Safi Sana: Marekani na ujanja wake kaingizwa mkenge na Venezuela kuhusu kuuziwa mafuta

Sema hizi habari huwezi kuzkuta BBC news[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
BBC, CNN na ALJAZEERA ni majanga tu kuhusu Africa kama njaa, magonjwa COVID-19, vimbunga, vita, tetemeko la ardhi, mafuriko, mateka ya Boko Haram, mtifuano wa wanasiasa na ukame jangwani....[emoji849]

Kwao USA, UK, SAUD ARABIA, na kwengineko duniani ni fulu bata kama wako mbinguni na wala hawana shida zozote....[emoji16]
 
Tunavyoongea utafikiri USA ni ka center flani hivi ambayo wanaishi watu wasiodizi 30 wenye njaa sana, jamiiforum Kuna watu kwelikweli.
Halafu tunaoongea sasa na kuanza kumwambia US atakoma tupo madongo kuinama huku Ulimwengu wa tatu kwenye dhiki tele hata kodi ya chumba kimoja kulipa ni shida.Nasoma comment za huu uzi huku nacheka sana 😀😀
 
Saudi Arabia hana uwezo wa kumdindia USA, US atafungulia Houthi rebels ndani ya siku 2 Saudi inakuwa Libya
US hawezi kugusa Saudi Arabia maana pale Kuna miji mitakatifu, Islam wako siriazi na dini yao sio Kama sisi wakristo Mara Mwamposa na Nabii Shila,

Irani na Saudi kutokuelewana ni sawa na mgogoro wa familia tu.
 
Habari yako haiko sawa na imekaa kichuki sana...
Sasa ni hivi...Marekani ina hifadhi kubwa ya mafuta kuliko nchi yoyote duniani
 
Aisee.. Noma sanaa

Niliiona hiyo ya Saudia kuwachunia ku pickup simu zao ila kuhusu venezuela sikujua kabisa..

No way itabidi akubali masharti ya venezuela tuu...
kwan hana namba yake ya watsap akmchek king mojakwa mojaaa si rahis fasta
 
Bado nasisitiza tu kwamba vijana wa kitanzania bado ni shida sana kwani hawapendi kusoma na kutafuta taarifa ila wao ni kukariri tu na ushabiki kama wa Simba na Yanga.

Marekani ni taifa lenye watu "Think Tanks" na ni taifa ambalo vitabu walivyoandikia mipango yao ya maendeleo kwa miaka 200 ijayo vinaweza vikajaza semi trela hata kumi hivyo kutegemea kwamba mambo yake yanaweza yakakwamishwa na tu-nchi kama Venezuela au sijui Saudi Arabia ni kufikiria kitoto sana.

Sasa hivi wameshaanza mpango wa kutoa mapipa milioni mbili za mafuta ghafi kila siku kutoka kwenye akiba yao ya Strategic Oil Reserve ilioko Alaska na kufanya bei ya mafuta ghafi ipungue kwenye soko la dunia kutoka USD 124/bbd mpaka USD 106/bbd (High) na USD 98.6/bbd (Low) bei ya leo na bado itaendelea kushuka unafuu ambao hata sisi tutanufaika nao.

Wenzetu walishajipanga siku nyingi na kujiwekea Contingency Plans kwa kufahamu kwamba kuna kipindi lazima watakutana na taharuki fulani fulani.

Itakumbukwa kwamba Marekani ndio taifa la pili duniani, nyuma ya Russia, kwa kuwa na akiba kubwa ya mafuta ghafi kwa hiyo wanaofikiria kwamba wanaweza wakakwama kwa kukosa hiyo rasilimali watakuwa wanakosea sana.
 
Ongezea sukari kidogo kwenye kahawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…