Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

aiseeeeee huyu mshkaji nomaa aisee........
 
Sasa mlitegemea afanye nini pale Magogoni, ndio maana tunapochagua viongozi wetu tuwe tunaangalia mambo ya msingi kwa maana yanakuja kutaghalimumbele ya safari.

Ni jambo lisilo kificho kuwa wenzetu hawa wa Bagamoyo au pwani , wawe wakwere au wazaramo ni watu wanaopenda sana visherehe, ****** mnyime chochote lakini kwenda ngomani ukimkataza itakula kwako kama ni mke atakuacha hii ipo kwenye damu ,Babu wee nakwenda ngomani !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Sasa ndio hiyo inakula kwetu, asili ya mtu inaleta shida
 
atafikisha tu mana kama kutuibia kashatuibia sana tu sasa unadhani hizo pesa alizoiba atatumia kufanyia nini? we fikilia mtoto wake tu anamiliki mambo makubwa vile sasa yeye itakuwaje?
 
Rais Jakaya Kikwete, aliondoka nchini jana kwenda Maputo, Msumbiji kuhudhuria Mkutano wa Mwaka wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc) unaoanza leo.

Kwenye mkutano huo wa siku mbili, Rais Kikwete anatarajiwa kuchaguliwa rasmi kuwa Mwenyekiti wa Chombo Maalum cha Sadc cha Kusimamia Masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika).

Kwa sasa Troika inaundwa na Tanzania, Afrika Kusini na Zambia.

Miongoni mwa mambo ambayo wakuu hao wa nchi wanachama wa Sadc watajadili ni pamoja na hali ya siasa na usalama katika eneo la Sadc na hasa katika nchi za Madagascar na Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambazo zote mbili ni wanachama wa Sadc.

Sadc ina nchi wanachama 15 ambazo ni Tanzania, Angola, Botswana, DRC, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Mozambique,Namibia, Shelisheli, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.

Wakati huo huo, Rais Kikwete ametuma salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha ghafla cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Handeni, mkoani Tanga, Athuman Ramadhan Chamuya, kilichotokea usiku wa kuamkia jana.

Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, ametuma salamu hizo kwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Mussa Shekimweri, akimweleza kuwa amepokea taarifa za kifo kwa huzuni na mshtuko.

"Chamuya ametutoka katika kipindi wakati uongozi wake katika Wilaya ya Handeni ulikuwa bado unahitajika sana. Nakutumia wewe Mwenyekiti wa Mkoa salamu zangu za rambirambi. Kupitia kwako natoa mkono wa pole na rambirambi kwa familia ya ndugu Chamuya. Aidha, nawapa pole wana-Handeni wote na wana-CCM wa wilaya hiyo," alisema.

Na katika hatua nyingine, Rais Kikwete, jana alipokea hati za utambulisho za mabalozi wa India na Hispania ambao wataziwakilishi nchi zao hapa nchini.

Akizungumza na Balozi wa India, Debnath Shaw, baada ya kupokea hati yake ya utambulisho katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete, amemhakikishia balozi huyo kuwa ni dhamira ya Serikali yake kukuza zaidi uhusiano kati ya Tanzania na India.

"Tanzania na India zimekuwa na uhusiano mzuri sana na muda mrefu sana. Tumekuwa na uhusiano kati yetu na pia tumeshirikiana kwenye taasisi mbalimbali za kimataifa ikiwamo ya Kundi la Nchi 77 na kwenye Umoja wa nchi zisizofungana na upande wowote," alisema Rais Kikwete.

Aliongeza: "Siyo tu kwamba uhusiano kati yetu umekuwa mzuri sana, lakini pia Tanzania imenufaika mno kutokana na uhusiano huo. India imekuwa chimbuko kubwa ya uwekezaji katika Tanzania. India pia imekuwa ni soko kubwa la bidhaa za Tanzania. Tungependa kuona uhusiano huu unakua zaidi."
=======
Hii ni ya ngapi?

 
crashwise, ungeaandika ni safari ya ngapi. ukifuatilia inakuwa ya 334 tangu awe rais
 
Mkuu, tunaweza pata picha ya boy 2 men tena? Mi nimewahi kuiona mwaka 2006 hivi kwenye gazeti moja la udaku
jiachie na hii!
attachment.php
 
Hatopita wiki moja toka sasa utasikia anakwenda Libya kwenye kikao cha usuluhishi

hahahaha watanzania tufunguke kijua chenyewe kidogo tusipowai kuanika tutatwanga mbichi!!!!! bt..... kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho........napita 2....
 
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
na haya ndo mafanikio ya safari hizo
Juzi nasikia amepata walimu wa kimarekani 47 kwa hiyo yanwekwa kwenye mafanikio ya raisi wetu....kwa kweli anajitahidi maana wazungu 47 kufundisha shule za kata siyo mchezo kwanza tutawafundisha kiswahili maana wanafunzi wetu hawajui hata kuandika halafu wataanza nao taratibu tutafanikiwa tu...CCM hoyiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
hahahaha watanzania tufunguke kijua chenyewe kidogo tusipowai kuanika tutatwanga mbichi!!!!! bt..... kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho........napita 2....

Kuna wengine wanasema tuvumilie tu mpaka 2015...
 
Juzi nasikia amepata walimu wa kimarekani 47 kwa hiyo yanwekwa kwenye mafanikio ya raisi wetu....kwa kweli anajitahidi maana wazungu 47 kufundisha shule za kata siyo mchezo kwanza tutawafundisha kiswahili maana wanafunzi wetu hawajui hata kuandika halafu wataanza nao taratibu tutafanikiwa tu...CCM hoyiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
yaani huyu rahisi wetu anatia kichefuchefu wallah! ni virus mbaya sana aliingia kututafuna 2005! MUNGU atuongoze tuchague kwa busara 2015!
 
anga litam-miss jk, kuanzia 2016! pathetic!

Hivi hajavunja rekodi ya Vasco Dagama tu maana anajua yeye mpaka sasa ameweka recodi ya rahisi aye safi sana dunia kuliko yoyote....
 
kwenye olimpiki hamna mashindano ya safari naamini Tanzania tungeambuli medali ya dhahabu.
 
niliwahi kusoma kwenye cv yake sehemu anasema hobby zake ni kusafiri na kucheza basketball na ndio maana mkapa alimpa uwaziri wa mambo ya nje..acha aendeleze hobby yake mpaka 2015 atimue zake...nahisi itabidi ajiuguze ili kila mara awe anaenda nje kutibiwa..qaqaqaqaqaqqqqaaaaa
 
Back
Top Bottom