Safari za Rais Samia nje ya nchi

Safari za Rais Samia nje ya nchi

Mjinga mimi nina swali. Ni swali kumhusu Rais Samia [baadhi yenu ni mama yenu].

Sina takwimu wala taarifa zingine zozote za kuufuta huu ujinga wangu.

Na hata sijui niende wapi ili kuzipata takwimu na taarifa hizo.

Hivyo basi, JamiiForums ndiyo kimbilio langu nitakapo kupata baadhi ya taarifa.

Kwa namna fulani, JF imekuwa ni injini ya utafutaji wa baadhi ya taarifa.

Sasa ni hivi; huyu Rais wetu tokea achukue madaraka, ameshakaa nchini kwa hata mwezi mzima [mmoja] bila kusafiri kwenda nje ya nchi?

Nauliza hivyo kwa sababu naona kama vile kila baada ya wiki mbili hivi huwa ni lazima asafiri kwenda nje ya nchi, jambo ambalo sidhani kama lina tija sana kitaifa.

Wajuzi nijuzeni, tafadhalini sana.
Naongezea swali.
Je safari zake zimelikwsmuaje Taifa kwenye external exchange au kuuza bidhaa zetu nje?
 
Gharama kiasi gani? Je hizo gharama zina impact gani kwenye hili ongezeko la pato la Taifa?

View attachment 2912570
Mfano Toka Magu aingie Madarakani hakuna mwaka ambao pato la Taifa limeongezeka zaidi ya 5B usd, ila miaka 3 tu ya mama ongezeko la zaidi ya 7B kila mwaka, je hizo Extra income compare na Gharama za usafiri ni worth it?
Hapa ndo wachumi huwa ninashindwa kuwaelewa, hivi mnaposema uchumi wa wadanganyika umepanda kwa takwimu hizo, mnamaanisha kwa sasa ambapo hatuna maji, fedha mifukoni, umeme, vitu bei juu, dola hakuna, sukari hakuna?.

Hebu wekeni taarifa zinazoaksi uhalisia wa maisha sahihi achaneni na nadharia na propaganda za kuhadaa watu.

Wananchi wa kawaida hali ni tete kuliko mnavyojisifia nyie wenye mianya ya kuchukua chako mapema.
 
Sidhani kama Rais anajipangia safari. Ana timu ya wataalamu wabobezi; mabingwa wa nyanja zote ambao hupanga safari zake. All options, possibilities, pros and cons; advantages and disadvantages zinakuwa zimezingatiwa by the time Rais anapokuwa anaelekea airport. Take that!
Mbona magufuri walikuwa wanampangia akawa anakataa,,ndo maana aliweza kuanzisha miradi mikubwa iliyowakifu hata chadema
 
Hizo taarifa za kupangiwa ila akawa anakataa umezitoa wapi?
 
Kwanza naona umeonyesha wasiwasi wako wa kuona kama ziara za Mheshimiwa Rais pengine hazina tija nje ya nchi.ningependa kukuhakikishia na kukuambia kuwa safari za Mheshimiwa Rais zimekuwa na tija kubwa sana kiuchumi , kibiashara.kuongeza watalii, wawekezaji na kujenga mahusiano mazuri na nchi mbalimbali, hasa kwa kuzingatia sera yetu ya mambo ya nje ambayo inahusu mambo ya uchumi.

Mfano ziara ya Mheshimiwa Rais ya hivi majuzi kule nchini Indonesia imepelekea na kusaidia kupata fursa ya uwekezaji utakao leta kicheko na tabasamu kwa mamilioni ya wakulima.kwa kuwa kuna kiwanda cha mbolea kinakuja kujengwa hapa nchini. Jambo litakalofanya mbolea kupatikana hapa hapa nchini na kwa bei nafuu zaidi itakayochochea uzalishaji kwa mkulima na hivyo kuongeza kipato na kuondoa umaskini wa kaya.

