Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Safari ya 337.. Anaanza ziara ya kikazi nchini Kenya.. Mungu atupe nini tena..?
 
jamani aje hatagangilonga iringa kuna jiwe kubwa kuhamasisha utalii wa nadni.jk go
 
ha ha cio mbaya watanzania tunatakiwa tujulikane kila kona ya nje ya nchi mwacheni rais wetu aweke heshma kwa kusafiri bwana
 
Huyo jamaa huwa hapendi kushauriwa ndio tatizo. Ila kila lenye mwanzo lina mwisho. Akimaliza Urais sidhani kama atafikisha tena hizo safari.

Akishamaliza muda wake, Atakuwa amemaliza kutembelea sehemu zote muhimu duniani...
 
Katika viongoz wanaokera huyu jamaa anaongoza kwa safar ambazo hazina kichwa wala miguu
 
Katika viongoz wanaokera huyu jamaa anaongoza kwa safar ambazo hazina kichwa wala miguu
Aliwahi kulalama etu watu wanalaumu anasafiri sana akahoji, watanzania wanataka tukae wote hapa bongo tule mihogo!
 
Kuna jamaa tayari ametaarifu jukwaa kwamba leo hii mkuu amegonga safari ya 337.

Kama taarifa hizi ni sahihi basi inamaana kiongozi huyu wa taifa letu masikini, lenye msingi wa kodi ya kuungaunga, atakua amebakisha safari nyingine kama 29 tu ili awe ametimiza mwaka mzima mawinguni.
 
Duh safari 337!!!I like Vasco da Gama, at least he is good at something!!
 
Hebu fikiri ikiwa kila safari kwa uchache imetumia mil 15x313=4,695,000,000/-

Uhakika ni kuwa safari anayotumia kiasi kidogo ni mil.56 (Sumaye alizitumia kutoka Dar kwenda Mombasa kupitia Tanga kwa siku mbili) na alikuwa PM kwa huyu ambaye ni President labda anatumia wastani wa mil. 80 kwa siku si kwa safari moja na kwahiyo badala ya kukokotoa safari anazosafiri tukokotoe siku anazokaa katika ziara na kila siku ni 80 mil.

Kwa hesabu ya kawaida labda kila safari ni wastani wa siku 4, moja kusafiri, pili kupumzika maana ni mgonjwa tatu business na nne kurudi nyumbani maana atapumzikia Magogoni utapata hesabu hii. 313x4 x 80 = 100,160,000,000.

Trilioni mia moja sawa na bajeti ya Tz ya miaka 10 kwa hiyo ndiyo maana tunabaki maskini maana bajeti yote ni katika safari za Mr. Mwigulu (nadhani naye ni akina Kiona umela wa kule kwa akina bibi Kiroboto). Maana tunapanga bajeti ya wastani wa trilioni 10 na mheshimiwa anatumia hizo hizo ni sawa na ZERO tu.
 
kule kwao wamezoea kucheza ngoma kila kukicha, sasa kama ngoma hakuna afanyeje, wakati miguu inamuwasha! By the way, who cares we don need him, even a monkey from the jungle can lead that country.
 
Hakika hadi amalize kipindi chake cha Uraisi atakuwa kaweka Record ya Dunia.... kusafiri siku zaidi ya 365 angani

Swali Nauliza nchi gani ambazo bado hajatembelea Tumkumbushie aende! Nahisi Nchi kama Nauru,Kiribati na Fiji bado Hajafika
 
Jason bourne naomba uiorodheshe hii Safari ya 336 ya Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaanza Ziara ya Kikazi ya Marekani na Ziara Rasmi ya Kiserikali ya Canada akianzia mjini New York, Marekani leo, Jumatatu, Oktoba Mosi, 2012.

Rais Kikwete na ujumbe wake uliondoka nchini usiku wa jana, Jumapili, Septemba 30, 2012, na utawasili mjini New York, Marekani mchana wa leo tayari kwa ziara hiyo ya Marekani.

Rais Kikwete atakuwa Marekani kwa siku mbili kabla ya kwenda Canada kwa ziara Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili.
Katika ziara yake mjini New York, Marekani, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki Moon ofisini kwa Katibu Mkuu huyo kesho asubuhi Oktoba 2, 2012.

Baada ya mazungumzo hayo, Rais Kikwete ataungana na Mheshimiwa Ban Ki Moon, Meya wa Jiji la New York na Mfadhili Mkubwa wa Misaada ya Kibinadamu Duniani, Mheshimiwa Michael Bloomberg; Mama Helen Agerup ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Misaada ya Kibinadamu ya H&B Agerup na Dkt. Kelly J. Henning, Mkurugenzi wa Mipango ya Sekta ya Afya ya Taasisi ya Bloomberg Philanthropies kwenye Uzinduzi wa Matokeo ya Mpango ya Ubunifu wa Afya ya Akinamama katika Tanzania.

Kwenye sherehe hiyo iliyopangwa kufanyika kwenye ukumbi uitwao Green Room kwenye makao makuu wa Umoja wa Mataifa, Rais Kikwete, Mheshimiwa Ban Ki Moon, Meya Bloomberg na mama Helen Agerup kwa pamoja watazindua Matokeo ya Mpango huu uitwao Innovative Maternal Health Program.

