Sakata la Bandari: Hayati Magufuli apewe maua yake

Sakata la Bandari: Hayati Magufuli apewe maua yake

Ingia darasani Cheti Feki kitaendelea kukutesa sana!
Kila mtu anakijisababu chake tu cha kumchukia mwamba.

Huyu lazima kuna sehemu jamaa alimgusa akambana.

Ila sisi tuonayo mazuri yake na utendaji wake.. Na hakuwahi kutugusa kwenye negative way, akatugusa in postive way.. Kwanini tusimpe sifa zake.

Apumzike kwa amani Mjomba Magufuli.
 
Huyo shetani akae huko huko shimoni. Anayemkumbuka ni shetani kama yeye tu.
 
Maoni na Ushauri wa Wataalam wa Bunge ulikuwa ni huu - Je ulizingatiwa? Ndio ni kweli Bandari yetu ina shida kubwa hasa ya uzembe, kuendeshwa kwa hasara na upigaji - Je swala la kubinafsisha ni lini ilifanyika Mjadala wa Kitaifa watu watoe maoni- Uwekezaji ni mzuri ila ni hatari sana usipopelekwa kwa umakini na uzalendo. Kwanini miaka 100
Wataalam a wa bunge wanasemaje? Kutokana na uchambuzi tuliofanya hapo juu, ni maoni na ushauri wetu kuwa, Bunge lipate ufafanuzi kutoka Serikalini katika maeneo machache yafuatayo:-

19 a. Ibara ya 25 (1) inaeleza kuwa kuna shughuli za awali za mradi (Early Project Activities) zitaanza kufanyika mapema baada ya kusainiwa Mkataba. Shughuli za awali za mradi zitafanyika kabla ya Bunge kuridhia Mkataba na kabla ya Mkataba kuanza kutumika rasmi kwa mabadilishano ya Hati za Uridhiaji kati ya Serikali zote mbili.
Shughuli za awali za mradi zimetafsiriwa katika Ibara ya 1 kuwa ni kufanya upembuzi yakinifu pamoja na kufanya tathmini ya kimazingira na kijamii ya mradi huu (environmental and social due diligence), kujenga barabara za muda kuwezesha kufika eneo la mradi, n.k.
Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi katika eneo hili, ambapo shughuli za Mradi zinaanza kabla ya Mkataba kuridhiwa na Bunge.

b. Ibara ya 20 kuhusu usuluhishi wa migogoro kufanyika Afrika Kusini na kwa kutumia Sheria za Usuluhishi za Kamisheni ya Umoja wa Mataifa juu ya Sheria zinazohusika na Biashara za Kimataifa (UNICITRAL Arbitration Rules), ni kinyume na maelekezo ya kifungu cha 11 cha Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili ya Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources [Permanent Sovereignty] Act, 2017).
Sheria tajwa inaelekeza kuwa mgogoro wowote unaotokana na matumizi ya rasilimali na maliasili za nchi hautatatuliwa katika mahakama na mabaraza ya nchi za nje, bali utatatuliwa na vyombo vya sheria vya Tanzania na kwa kutumia sheria za Tanzania.
c. Ibara ya 23 (4) kuhusu kusitisha Mkataba, inaeleza bayana kuwa Serikali husika katika Mkataba hazitakuwa na haki ya kuvunja Mkataba (denounce), kujitoa (withdraw from), kuahirisha (suspend) au kusitisha (terminate) Mkataba katika mazingira yoyote, ikiwa ni pamoja na mazingira ya uvunjaji mkubwa wa masharti ya Mkataba huu (material breach), mabadiliko ya msingi katika mazingira ya utekelezaji Mkataba (fundamental change of circumstances), mgogoro mkubwa wa kidiplomasia (severance of diplomatic or consular relations), au sabau zozote zile zinazotambulika katika sheria za kimataifa.
Masharti ya Ibara hii yanatakiwa kufafanuliwa na Serikali.

d. Muda wa utekelezaji Mkataba huu haujawekwa bayana, bali Ibara ya 23 1) inasema kuwa ukomo wa Mkataba huu ni mpaka hapo shughuli za mradi huu zitakapokuwa zimekamilika. Serikali iombwe kutoa ufafanuzi kuhusu jambo hili la ukomo wa Mkataba.