Ziara ya Mheshimiwa Rais kule chini ilifungua ukurasa mpya katika mambo mbalimbali ya kiuwekezaji na kidiplomasia ,ambapo ni katika ziara hiyo tuliweza kusamehewa deni la takribani billion 31 fedha ambazo zinaweza kujenga zaidi ya km 30 za barabara au vituo vya afya takribani 61 vya millioni mia tano tano au kutoa Ruzuku katika mbolea au kununua vifaa tiba mahospitalini n.k.

Ziara ya Mheshimiwa Rais kule Marekani ilifungua pia fursa mbalimbali ambapo pia alipata kuonana na makampuni mbalimbali ya utalii akafanya nayo mazilungumzo ,jambo ambalo kwa sasa limepelekea kupata mafuriko ya watalii wanaomiminika na kupishana angani kuja Tanzania kama mwewe na sasa tunapokea watalii zaidi ya milioni moja na laki nane..lakini pia ni katika ziara hizo na kujenga mahusiano mazuri tumeweza kurudishwa katika mpango wa mapesa ya millenium challenge.

Amekuwa pia huko india ambako tumepata soko kwa ajili ya mbaazi na korosho zetu ambapo hapo awali bei ya mazao hayo ilikuwa imeporomoka kama jiwe lililodondoka toka darini.lakini pia hospitali ya Apollo itajenga hapa hospitali nyingine ambapo badala ya wagonjwa kusafirishwa kwenda india watakuwa wanapatiwa matibabu hapa hapa na hivyo kuokoa matumizi ya dollal ambayo itatumika katika manunuzi ya bidhaa zingine muhimu nje ya nchi.

Amekwenda kule Ufaransa nako tumeweza kusainiana mikataba yenye manufaa makubwa sana kiuchumi na kibiashara.

Kwa ufupi ni kuwa Rais samia Amekuwa ni Rais mwenye shabaha ambaye anafanya ziara kwa shabaha maalumu ya kupata na kulenga kitu fulani chenye manufaa kwa Taifa letu Rais Samia hasafiri tu ilimradi. Lakini pia Mheshimiwa Rais amekuwa akihudhuria vile vikao muhimu ambavyo huwakutanisha wakuu wa nchi na serikali mbalimbali hapa Duniani.mfano kama vikao vya umoja wa mataifa.vikao vilivyowakutanisha wakuu wa nchi na serikali katika kujadili matumizi ya nishati safi na salama badala ya matumizi ya kuni .vikao vilivyowakutanisha wakuu wa nchi na serikali pamoja na umoja falme za kiarabu kule Dubai n.k.

Usiangalie gharama linapokuja suala la kukutana na viongozi wenzako bali angalia tija ya vikao na ziara hizo.itakayopatiakana kwa Taifa lako. Ziara za Mh Rais zimeleta matokeo chanya sana kwa Taifa letu.imeifungua nchi yetu na sasa fursa za kiuchumi zinatiririka nchini kama maji ya mafuriko.
Bwana mdogo, nataka kubinafusisha familia yako kwa muda wa miaka kumi, baada ya muda huo, utakuwa umepata uzoefu wa kutosha wa kuingoza familia yako. Nasubilia mrejesho
 
Sidhani kama Rais anajipangia safari. Ana timu ya wataalamu wabobezi; mabingwa wa nyanja zote ambao hupanga safari zake. All options, possibilities, pros and cons; advantages and disadvantages zinakuwa zimezingatiwa by the time Rais anapokuwa anaelekea airport. Take that!
Umejibu swali au una hoja na wewe ya kwako?!.
 
Kazi ya balozi ni ipi nje ya nchi?
 
Kwenda nje siyo shida.

Shida ni pale safari zinapozidi kuwa nyingi.ku
Kumbe kwenda nje sio shida, shida yako unataka outcome ya hizo safariii, si ndioo?? Kama nimatokeo chanya ya safariii za dr. Samia kwenda njee ni nyingiii saaana. Mfano wawekezaji wko wengi wameongezeka, wataliii na sekita mbalimbali za kitalaamu zimeboreshekaaa hata kisiasaa nchi imepiga hatua saaana ikiwemo hata 4 R zote hizi na uchumi kuimalika ni miongoni mwa faida za raisi kusafiri kwenda njee, zaidi na nzuriii zaidi ni hii ya kuboresha diplomasia na mataifa mengiiii duniani
 