Kwenye shughuli hiyo pia Meya Bloomberg atatangaza matokeo ya miaka mitatu ya misaada ya kiafya chini ya mpango huo kwa akinamama iliyotolewa na taasisi ya inayomilikiwa na Meya Bloomberg ya Bloomberg Philanthropies.
Aidha, kwenye shughuli hiyo, Meya Bloomberg atatangaza misaada mpya wa mabilioni ya fedha kuboresha afya ya akinamama katika Tanzania chini ya mpango huo na atatangaza mshirika mpya ambaye atasaidiana na taasisi ya Bloomberg Philanthropies katika kuunga mkono huduma bora za afya kwa akinamama wa Tanzania.

Katika Tanzania, misaada ya taasisi ya Bloomberg Philanthropies huelekezwa katika maeneo ya vijijini yasiyokuwa na huduma bora zaidi kwa kiafya na huduma ambazo hutolewa ni zile za kuokoa maisha ya akina mama hasa wakati wa uzazi.

Tokea mwaka 2006, taasisi hiyo imetoa kiasi cha dola za Marekani milioni 11.5 Fedha hizo ni sehemu ya kiasi cha dola za Marekani milioni 330 ambazo zilitolewa na taasisi hiyo kwa nchi mbali mbali duniani kwa mwaka jana peke yake.

Taasisi hiyo hufanya kazi ya kuendeleza maeneo matano duniani ambayo ni Usanii, Elimu, Mazingira, Ubunifu katika Serikali na Afya ya Umma.
Rais Kikwete ataondoka Marekani kwenda Canada keshokutwa Jumatano Oktoba 3, 2012 kwa ajili ya Ziara Rasmi ya Kiserikali ya siku mbili katika nchi hiyo kwa mwaliko wa Gavana Jenerali wa nchi hiyo, Mheshimiwa David Johnston.

Imetolewa na
:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
1 Oktoba, 2012
 
Uhakika ni kuwa safari anayotumia kiasi kidogo ni mil.56 (Sumaye alizitumia kutoka Dar kwenda Mombasa kupitia Tanga kwa siku mbili) na alikuwa PM kwa huyu ambaye ni President labda anatumia wastani wa mil. 80 kwa siku si kwa safari moja na kwahiyo badala ya kukokotoa safari anazosafiri tukokotoe siku anazokaa katika ziara na kila siku ni 80 mil. Kwa hesabu ya kawaida labda kila safari ni wastani wa siku 4, moja kusafiri, pili kupumzika maana ni mgonjwa tatu business na nne kurudi nyumbani maana atapumzikia Magogoni utapata hesabu hii. 313x4 x 80 = 100,160,000,000. Trilioni mia moja sawa na bajeti ya Tz ya miaka 10 kwa hiyo ndiyo maana tunabaki maskini maana bajeti yote ni katika safari za Mr. Mwigulu (nadhani naye ni akina Kiona umela wa kule kwa akina bibi Kiroboto). Maana tunapanga bajeti ya wastani wa trilioni 10 na mheshimiwa anatumia hizo hizo ni sawa na ZERO tu.


313x4x80Ml = 100bl+
Na sio 100tilioni ka ulivyoitamka
 
Leo rais yupo Canada, akiendelea na ziara yake inayo fika siku ya 4 sasa
 
taarifa ina maelezo mengi yasiyo na maana yoyote. Tarehe ya kurudi imeonyeshwa? Hamuwezi kumshauri awe na safari za kimkakati badala ya mialiko tu, parties na birthdays?Taarifa inaweza kuboreshwa kuonyesha ni safari ya ngapi nje ya Nchi ili wananchi wasipotoshwe kwa kuona mkulu anasafiri sana?
Mwisho, malengo ya mkukuta yanamuhusu? Wingi wa safari a gharama, anatekeleza lengo lipi? Naomba taarifa iboreshwe, kujumuisha haya.
 
Kuna jamaa tayari ametaarifu jukwaa kwamba leo hii mkuu amegonga safari ya 337.

Kama taarifa hizi ni sahihi basi inamaana kiongozi huyu wa taifa letu masikini, lenye msingi wa kodi ya kuungaunga, atakua amebakisha safari nyingine kama 29 tu ili awe ametimiza mwaka mzima mawinguni.

Nafikiri hesabu yako ingekutupa mwanga kama ungehesabu idadi ya siku ambazo Mheshimiwa Rais anakuwa hayuko nchini kutokana na hizi safari 337. Mfano chukulia kila safari ni siku 5, basi ni jumla ya siku 1,685 hayuko nchini yaani miaka 4.6 au 65.9 % ya muda wake wa miaka 7 madarakani, ni makisio tu!!!!
[TABLE="width: 64"]
[TR]
[TD="width: 64, align: right"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Jamani mi naogopa kuunguzwa (ban), nimekasirika na nikiwa hivi huwa sina nidhamu so sichangii.
 
Back
Top Bottom