Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

Safari za Rais Jakaya Kikwete tangu aingie madarakani 2005

..ninawashangaa sana sana wale wanaodai eti watanzania hatuitaji kujua hizi safari za rais??....why?...watanzania ambao ndio tunalipia safari hizi (kwa kodi zetu)tunahitaji sana sana kujua kila safari anayofanya rais.....haswa pale safari hizi zinapofanywa kila kukicha.....Mnafikiri mnapolalamika kuwa bajeti za serikali hazina fedha ...fedha zinaendaga wapi???safari hizi ni mojawapo ya loophole za matumizi ya hovyo ya fedha zetu.....inasikitisha wabunge wamekaa Dodoma wanalalamika bajeti zilizopitishwa hazikupewa fedha yote!!!!.......zitoke wapi fedha wakati mnamruhusu rais kusafiri atakavyo kila kukicha????.......


Mfano tu...Kwenye uzi huu kuna baadhi ya estimates za gharama za safar moja tu inayogharimu karibu mil.300.....huu si utani ni fedha ndefu sana hii ya nchi.....ukizidisha na safari za kila leo za JK unaweza usiamini ...maana inatisha....inasikitisha jambo hili wabunge wanaona sawa.....alafu wao hao wanalalamika bajeti hazipewi fedha....tuache mzaha wabongo....we can't be serious....
 
Dodoma, Tanzania

11 June 2014

Mabilioni yafyekwa safari za Kikwete

Habari kutoka ndani ya kikao cha majadiliano baina ya Serikali na Kamati ya Bunge ya Bajeti zinasema, Sh11 bilioni zimepunguzwa katika fungu hilo na kubakiza Sh39 bilioni.



Hata hivyo, kiasi kilichobakishwa ni ongezeko la asilimia 260 la Sh15 bilioni zilizopitishwa na Bunge mwaka jana kwa ajili ya safari za Rais katika mwaka wa fedha unaomalizika Juni 30 mwaka huu.



"Katika bajeti ya 2013/14 safari za Rais zilitengewa Sh15 bilioni lakini inaonekana fedha zilizotumika ni nyingi zaidi maana ndani ya miezi miwili tu zote zilikuwa zimemalizika," kilisema chanzo chetu na kuongeza:




"Kwa hiyo kwa mwaka 2014/15 Serikali ilimtengea Rais Sh50 bilioni za safari, ila tumekata Sh11bilioni ili kupelekwa katika shughuli nyingine za maendeleo. Kwa hiyo kwa mwaka ujao wa fedha, safari za Rais zitatengewa Sh39 bilioni".

jk.gif


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge alipoulizwa kuhusu hatua iliyofikiwa katika majadiliano alisema: "Subirini itakaposomwa bajeti mtajua kilichoamuliwa."

Source: Mabilioni yafyekwa safari za Kikwete - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Wakuu kwa takribani miaka mitatu na nusu rais wetu ametumia muda mwingi kusafiri nje ya nchi,safari hizo zimekomba mabilioni ya pesa za walipa kodi walala hoi,wakati wawekezaji wanafutiwa kodi. Kwa muda aliodumu madarakani amesafiri safari zaidi ya mia tatu zote nje ya nchi kiasi kwamba ahadi zote tangu 2005 asilimia kubwa hazijatekelezwa kwa maana ya kutowatendea haki wananchi waliomwamini,mfano madaktari na walimu kupelekea migomo yenye kutesa wananchi wa kawaida. Chonde! rais aachane na safari za nje kwa muda japo mchache kikatiba kukagua miradi ya maendeleo kwa wananchi tumuelewe,hizo safari za jk ni mzigo kwetu,pia wabunge tuteeni kwenye bunge la bajeti
 
Achana na rais wa sasa,fikiria kesho yako,yaani rais ajaye.
Kama tulifanya makosa,basii.Tusirudie makosa mwakani.
Hamna haja ya kulalamika mwaka wa 9/10.
 
