Sakata la Bandari na DP World: Serikali yashtakiwa Mahakamani

Kwa mara ya kwanza watanzania tumefunguka! Mungu wa mbinguni tunakushuru saana! Lazima wananchi tuamke tutoke usingizini nchi ikiuzwa hatuna pa kwenda! Watoto na wajukuu zetu watakuwa watumwa. Ongera sana watanzania wazalendo kwa kufungua shauri hili na kuwaburuza kwenda kwenye mkono wa sheria na haki
 
Kwenye jambo muhimu kama hili, ninapendekeza mawakili wote wanne wanaohusika katika jambo hilo majina yao yatajwe na yapewe uzito stahiki.
Hawa ni mashujaa wa nchi, iwe wamefanikiwa au hawakufanikiwa katika juhudi zao za kuipigania Tanzania.
Hakika.
 
wewe unasubiri utajiri wako toka kwa Azizi Rostam, au Samia?

Utasubiri sana!
Wewe endelea tu kuwachukia Matajiri kwa sababu lile shetani lenu la Chato ndo lilivyowaaminisha wakifilisika nyie ndo mtatoka kwenye unyonge aliokuachieni
 
Wewe endelea tu kuwachukia Matajiri kwa sababu lile shetani lenu la Chato ndo lilivyowaaminisha wakifilisika nyie ndo mtatoka kwenye unyonge aliokuachieni
Hakuna anayewachukia matajiri hata siku moja maana katika jamii yoyote ile kama hakuna matajiri basi jamii hiyo imekufa.Utaratibu unaotumika awamu hii wa kugawa Rasilimali zetu kwa wageni huku wakisingizia maendeleo kwa kusaini mikataba mibovu ni uhaini.
 
Wewe endelea tu kuwachukia Matajiri kwa sababu lile shetani lenu la Chato ndo lilivyowaaminisha wakifilisika nyie ndo mtatoka kwenye unyonge aliokuachieni
Huu ndio ujinga, kudhani kila mtu anayepinga anapinga kwa sabau ya huyo wa Chato. Unapokuwa na akili ya namna hiyo unajionyesha upungufu mkubwa sana.

Hilo la "kuchukia matajiri" ni lako mwenyewe kwa sababu zako uzijuazo. Tajiri anayepata utajiri kwa juhudi zake mwenyewe, tena kwa haki, utaanzia wapi kumchukia mtu kama huyo?
 
Hakika.
 
Wakili Msomi ndugu Lisu, ongezeka kwenye hilo jopo letu la Mawakili tukapambane nao.
 
CCM ni moja na wanaccm tuko pamoja na Samia mbebamaono ya nchi. DP world welcome and Samia hoyeeeee!
Tulia kijana,uzuri huu mziki ni baina ya CCM maslahi na CCM uzalendo,hayupo mpinzani hapo.

Acha waumane wao kwa wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…