e. Ibara ya 27 inaweka masharti kwamba, pale ambapo Mkataba huu utaanza kutumika rasmi, Serikali yeyote katika Mkataba huu haitaingia au kuwa sehemu ya makubaliano ya ndani ya nchi au ya kimataifa wakati wa utekelezaji wa Mkataba.
Serikali iombwe kutoa ufafanuzi wa Ibara hii. Mkataba huu haujaweka muda wa ukomo, hivyo Serikali haitakuwa na nafasi ya kuingia makubaliano mengine kuhusu kuendeleza au kuboresha na kuendesha bandari zake.
f. Ibara ya 30 inaweka masharti ya kuwa na uthabiti, uimara na uhakika wa kutoyumbisha Mkataba huu (Stabilization). Eneo hili lipate ufafanuzi wa Serikali. Kwa kuzingatia kuwa Mkataba huu hauna muda wa ukomo. Hivyo, kuna mazingira sheria zitahitaji kufanyiwa mabadiliko kulingana na wakati, ambapo mabadiliko hayo yanaweza kuathiri masharti ya Mkataba huu na kuchukuliwa kuwa ni kuyumbisha Mkataba huu.

g. Kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mamlaka ya kusaini mMkataba huu yametolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hata hivyo, kwa upande wa Serikali ya Dubai haijawekwa wazi. Tunashauri Serikali itoe ufafanuzi kuhusu mamlaka ya kusaini Mkataba huu kwa upande wa Serikali ya Dubai
Imeandaliwa na Sekretariati ya Bunge

Sent using Jamii Forums mobile app
huu mkataba ni. HATARI kwa nchi, huu mkataba umekaa kimabavu Sana !! ukiusoma vizuri na kwa utulivu!!!. Yaani ukitia saini tu Basi huruhusiwi kujikuna kwa lolote hata Kama unakanyagwa, na ukitaka kujikuna unatakiwa kupanda dreamlimer au Ethiopia airline mpaka Africa kusini ukatoe malalamiko huko, na Hata Kama hujapata haki huruhusiwi kuvunja mkataba . DAAAH NI KICHAA TU NDO ANAWEZA KUUELEWA HUU MKATABA.
 
HUU NDIO UKWELI JUU YA MKATABA WA .

[emoji736]Mkataba huu kati ya DP World na TPA kwa niaba ya Serikali ya JMT chini ya Rais Samia Suluhu una faida gani kwetu, kwanini mkataba huu ni muhimu sana wakati huu kuliko wakati wowote ule?

[emoji736]Kwanza, achana kabisa na propaganda za UFIPA juu ya kwamba tumetoa bandari yetu 100% iendeshwe na DP World, huu ni uwongo na wala huitaji degree wala elimu ya darasa la 7 kujua kuwa huu ni uwongo.

[emoji736]Hadi muda huu tunachojua ni kwamba, makubaliano ya awali yamesainiwa Dubai wakati Rais Samia Suluhu alipokwenda kwenye maonesho ya Dubai Expo 2020, na kama makubaliano ya mwisho yatasainiwa, basi mkataba huu utakuwa na thamani ya USD 500 milioni.

Nini Mtanzania unapaswa kujua kuhusu mkataba huu?

Kwanza, unatakiwa kujua kwamba DP World itapewa
kushughulikia gati ya 5 hadi 7.

DP World mbinu yake ni kuondoa vizuizi vya biashara na kuunda mfumo ikolojia wa biashara ili kupanua mtiririko wa biashara ya kikanda na kimataifa.

[emoji3504]Kama mkataba huu utasainiwa, ndani ya miaka 10 ijayo, ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam utaongezeka kwa asilimia 233.7%

[emoji3504]Mapato ya Bandari ya Dar es Salaam kuongezeka kutoka Trilioni 7.79 kwa mwaka hadi Trilioni 26, ndani ya miaka 10 ijayo.

[emoji3504]Ufanisi wa Bandari utaongezeka, mizogo itatoa haraka, ajira zitazalishwa kwa wingi na pia pato la taifa kuimarika maradufu.

[emoji3504]Mapato yakiongezeka kwenye kupitia Bandari ya Dar, serikali itapunguza mzigo wa kodi kwa Watanzania hivyo kuboresha hali ya maisha ya watu.

[emoji3504]DP World hawatowekeza bandari ya Dat tu, bali na bandari nyingine nchini na pia, wataalamu wetu watakwenda kupewa mafunzo na kuongezewa ubunifu kwenye utendaji wao.
Eti mapato yakiongezeka serikali itapunguza mzigo wa kodi kwa watanzania, bladifakeni.
 
