Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

nahisi kabla ya kumaliza hii ngwe ilyobaki huenda anataka kufika mpaka visiwa vya Tonga,Vanuatu,New papua Guinea,Somoa,Sumatra,Guyana,Fiji n.k.
Rais wetu inabidi ajifakirie mara mbili sasa kuhusu safari zake.Thats too much!

Wakati kweli anaweza kwenda huko, katika Ziwa Viktoria lenye zaidi ya visiwa 200 upande wa Tanzania amewahi kufika Ukerewe na Ukara tu. Tukimbatiza jina la Vasco da Gama mnakasirika!
 

SAFARI YA 355


Tarehe 05/09/2013

Rais Jakaya Kikwete anawasili mjini
Kampala katika mkutano wa saba wa kimataifa wa nchi za maziwa makuu, unaofanyika Kampala, Uganda

Pamoja na mkutano huo, pia anapata fursa ya kukutana na hasimu wake Rais wa Rwanda Paul Kagame na kumaliza tofauti zao kinadharia.

Mkuu hebu weka update ya ziara ya Namibia amekwenda huko Juzi
 
Huyu jamaa mm kama mm sidhani kama ana sifa za kuwa raisi maana ni muoga balaa,safari zake mm namchukulia kama vasco da gama.
 
Mheshimiwa wa magogoni alisafiri kinyemela bila kutuaga waajili wake na kwenda Juba South Sudani kwenye birthday ya taifa hilo!
Hiyo ni safari ya 313 ta awe rais wa tz mwaka 2005



UPDATES:

SAFARI YA 355


Tarehe 05/09/2013

Rais Jakaya Kikwete anawasili mjini
Kampala katika mkutano wa saba wa kimataifa wa nchi za maziwa makuu, unaofanyika Kampala, Uganda

Pamoja na mkutano huo, pia anapata fursa ya kukutana na hasimu wake Rais wa Rwanda Paul Kagame na kumaliza tofauti zao kinadharia


Mkuu Jason bourne je kuna uwezekano ukatufanyia utafiti wa gharama za safari hizi ili tumdai Jk mida ya Nov.2015

Kubwa kuliko yote nadhani mpaka tufike Oct.2015 Jk lazima atakuwa amevunja rekodi hii.


Kwa kasi hii, Kikwete atavunja rekodi ya Obasanjo!

 
Last edited by a moderator:
Halafu bwana mkubwa anasema 2015 atatunyamazisha eti kwa kitu anachosema kutuletea maendeleo,asijidanganye watanzania tumeamka we deserve more than that
 
Nadhani ni wakati muafaka sasa Safari za Raisi ziwekewe mipaka Kikatiba,maana hii imezidi uhalisia? (Safari za nje 355/10yrs =35.5 @ mwaka/12=2.9 kila mwezi acha za ndani ndiyo maana kila kitu kinakwenda ndivyo sivyo Serikalini maana gari bila dereva lazima liingie shimoni.

 
Kagonga ya 356 yuko Marekani na Canada ili kupewa PHD ya heshima!
 
Kagonga ya 356 yuko Marekani na Canada ili kupewa PHD ya heshima!

Ni 356 na 357. Long live my president maana hakuna rais mwingine kokote ameweza kuifikia rekodi yako kwa miaka nane. Usisahau kutembeza bakuri la misaada huku home bado hospitali hazina dawa wakamue hao wazungu wamezidi kutunyonya
 
Ni 356 na 357. Long live my president maana hakuna rais mwingine kokote ameweza kuifikia rekodi yako kwa miaka nane. Usisahau kutembeza bakuri la misaada huku home bado hospitali hazina dawa wakamue hao wazungu wamezidi kutunyonya
Dah, kazi tunayo weli kweli!!!!!!
 
357-400=43 hizi 43 kufikia mwakani miezi kama hii atakuwa amemaliza!
 
Hata ukila miguu ya kuku sio hivi,khaaaa!!
Kikwete amezidi jamani..
 
Ikulu ihamishiwe airport.357 yaani bado safar kama kumi kutimia siku 366 ambayo ni mwaka mzima au miezi kumi na mbili mwanaume yupo angani.
 
Tuwekewe idadi ya siku ambazo hakuwepo nchini...!
 
KITAIFA
[h=1][/h]
tanzania.jpg
Tanzania
Na George Njogopa. Mwanachi

Posted Ijumaa,Septemba20 2013 saa 9:35 AM

KWA UFUPI

  • Viza hizo za kipaumbele zinatazamiwa kutolewa katika makundi mbalimbali ikiwamo wafanyabiashara, wanafunzi na wale wanaokwenda kwa matembezi ya kawaida.




Ni kupitia utaratibu waliouanzisha utakaojulikana kama ‘viza za kipaumbele’.

Dar es salaam. Ili kuimarisha biashara, Ubalozi wa Uingereza nchini umesema, kuanzia sasa Watanzania wanaotaka huduma za viza kwa ajili ya kwenda nchini humo wanaweza kupata huduma hiyo katika kipindi cha muda mfupi kutokana na kuanzishwa kwa kile kinachoitwa ‘viza za kipaumbele’.

Huduma hiyo ambayo pia imeanza kutumika katika nchi nyingine za Uganda na Kenya inaelezwa kuwa ni moja ya mkakati wa Serikali ya Uingereza kuongeza kasi ya ushirikiano na uwekezaji nchini.

Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose alisema uhusiano wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili umeimarika zaidi katika miaka ya hivi karibuni hivyo kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya kutasaidia kuharakisha kufikia malengo ya kibiashara kwa pande zote.

“Huduma hii ya kipaumbele itahakikisha maombi ya viza yanafanyiwa kazi ndani ya siku tano na mwombaji atatakiwa kulipia kiasi cha Sh250,000,” alisema Balozi Melrose.

Hata hivyo, alifafanua kuwa, pamoja na kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya, zoezi la utoaji viza litaendelea kufanywa kwa kufuata sheria za kawaida za uhamiaji.

Viza hizo za kipaumbele zinatazamiwa kutolewa katika makundi mbalimbali ikiwamo wafanyabiashara, wanafunzi na wale wanaokwenda kwa matembezi ya kawaida.

Alisisitiza kuwa viza za kipaumbele zina lengo la kufanya mchakato wa maombi kuwa wa kasi zaidi hasa kwa wafanyabiashara pamoja na wengine ambao watahitaji kufanya maombi ndani ya muda mfupi.

“Tunafanya hivi kutokana na maombi ya wengi, pia kutokana na kukua kwa uhusiano wa kibiashara ili kuleta maendeleo na ajira kwa Watanzania na Waingereza,” alisema Balozi Melrose.

Kuhusu utoaji viza kupitia ubalozi wake Nairobi, Kenya, Balozi Melrose alisema “Tunafanya hivyo ili kuwa na ufanisi mzuri wa kazi na hakuna upendeleo wowote.”
 
Back
Top Bottom