- Thread starter
- #101
ngoja nikusaidieKutoka mjini kati kwenda morombo km ngapi?
safari ya dakika 20 tu kutoka mjini kati ushaacha lami
kwanza muundo wa Arusha dodoma au nairobi ni tofauti na mwanza
Arusha kuna barabara zaidi ya 6 za kutoka mjini wakati mwanza ni mbili tu kwa maana ya usagara na ile ya kisesa
hujasemea barabara ya Arusha hadi kia km 50 ni lami
kuna Nairobi road ni lami hadi namanga
kuna dodoma road ni lami hadi babati
kuna bypass km 42 zote ni lami kuna barabara ya chekereni hadi usa km 25 zote ni lami
sasa tukija kwa hapo Morombo unapopasemea ile barabara ipo chini ya tanroads ambayo inaenda simanjiro hadi dodoma na jiji halina mamlaka ya kuitengeneza
lakini bado hiyo barabara ya vumbi inaenda km 1.3 tu kabla hujafika barabara ya east africa ambayo nayo ni lami
haya kutoka hapo hapo Morombo kuna barabara ya kwenda dampo nayo ni lami kutoka dampo tena wamejenga kuonganisha na barabara ya east africa nayo tena ni lami