JK pamoja na mapungufu yake, kila mtu alinufaika kwa namna yake.
Mikopo Elimu ya juu ilikuwa sio haba kulingana na vigezo kama priority ila alipoingia JPM alivuruga sana, hats wewe utakuwa shahidi hadi watu(wanafunzi) wakaanza kushinikiza hadi utaratibu wa zamani ukarejeshwa.
Kuhusu mishahara ingawa ilikuwa na ucheleweshwaji lakini waliipata na stahiki zao zote za madaraja na nyongeza walizipata. Hata kama Mtu alikuwa anakopa kwa Mangi ila alikuwa na uhakika wa kurejesha. Kwa JPM ikawa ni tofauti, stahiki zote zilipigwa pini.