Eyce
JF-Expert Member
- Mar 16, 2016
- 7,185
- 24,330
Pengine ulipokulia hapaendani na tabia na ndoto zako .... sometimes tunajikuta tunalelewa katika mazingira ambayo si rafiki na tabia zetu hivyo tunajikuta tumejifunga na kujiona kuwa tupo tofauti na wengineo ama tumekosewa ama sisi tuna matatizo ;dah mkuu hapo umenigusa kweli kuhusu kuwa na mtu nampa siri zangu kwa kwelii sina kama rafiki nazungumza nae kawaida
na sina mtu wa kumuambia yale ya siri kwa sababu hawa rafiki nilionao unaweza kinmuambia jambo lako kisha baadae akikaa na washkaji wengine kunogesha story naye anasimulia yale ulomuambia
sasa imenifanya nitizame kwanza yupi wa kumfanya msiri jambo ambalo naona bora ishu nikae nazo mwenyewe kuliko kumuambia mtu ambae naye anazisambaza kwa wengine naona ananipa stress zaidi..
au unanipa wazo gani kuhusu hili mkuu Tobaa
ukweli ni kuwa hata muerevu akikaa katika kundi la wasiojielewa huishia kuonekana mwendawazimu hivyo sometimes sio kosa letu
Pili yawezekana unakuwa na marafiki ambao hamuendani na hamfai kuchangamana ...mfano cocoa na maziwa vina asili na ladha tofauti ila vikichanganywa huleta ladha bora zaidi lakini mafuta na maji kamwe havichangamani ...
Namaanisha mnaweza kuwa marafiki wenye tabia mbili tofauti na mkarandana kama mcheshi na mtaratibu lakini kuna tabia ambazo huwa haziendani na hazichangamani...pengine upo katika kundi mojawapo
Alafu usijipe limits maana huwezi kaa ndani ukategemea kupata rafiki sahihi ingawa inawezekana maana nimepata rafiki jf kimasikhara tu na tunaongea deep issues ambazo hata siwezi kumuambia mtu mwingine na hapo bado hatujakutana lakini kutokana na chats tukajua kuwa tunarandana kwa vitu vingi ...
Kingine mtu perfect hayupo duniani lakini usije kujidanganya kufuga kunguru ili ageuke njiwa kisa njiwa hawapatikani ..huo ni wendawazimu ..Kheri uwe peke yako na ukaitunza furaha yako kuliko kuwa na watu wanaokufanya ujihisi mpweke zaidi ..usiwe desperate ..take your time