Mbona hukumshauri shujaa wa Africa abinafsishe Bandari?
Mchakato wa ubinafsishaji ulishafanywa na Dr Mwakyembe wa Kyela enzi za awamu ya 4 kilichobaki ilikuwa ni ujasiri wa utekelezaji na vipaumbele vya Marais na Mabunge yajayo

Ni kama Serikali kuhamia Dodoma au Bwawa la Nyerere yaani Vipaumbele!

Baraza la Mawaziri la awamu ya 4 hata hapo Mwanjelwa mnawajua Wajumbe wake wa Kudumu 😂!
 
Mchakato wa ubinafsishaji ulishafanywa na Dr Mwakyembe wa Kyela enzi za awamu ya 4 kilichobaki ilikuwa ni ujasiri wa utekelezaji na vipaumbele vya Marais na Mabunge yajayo

Ni kama Serikali kuhamia Dodoma au Bwawa la Nyerere yaani Vipaumbele!

Baraza la Mawaziri la awamu ya 4 hata hapo Mwanjelwa mnawajua Wajumbe wake wa Kudumu 😂!
Kwa nini shujaa wako uchwara hakutekeleza?
 
Magufuli ameanza kukumbukwa kwasababu alikuwa na akili zaidi ya huyu tuliyenaye, ni hivyo tu.
 
Haya umeeleza vizuri Sana , swali langu Hayo mazuri yooote , na hivyo sijui vikwazo kwanini tusifanye wenyewe !!?? Yaani eti tunapambania tufanyiwe ni ujinga huu , li nchi likubwa hili tunashindwaje kufanya!?? Halafu hakuna mwekezaji ambaye haji tu bule kuwafanyia Kama haioni faida pale .ukweli ni kwamba jamaa akijenga pesa zote atakuwa akisomba , na ss tutambulia visent , na Hadi mkataba unaisha ataondoka na kutuachia mitambo ambayo tayari itakuwa vyuma chakavu , na pot iliyochoka tayari inayohitaji marekebisho Tena , visent ambavyo tutakuwa tunaonjesha kwa kipindi choote Cha mkataba vitaenda Tena kwenye ukarabati na kutengeneza vyuma chakavu tutakavyoachiwa !!!
Serikali haziwezi kufanya biashara. Hata ATCL nayo ikodishwe tu
 
muuwaji, mporaji, mnyang'anyi, asiyepingwa, asiyetaka upinzani, muonevu we nenda tu bora umaskini wenye amani
 
Serikali haziwezi kufanya biashara. Hata ATCL nayo ikodishwe tu
Kagame aliomba apewe Bandari ya Dar aisimamie enzi za KIKWETE na alionekana anatudharau, tukasema tunaweza kuendesha wenyewe.

Leo iweje bandari hiyo hiyo apewe mwarabu Kwa mkataba wa kijuha?

Tukirudi kati Kwa Maslahi ya Taifa sioni kama Kuna tatizo.

Turudi tu kati Dodoma, tuhakikishe Maslahi ya Taifa yanaazingatiwa na mkataba unarudishwa Kwa aliyeuleta utupwe Kapuni.
 
Asingeuliwa yote yangekamilika

Hata huo Uwanja wa Wanyakyusa hapo Sokoine ungebomolewa na kujenga wa Kisasa!

Ndio sababu Mbeya mjini aliiweka mikononi kwa Mbunge mzawa Dr Mwansasu 😀😀
Nani alimuua shujaa? Si alikuwa anakindwa na Mitambo kutoka Israel na walenga shabaha ambao wewe ulikuwa Kiongozi wao bila kusahau waganga,vipi ulishindwaje kazi Yako au wew ndio ulimuia? 🤣🤣
 
Ilani ya Uchaguzi anayoitumia sa100 ni ilani ya Uchaguzi ya 2020.

Ilani hiyo Alipewa Magu na sa100 Kwa uchaguzi wa 2020.

Ilani hiyo haikuelekeza kuuza bandari Bali kuiboresha kuleta ufanisi.

Serikali ya sa100 inafanya usaliti Kwa Watanzania na Haina mamlaka kufanya hivyo.

Hili halikubaliki!!!!!
 
Nani alimuua shujaa? Si alikuwa anakindwa na Mitambo kutoka Israel na walenga shabaha ambao wewe ulikuwa Kiongozi wao bila kusahau waganga,vipi ulishindwaje kazi Yako au wew ndio ulimuia? 🤣🤣
Ungekuwepi enzi za Sokoine na akina Dube usingeuliza hili swali Bwashee 😂

Hakuna mtu alikuwa na kikosi cha Waganga kama Kolimba wa Ludewa

Sema tu kazi ya Mungu haina makosa!
 
Back
Top Bottom