganisha na ikulu zote duniani..........
Nitaendelea kulia na Jaji Makame na Kiravu...
JK AMEKAA NJE YA NCHI ZAIDI YA MIAKA 2, SIKU 966 NA TRIPU 322.
Wakuu baada ya kufuatilia kwa karibu safari za Rais Jakaya Kikwete nje ya nchi, nikatafakari kuhusu muda anaotumia kuitumikia nchi na gharama zake anazotumia ktk safari hizo. Muda
Rais amesafiri nje ya nchi mara 322. Hilo halijadiliki Liko wazi hapa JF na magazetini. Na halijawahi kukanushwa na mtu yeyote, ikiwepo ikulu yenyewe.
Safaru nyingi za Rais anatumia kuanzia siku 4, 5 , 7 hadi siku 14 na kuendelea. Safari ya mwisho ya Davos wiki iliyopita alitumia wiki moja.
kwa kuwa safari zake nyingi ni nje ya Afrika Masharika ambayo hutumia siku moja kwa kwenda na siku moja kurudi ni sawa na kusema anatumia Jumla ni siku 2 njiani kwa tripu mmoja tu.
Kwa hiyo tukikadiria kuwa Rais ktk safari zake amefanya kazi kwa siku 2 tu. Ukijumlisha siku 2 ya kwenda na kurudi. Jumla ni siku 4 kwa wastani - kwa safari mmoja ya majuu.
GHARAMA
Kwakuwa sote tunakubaliana kuwa Rais amesafiri mara 322, tuzidishe hiyo idadi ya tripu/safari ( 322) kwa wastani wa hizo siku 4 kwa kila tripu/safari. Utapata jumla ya siku 1288. Hizi siku 1288 ukiZIgawa kwa siku 365/366 ( siku za mwaka mmoja) utapata miaka 3.5 (yaani mika 3 na miezi 6) Rais amekaa nje ya mipaka ya Tanzania.
Kwa kuwa Rais Jk aliingia madarakani mwaka 2005 na hadi sasa 2012 amekaa madarakani kwa miaka 6. Kwa hiyo, Rais amekaa nje ya nchi nusu ya muda wake wote aliokaa ktk nafasi urais( 3.5 yrs out of 6 years)
Je, Rais hajavunja rekodi ya kuingizwa ktk G. book of rekodi ya dunia? Yaani Rais aliyekaa nje ya nchi yake kwa muda mrefu kuliko marais wote wa dunia? Rais gani amemezidi Rais wetu?
NB Rais wa Marekani ambao ni wafadhili wetu hata kwenye bajeti kuu aliyesafiri sana nje ya nchi zaidi tripu 70 (kama 74?) alipigiwa kelele. Wasaidiwa - TZ wanafanya tripu 322?
Je, tumepata jibu la kwanini Rais mara nyingi husaini nyaraka feki kwa sababu ya ukosefu wa Muda wa kuzisoma?
GHARAMA
Safari ya mwisho ( safari ya 322) ya Davos iliigharimu Serikali Tsh mil 300. Nikiamu kuchukua theluthi mbili ya gharama hizo - yaani mil 200, kisha nikazidisha kwa idadi ya tripu 322. Jumla yake ni 64,400,000,000. Mabilioni haya ni mengi sana. Ukizigawa mil 50 ambazo ndio gharama ya kujenga zahanati mmoja kwa wastani, utapata jumla ya Zahanati 1288. Zahanati hizi ni sawa na idadi ya siku alizokaa nje ya nchi Rais wetu(refer red above).
Pili,Kiasi hiki hizi zingetosha kuweka Zahanati kwenye zaidi ya 50% ya kila kata nchi nzima. Nchi yetu ina kata 2000 na kidogo. Ikumbukwe kuwa Tz wanawake wajawazito kati 24 hadi 36 kwa siku wanakufa kwa sababu kadhaa ikiwepo kutokuwepo kwa zahanati au ziko mbali.
NB Hata ukisema Rais amefanya kazi nje ya nchi kwa siku moja tu( kitu ambacho binafsi siamini na inapingana na uzoefu halisi wa JK), jumlisha na siku 2 za kwenda na kurudi, unapata jumla ya siku 3 kwa tripu mmoja ya nje. Ukizidisha kwa tripu za nje 322 utapata siku 966 ambazo ukizigawa kwa siku 365/366 utapata 2. 5 (yaani miaka 2 na nusu.)
Maswali ya ziada.
Watetezi wa safari hizi za JK watueleze faida ya safari hizo ukilinganisha na gharama tulizoingia. Je, hizo neti za Gorge Bush zinaendana na Gharama tuliyoingia?
Ikiwa Rais yuko nje ya nchi kwa safari mbali mbali kwa nusu ya muda wake wa kukaa ikulu, nani anakaa ikulu na kutafakari kuhusu utatuzi wa matatizo yetu?
Je, Rais kwanini asiwatume watu wengine ( PM, Makamo, nk kufanya baadhi ya safari nje ya nchi kwa niaba yake?
Je, Rais lazima aende na delegation kubwa ambayo inaongeza gharama za safari zake?
Je, tutakwenda kwa mwendo huu mpaka 2015 kwa amani kweli?
NB; Ikumbukwe safari hizi zinahusisha kwenda kutembelea wanamuziki maarufu wa USA - Boys 2 men na kubembea majuu.
Your ideas please!
Heheehee kama safari moja tu kwaharaka inatumia 1.5bil je safari 321 itakuwaje?Tanzania maskini ila ikulu ya tanzania ni tajiri kulinganisha na ikulu zote duniani..........