Hili suala ni serious sana kwa nchi ambayo ni maskini kama Tanzania. Ili kuthibiti hali hii ya Rais kusafiri ovyo ni vizuri ikawekwa kwenye katiba mpya ili kuondokana na 'hobby' za ajabu kama hii. Ijulikane kabisa kuwa rais kwa mwaka anapaswa kusafiri mara ngapi na safari hizo ziwe ni za kikazi tu maana kuna ziara zingine za JK ambazo sio za kikazi lakini tunadanganywa kuwa ni za kikazi. Kama zote zingekuwa za kikazi basi zingekuwa na tija kwa taifa. Ikibidi naye akaguliwe uwanjani anaposafiri si ajabu safari hizo nyingi zina maslahi kwake sio bure....