Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo jamaa huwa hapendi kushauriwa ndio tatizo. Ila kila lenye mwanzo lina mwisho. Akimaliza Urais sidhani kama atafikisha tena hizo safari.
Aliwahi kulalama etu watu wanalaumu anasafiri sana akahoji, watanzania wanataka tukae wote hapa bongo tule mihogo!Katika viongoz wanaokera huyu jamaa anaongoza kwa safar ambazo hazina kichwa wala miguu
Hebu fikiri ikiwa kila safari kwa uchache imetumia mil 15x313=4,695,000,000/-
Update ya leo Kenya bado weka
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIARais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaanza Ziara ya Kikazi ya Marekani na Ziara Rasmi ya Kiserikali ya Canada akianzia mjini New York, Marekani leo, Jumatatu, Oktoba Mosi, 2012.DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Kikwete na ujumbe wake uliondoka nchini usiku wa jana, Jumapili, Septemba 30, 2012, na utawasili mjini New York, Marekani mchana wa leo tayari kwa ziara hiyo ya Marekani.
Rais Kikwete atakuwa Marekani kwa siku mbili kabla ya kwenda Canada kwa ziara Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili.Katika ziara yake mjini New York, Marekani, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki Moon ofisini kwa Katibu Mkuu huyo kesho asubuhi Oktoba 2, 2012.
Baada ya mazungumzo hayo, Rais Kikwete ataungana na Mheshimiwa Ban Ki Moon, Meya wa Jiji la New York na Mfadhili Mkubwa wa Misaada ya Kibinadamu Duniani, Mheshimiwa Michael Bloomberg; Mama Helen Agerup ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Misaada ya Kibinadamu ya H&B Agerup na Dkt. Kelly J. Henning, Mkurugenzi wa Mipango ya Sekta ya Afya ya Taasisi ya Bloomberg Philanthropies kwenye Uzinduzi wa Matokeo ya Mpango ya Ubunifu wa Afya ya Akinamama katika Tanzania.
Kwenye sherehe hiyo iliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi uitwao Green Room kwenye makao makuu wa Umoja wa Mataifa, Rais Kikwete, Mheshimiwa Ban Ki Moon, Meya Bloomberg na mama Helen Agerup kwa pamoja watazindua Matokeo ya Mpango huu uitwao Innovative Maternal Health Program.
Kwenye shughuli hiyo pia Meya Bloomberg atatangaza matokeo ya miaka mitatu ya misaada ya kiafya chini ya mpango huo kwa akinamama iliyotolewa na taasisi ya inayomilikiwa na Meya Bloomberg ya Bloomberg Philanthropies. Aidha, kwenye shughuli hiyo, Meya Bloomberg atatangaza misaada mpya wa mabilioni ya fedha kuboresha afya ya akinamama katika Tanzania chini ya mpango huo na atatangaza mshirika mpya ambaye atasaidiana na taasisi ya Bloomberg Philanthropies katika kuunga mkono huduma bora za afya kwa akinamama wa Tanzania.
Katika Tanzania, misaada ya taasisi ya Bloomberg Philanthropies huelekezwa katika maeneo ya vijijini yasiyokuwa na huduma bora zaidi kwa kiafya na huduma ambazo hutolewa ni zile za kuokoa maisha ya akina mama hasa wakati wa uzazi.
Tokea mwaka 2006, taasisi hiyo imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 11.5 Fedha hizo ni sehemu ya kiasi cha dola za Marekani milioni 330 ambazo zilitolewa na taasisi hiyo kwa nchi mbali mbali duniani kwa mwaka jana peke yake.
Taasisi hiyo hufanya kazi ya kuendeleza maeneo matano duniani ambayo ni Usanii, Elimu, Mazingira, Ubunifu katika Serikali na Afya ya Umma.Rais Kikwete ataondoka Marekani kwenda Canada keshokutwa Jumatano Oktoba 3, 2012 kwa ajili ya Ziara Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili katika nchi hiyo kwa mwaliko wa Gavana Jenerali wa nchi hiyo, Mheshimiwa David Johnston.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
1 Oktoba, 2012
Uhakika ni kuwa safari anayotumia kiasi kidogo ni mil.56 (Sumaye alizitumia kutoka Dar kwenda Mombasa kupitia Tanga kwa siku mbili) na alikuwa PM kwa huyu ambaye ni President labda anatumia wastani wa mil. 80 kwa siku si kwa safari moja na kwahiyo badala ya kukokotoa safari anazosafiri tukokotoe siku anazokaa katika ziara na kila siku ni 80 mil. Kwa hesabu ya kawaida labda kila safari ni wastani wa siku 4, moja kusafiri, pili kupumzika maana ni mgonjwa tatu business na nne kurudi nyumbani maana atapumzikia Magogoni utapata hesabu hii. 313x4 x 80 = 100,160,000,000. Trilioni mia moja sawa na bajeti ya Tz ya miaka 10 kwa hiyo ndiyo maana tunabaki maskini maana bajeti yote ni katika safari za Mr. Mwigulu (nadhani naye ni akina Kiona umela wa kule kwa akina bibi Kiroboto). Maana tunapanga bajeti ya wastani wa trilioni 10 na mheshimiwa anatumia hizo hizo ni sawa na ZERO tu.
Kuna jamaa tayari ametaarifu jukwaa kwamba leo hii mkuu amegonga safari ya 337.
Kama taarifa hizi ni sahihi basi inamaana kiongozi huyu wa taifa letu masikini, lenye msingi wa kodi ya kuungaunga, atakua amebakisha safari nyingine kama 29 tu ili awe ametimiza mwaka mzima mawinguni.