HUU NDIO UKWELI JUU YA MKATABA WA .
✅Mkataba huu kati ya DP World na TPA kwa niaba ya Serikali ya JMT chini ya Rais Samia Suluhu una faida gani kwetu, kwanini mkataba huu ni muhimu sana wakati huu kuliko wakati wowote ule?
✅Kwanza, achana kabisa na propaganda za UFIPA juu ya kwamba tumetoa bandari yetu 100% iendeshwe na DP World, huu ni uwongo na wala huitaji degree wala elimu ya darasa la 7 kujua kuwa huu ni uwongo.
✅Hadi muda huu tunachojua ni kwamba, makubaliano ya awali yamesainiwa Dubai wakati Rais Samia Suluhu alipokwenda kwenye maonesho ya Dubai Expo 2020, na kama makubaliano ya mwisho yatasainiwa, basi mkataba huu utakuwa na thamani ya USD 500 milioni.
Nini Mtanzania unapaswa kujua kuhusu mkataba huu?
Kwanza, unatakiwa kujua kwamba DP World itapewa
kushughulikia gati ya 5 hadi 7.
DP World mbinu yake ni kuondoa vizuizi vya biashara na kuunda mfumo ikolojia wa biashara ili kupanua mtiririko wa biashara ya kikanda na kimataifa.
▶️Kama mkataba huu utasainiwa, ndani ya miaka 10 ijayo, ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam utaongezeka kwa asilimia 233.7%
▶️Mapato ya Bandari ya Dar es Salaam kuongezeka kutoka Trilioni 7.79 kwa mwaka hadi Trilioni 26, ndani ya miaka 10 ijayo.
▶️Ufanisi wa Bandari utaongezeka, mizogo itatoa haraka, ajira zitazalishwa kwa wingi na pia pato la taifa kuimarika maradufu.
▶️Mapato yakiongezeka kwenye kupitia Bandari ya Dar, serikali itapunguza mzigo wa kodi kwa Watanzania hivyo kuboresha hali ya maisha ya watu.
▶️DP World hawatowekeza bandari ya Dat tu, bali na bandari nyingine nchini na pia, wataalamu wetu watakwenda kupewa mafunzo na kuongezewa ubunifu kwenye utendaji wao.