Unakumbuka shuka kumeshakucha? Hiyo miaka mitatu tu ndo uliona? Hujui kwamba JK ameshamaliza muda wake na sasa anapalilia mahusiano mema na marafiki zake ili uzeeni, apate pa kwenda kurefresh mind badala ya kuwa bored kijijini kwake msoga?
 
unafikiri bila kwenda kuomba omba 2taishije sisi,, baba endelea kutembeza bakuri mpaka sole za viatu zitoboke
 
Walau mkuu wa nchi hajasafiri tena toka aliposafiri mara ya mwisho hapo October 2013
 
Walau mkuu wa nchi hajasafiri tena toka aliposafiri mara ya mwisho hapo October 2013
50thebe, are you kidding me? Chezea Dr. Dr. Dr. Kikwete, kwetu watu wasiotulia husemekana waliwahi kulisukuma fuvu la kichwa cha faru! Jason Bourne uko wapi? Mbona updates hazipo? Ninavyoelewa toka October 2013 kafanya safari si chini ya kumi!
 
Last edited by a moderator:
50thebe, are you kidding me? Chezea Dr. Dr. Dr. Kikwete, kwetu watu wasiotulia husemekana waliwahi kulisukuma fuvu la kichwa cha faru! Jason Bourne uko wapi? Mbona updates hazipo? Ninavyoelewa toka October 2013 kafanya safari si chini ya kumi!

Mkuu Mag3

Miaka 50 ijayo, kizazi kipya cha wakati huo kitakuwa kinajiuliza, hivi ilikuwaje Mh Raisi wa miaka ile alikuwa anaweza kusafiri mara zote zile? Alikuwa anatumwa na Watanzania? Kama walikuwa hawamtumi, kwa nini walikuwa hawamkatazi? Yaani miaka hiyo itakuwa full maswali wakijiuliza na kutushangaa.

Anyway, imeandikwa kuwa kila kizazi kinazo changamoto zake.
 
Huyo ndio jakaya kikwete a.k.a vasco dagama a.k.a ibn battuta a.k.a the explorer
 
Wakuu hakuna shaka sasa kuwa awamu hii kikwete amevunja records za kuzuru duniani tangu yesu kristo aje duniani.

Ni miaka 2013 imepita tangu yesu aje na kurudi kwa baba yake tungali tunamngoja... amin

Kuanzia mwaka wa Kwanzaa alipokuja nasi wanadamu tukaanza kuhesabu siku na miaka...ni kikwete pekee kavunja history ya dunia kwa kutembea bila kutatua matatizo ya taifa lake.

Nb; tufikiri upya wakuu ktk taifa letu hatukuibiwa kura ili kupata vasco dagama mpya.. tuchukue hatua
 
updates vip jaman au mmemvulia kofia no more updates rekodi imeshavunjwa nasubiri baada ya kumaliza muda wake 2015 aingie kwenye kitabu cha GUINNESS!
 
Dodoma, Tanzania

11 June 2014

Mabilioni yafyekwa safari za Kikwete

Habari kutoka ndani ya kikao cha majadiliano baina ya Serikali na Kamati ya Bunge ya Bajeti zinasema, Sh11 bilioni zimepunguzwa katika fungu hilo na kubakiza Sh39 bilioni.



Hata hivyo, kiasi kilichobakishwa ni ongezeko la asilimia 260 la Sh15 bilioni zilizopitishwa na Bunge mwaka jana kwa ajili ya safari za Rais katika mwaka wa fedha unaomalizika Juni 30 mwaka huu.



“Katika bajeti ya 2013/14 safari za Rais zilitengewa Sh15 bilioni lakini inaonekana fedha zilizotumika ni nyingi zaidi maana ndani ya miezi miwili tu zote zilikuwa zimemalizika,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:




“Kwa hiyo kwa mwaka 2014/15 Serikali ilimtengea Rais Sh50 bilioni za safari, ila tumekata Sh11bilioni ili kupelekwa katika shughuli nyingine za maendeleo. Kwa hiyo kwa mwaka ujao wa fedha, safari za Rais zitatengewa Sh39 bilioni”.

jk.gif


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge alipoulizwa kuhusu hatua iliyofikiwa katika majadiliano alisema: “Subirini itakaposomwa bajeti mtajua kilichoamuliwa.”

Source: Mabilioni yafyekwa safari za Kikwete - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Asante rais wetu
 
Back
Top Bottom