Kwanza naona umeonyesha wasiwasi wako wa kuona kama ziara za Mheshimiwa Rais pengine hazina tija nje ya nchi.ningependa kukuhakikishia na kukuambia kuwa safari za Mheshimiwa Rais zimekuwa na tija kubwa sana kiuchumi , kibiashara.kuongeza watalii, wawekezaji na kujenga mahusiano mazuri na nchi mbalimbali, hasa kwa kuzingatia sera yetu ya mambo ya nje ambayo inahusu mambo ya uchumi.
Mfano ziara ya Mheshimiwa Rais ya hivi majuzi kule nchini Indonesia imepelekea na kusaidia kupata fursa ya uwekezaji utakao leta kicheko na tabasamu kwa mamilioni ya wakulima.kwa kuwa kuna kiwanda cha mbolea kinakuja kujengwa hapa nchini. Jambo litakalofanya mbolea kupatikana hapa hapa nchini na kwa bei nafuu zaidi itakayochochea uzalishaji kwa mkulima na hivyo kuongeza kipato na kuondoa umaskini wa kaya.
Ziara ya Mheshimiwa Rais kule china ilifungua ukurasa mpya katika mambo mbalimbali ya kiuwekezaji na kidiplomasia ,ambapo ni katika ziara hiyo tuliweza kusamehewa deni la takribani billion 31 fedha ambazo zinaweza kujenga zaidi ya km 30 za barabara au vituo vya afya takribani 61 vya millioni mia tano tano au kutoa Ruzuku katika mbolea au kununua vifaa tiba mahospitalini n.k.
Ziara ya Mheshimiwa Rais kule Marekani ilifungua pia fursa mbalimbali ambapo pia alipata kuonana na makampuni mbalimbali ya utalii akafanya nayo mazungumzo ,jambo ambalo kwa sasa limepelekea kupata mafuriko ya watalii wanaomiminika na kupishana angani kuja Tanzania kama mwewe na sasa tunapokea watalii zaidi ya milioni moja na laki nane..lakini pia ni katika ziara hizo na kujenga mahusiano mazuri tumeweza kurudishwa katika mpango wa mapesa ya millenium challenge.
Amekwendaa pia huko india ambako tumepata soko kwa ajili ya mbaazi na korosho zetu ambapo hapo awali bei ya mazao hayo ilikuwa imeporomoka kama jiwe lililodondoka toka darini.lakini pia hospitali ya Apollo itajenga hapa hospitali nyingine ambapo badala ya wagonjwa kusafirishwa kwenda india watakuwa wanapatiwa matibabu hapa hapa na hivyo kuokoa matumizi ya dollar ambayo itatumika katika manunuzi ya bidhaa zingine muhimu nje ya nchi.
Amekwenda kule Ufaransa nako tumeweza kusainiana mikataba yenye manufaa makubwa sana kiuchumi na kibiashara.
Kwa ufupi ni kuwa Rais samia Amekuwa ni Rais mwenye shabaha ambaye anafanya ziara kwa shabaha maalumu ya kupata na kulenga kitu fulani chenye manufaa kwa Taifa letu Rais Samia hasafiri tu ilimradi. Lakini pia Mheshimiwa Rais amekuwa akihudhuria vile vikao muhimu ambavyo huwakutanisha wakuu wa nchi na serikali mbalimbali hapa Duniani.mfano kama vikao vya umoja wa mataifa.vikao vilivyowakutanisha wakuu wa nchi na serikali katika kujadili matumizi ya nishati safi na salama badala ya matumizi ya kuni .vikao vilivyowakutanisha wakuu wa nchi na serikali pamoja na umoja wa falme za kiarabu kule Dubai n.k.
Usiangalie gharama linapokuja suala la kukutana na viongozi wenzako bali angalia tija ya vikao na ziara hizo itakayopatikana kwa Taifa lako. Ziara za Mh Rais zimeleta matokeo chanya sana kwa Taifa letu.imeifungua nchi yetu na sasa fursa za kiuchumi zinatiririka nchini kama maji ya mafuriko.
Tanzania siyo kisiwa na kama Taifa hatuwezi kujifungia ndani wenyewe na mambo yetu wenyewe utafikiri watu wenye ukoma au wagonjwa wa corona au kipindupindu .ni lazima mkuu wetu wa nchi afanye ziara za kuonana na wenzake katika kujadili masuala mbalimbali yatakayoleta na kuchochea fursa za biashara.hatuwezi tukasema tutalima sana kila aina ya zao wakati hujaweka mikakati ya wapi utauza bidhaa zako pamoja na wapi utapata mbolea au fedha za kuwekeza katika ujenzi wa viwanda au kuvutia watu wakija kujenga viwanda vya bidhaa fulani lakini ukitoka nje ya nchi au kualika wenzako basi utapata fursa mbalimbali zenye matokeo chanya kwa Taifa lako.
Tupo katika Dunia ya ushindani,Dunia ambayo kila mtu anatafuta fursa kwa ajili ya Taifa lake.ndio maana hakuna anayetulia na kujifungia ndani tu kama kipofu wakati wenzako wanakulika fursa hadi kwa tochi.