Sidhani kama Rais anajipangia safari. Ana timu ya wataalamu wabobezi; mabingwa wa nyanja zote ambao hupanga safari zake. All options, possibilities, pros and cons; advantages and disadvantages zinakuwa zimezingatiwa by the time Rais anapokuwa anaelekea airport. Take that!
...ambao walikuwa na hamu sana na safari hizo.Mungu awape nini sasa?Hivyo basi,wanampangia ratiba nzurinzuri zenye kufuatana ili kupata posho,kuosha macho na kufidia zile ambazo hawakuenda awamu ya tano.
 
Kazi ya balozi ni ipi nje ya nchi?
Tangia lini balozi akachukua nafsi ya Rais? Balozi atasaini na kujadili kila mkataba? Atakaa mezani na kufanya maamuzi kama ambayo yangefanywa na mkuu wa nchi? Basi kama ndio kusingekuwa na maana ya wakuu wa nchi kukutana sehemu yoyote ile maana kazi hiyo ingefanywa na mabalozi tu.
 
Mjinga mimi nina swali. Ni swali kumhusu Rais Samia [baadhi yenu ni mama yenu].

Sina takwimu wala taarifa zingine zozote za kuufuta huu ujinga wangu.

Na hata sijui niende wapi ili kuzipata takwimu na taarifa hizo.

Hivyo basi, JamiiForums ndiyo kimbilio langu nitakapo kupata baadhi ya taarifa.

Kwa namna fulani, JF imekuwa ni injini ya utafutaji wa baadhi ya taarifa.

Sasa ni hivi; huyu Rais wetu tokea achukue madaraka, ameshakaa nchini kwa hata mwezi mzima [mmoja] bila kusafiri kwenda nje ya nchi?

Nauliza hivyo kwa sababu naona kama vile kila baada ya wiki mbili hivi huwa ni lazima asafiri kwenda nje ya nchi, jambo ambalo sidhani kama lina tija sana kitaifa.

Wajuzi nijuzeni, tafadhalini sana.
Jimama tapeli
 
Kumbe kwenda nje sio shida, shida yako unataka outcome ya hizo safariii, si ndioo?? Kama nimatokeo chanya ya safariii za dr. Samia kwenda njee ni nyingiii saaana. Mfano wawekezaji wko wengi wameongezeka, wataliii na sekita mbalimbali za kitalaamu zimeboreshekaaa hata kisiasaa nchi imepiga hatua saaana ikiwemo hata 4 R zote hizi na uchumi kuimalika ni miongoni mwa faida za raisi kusafiri kwenda njee, zaidi na nzuriii zaidi ni hii ya kuboresha diplomasia na mataifa mengiiii duniani
Hujaelewa nilichokiandika, au?
 
Kwanza naona umeonyesha wasiwasi wako wa kuona kama ziara za Mheshimiwa Rais pengine hazina tija nje ya nchi.ningependa kukuhakikishia na kukuambia kuwa safari za Mheshimiwa Rais zimekuwa na tija kubwa sana kiuchumi , kibiashara.kuongeza watalii, wawekezaji na kujenga mahusiano mazuri na nchi mbalimbali, hasa kwa kuzingatia sera yetu ya mambo ya nje ambayo inahusu mambo ya uchumi.

Mfano ziara ya Mheshimiwa Rais ya hivi majuzi kule nchini Indonesia imepelekea na kusaidia kupata fursa ya uwekezaji utakao leta kicheko na tabasamu kwa mamilioni ya wakulima.kwa kuwa kuna kiwanda cha mbolea kinakuja kujengwa hapa nchini. Jambo litakalofanya mbolea kupatikana hapa hapa nchini na kwa bei nafuu zaidi itakayochochea uzalishaji kwa mkulima na hivyo kuongeza kipato na kuondoa umaskini wa kaya.

