Sakata la Bandari na DP World: Serikali yashtakiwa Mahakamani

Makahakama za Kisutu. ROstam Anasema huwa zinapigiwa simu namna kesi inavyopaswa kuwa
 
Angalau wamefanya kitu mkuu, usiwabeze au kukatisha tamaa, angalau hawajalalamika twitter, insta n.k ni jambo zuri litakavotolewa maamuzi sawa tu ila angalau wanaona jinsi raia wa kawaida wako concerned kiasi gani.
Hakuna chochote wala lolote, ni mjinga tu ndio anaweza kuwaamini CCM na Serkali yake.
 
Shauri lisikilizwe open court badala ya in-camera. Tena iwe live televised ili hata Wakerewe wenye bandari-kivuko wajuwe hatima yao inavyoamuliwa.

Bunge lilijadili hadharani kupitia Media, Mahakama nayo isikilize hadharani kupitia Media.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Lazima nihudhurie!
 
afu anayeamua kesi iendelee ama ifutwe mtendaji mwandamizi wa serikali (DPP) ambaye anateuliwa na Rais. Ukizingatia hili jambo lisingefika hapo lilipo bila baraka za Rais.
 
Wakitoka huko baada ya kushindwa kesi ‘fair and square’ unajua sampuli ya aina hii itakachosema, “judge amepokea maagizo kutoka juu”.

Kama mpaka dakika kuna mtu ajaelewa majibu ya serikali huo sio mkataba rasmi wa kibiashara; awezi elewa tena.

Unapata picha kwanini ata inapotokea serious breach ya mtu kutekeleza shamba kwa miaka kadhaa, wazi serikali ipo sahihi kutaifisha; kesi ikienda arbitration wanashindwa na ndege kukamatwa.

Kwa wanasheria hawa awashindi kesi ya biashara nje ya nchi.

It’s time UDSM ianzishe business law; hakuna hao wanasheria Tanzania.

Ifundishe pia module za introduction to contract law, tort law and business law. Kwenye degree za masomo ya biashara. It’s standard mtu anaesoma masomo ya biashara na finance awe na elementary knowledge ya hayo mambo. Uelewa wa jamii kwenye hayo maswala unapwaya to say the least.
 
Mahakama ipi?
Wajiandae au kufuta kesi au kukata rufaa
 
Seconded as guiding principles for anybody pursuing justice against this Kleptocracy (thievocracy) and state capture of the oligarchs [emoji112][emoji112][emoji112][emoji112][emoji112]

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Maswali yako ni muhim endapo tu IGA na HGAs na Project Agreements vingekuwa na vifungu hivyo.
Ni wakati sasa tusaidiane kwa mtu kuweka kifungu.
..WHAT YOU HAVE TO FEAR IS FEAR ITSELF!
Hii inatuonyesha sasa ccm hawaaminiki tena kias kwamba hawaaminik kuingia mkataba wowote.
 
Vifungu vipo kwenye huo mkataba , nanukiwekwa humu, utafute uusome kama una mashaka
 
Haya ndiyo mambo ya kuunga mkono,siyo.watu wachache watufanye watu milioni 60 mafala.
 

Hatima ya uhalali wa mkataba wa makubaliano ya ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania nay a Dubai sasa kuamuriwa na Mahakama baada ya jopo la mawakili wanne kuiburuza Serikali mahakamani kupinga mkataba huo.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na mjadala mkali kuhusu uhalali wa mkataba huo baina ya Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Dubai kupitia Kampuni ya Dubai Port World kuhusu uboreshaji na uendeshaji wa bandari nchini.

Juni 10, 2023, Bunge la Tanzania lilipitia azimio la kuridhia ushirikiano.

Licha ya Bunge kuridhia, mjadala umeendelea kuhusu ushirikiano huo huku Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwaeleza Watanzania kutokuwa na wasiwasi kwani Serikali haitadharau maoni, ushauri na mapendezo yatakayokuwa yametolewa.

Hata hivyo, wakati mjadala huo ukiendelea kutoka kwa makundi mbalimbali, jopo la mawakili wanne wamechukua hatuza za kisheria kwa kuufikisha mjadala huo mahakamani.

Mawakili hao, Alphonce Lusako, Emmanuel Kalikenya Changula, Raphael Japhet Ngonde na Frank John Nyalusi, wameiburuza mahakamani Serikali, kutokana na kupitisha mkataba huo kwa kile wanachodai hauzingatii maslahi ya nchi.

Kwa mujibu wa nyaraka ambazo Mwananchi limeziona kuthibitishwa na wakili Lusako leo Jumanne, Juni 27, 2023, mawakili hao wamefungua kesi hiyo Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Katibu wa Bunge la Tanzania.

Madai dhidi ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi pamoja na Katibu Mkuu wake wanadaiwa kusaini mkataba huo wa kimataifa na kuupeleka bungeni kwa ajili ya kupitishwa bila kushirikisha umma na kutoa nafasi ya kutosha kwa wananchi kutoa maoni yao.

Wanadaiwa kwa kufanya hivyo wamekiuka Sheria ya Rasilimali za Taifa namba.5 ya mwaka 2017, kifungu cha 11 (1) na (2).

Kwa upande wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Katibu wa Bunge madai yanayowakabili katika shauri hilo ni kuwaongoza wabunge vibaya, kupiga kura ya kuitikia kwa ujumla kwa pamoja (yaani kura ya ndio) badala ya kura ya Mbunge mmoja mmoja.

Wadai hao katika shauri hilo wanadai kuwa wadaiwa hao kuwaongoza wabunge kupiga kura ya namna hiyo ni kinyume cha Sheria.

Kwa mujibu wa hati ya wito wa kufika mahakamani, ambayo Mwananchi limeiona nakala yake, shauri hilo limepangwa kuanza kutajwa Julai 3, 2023 saa 3:00 asubuhi na Serikali (wadaiwa) wametakiwa kufika mahakamani siku hiyo bila kukosa.

Shauri hilo la maombi mchanganyiko namba 5 la mwaka 2023, limepangwa kusikilizwa na jopo la majaji watu lianoloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akishirikiana na majaji Mustafa Ismail na Abd Kagomba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…