Ziara ya Mheshimiwa Rais kule china ilifungua ukurasa mpya katika mambo mbalimbali ya kiuwekezaji na kidiplomasia ,ambapo ni katika ziara hiyo tuliweza kusamehewa deni la takribani billion 31 fedha ambazo zinaweza kujenga zaidi ya km 30 za barabara au vituo vya afya takribani 61 vya millioni mia tano tano au kutoa Ruzuku katika mbolea au kununua vifaa tiba mahospitalini n.k.

Ziara ya Mheshimiwa Rais kule Marekani ilifungua pia fursa mbalimbali ambapo pia alipata kuonana na makampuni mbalimbali ya utalii akafanya nayo mazungumzo ,jambo ambalo kwa sasa limepelekea kupata mafuriko ya watalii wanaomiminika na kupishana angani kuja Tanzania kama mwewe na sasa tunapokea watalii zaidi ya milioni moja na laki nane..lakini pia ni katika ziara hizo na kujenga mahusiano mazuri tumeweza kurudishwa katika mpango wa mapesa ya millenium challenge.

Amekwendaa pia huko india ambako tumepata soko kwa ajili ya mbaazi na korosho zetu ambapo hapo awali bei ya mazao hayo ilikuwa imeporomoka kama jiwe lililodondoka toka darini.lakini pia hospitali ya Apollo itajenga hapa hospitali nyingine ambapo badala ya wagonjwa kusafirishwa kwenda india watakuwa wanapatiwa matibabu hapa hapa na hivyo kuokoa matumizi ya dollar ambayo itatumika katika manunuzi ya bidhaa zingine muhimu nje ya nchi.

Amekwenda kule Ufaransa nako tumeweza kusainiana mikataba yenye manufaa makubwa sana kiuchumi na kibiashara.

Kwa ufupi ni kuwa Rais samia Amekuwa ni Rais mwenye shabaha ambaye anafanya ziara kwa shabaha maalumu ya kupata na kulenga kitu fulani chenye manufaa kwa Taifa letu Rais Samia hasafiri tu ilimradi. Lakini pia Mheshimiwa Rais amekuwa akihudhuria vile vikao muhimu ambavyo huwakutanisha wakuu wa nchi na serikali mbalimbali hapa Duniani.mfano kama vikao vya umoja wa mataifa.vikao vilivyowakutanisha wakuu wa nchi na serikali katika kujadili matumizi ya nishati safi na salama badala ya matumizi ya kuni .vikao vilivyowakutanisha wakuu wa nchi na serikali pamoja na umoja wa falme za kiarabu kule Dubai n.k.

Usiangalie gharama linapokuja suala la kukutana na viongozi wenzako bali angalia tija ya vikao na ziara hizo itakayopatikana kwa Taifa lako. Ziara za Mh Rais zimeleta matokeo chanya sana kwa Taifa letu.imeifungua nchi yetu na sasa fursa za kiuchumi zinatiririka nchini kama maji ya mafuriko.

Tanzania siyo kisiwa na kama Taifa hatuwezi kujifungia ndani wenyewe na mambo yetu wenyewe utafikiri watu wenye ukoma au wagonjwa wa corona au kipindupindu .ni lazima mkuu wetu wa nchi afanye ziara za kuonana na wenzake katika kujadili masuala mbalimbali yatakayoleta na kuchochea fursa za biashara.hatuwezi tukasema tutalima sana kila aina ya zao wakati hujaweka mikakati ya wapi utauza bidhaa zako pamoja na wapi utapata mbolea au fedha za kuwekeza katika ujenzi wa viwanda au kuvutia watu wakija kujenga viwanda vya bidhaa fulani lakini ukitoka nje ya nchi au kualika wenzako basi utapata fursa mbalimbali zenye matokeo chanya kwa Taifa lako.

Tupo katika Dunia ya ushindani,Dunia ambayo kila mtu anatafuta fursa kwa ajili ya Taifa lake.ndio maana hakuna anayetulia na kujifungia ndani tu kama kipofu wakati wenzako wanakulika fursa hadi kwa tochi.
Huo ni uzululaji tu, katika Dunia ya kisasa siyo lazima utembee, kuna namna nyingi za kufanya mawasiliano, na isitoshe hizo nchi zina balozi wetu
Huyu ni mzululaji kama kakake
 
Back
Top Bottom