Sakata la Jerry Silaa kuvunja majumba ya watu nchi nzima: Johnson Mahululu aidai serikali ya Tanzania bilioni 20

Kwa nini mahululu ana kesi nyingi za viwanja? Hapa ndo panafanya nifikirie pengine waziri yuko sawa.
 
Ina semekana Johnson yuko selo ya polisi ostabey leo siku ya tano bila dhamana wala mawakili na ndugu zake kuruhusiwa kumuona.

Pia kuna tetesi za kumfungulia kesi ya uhujumu uchumi.
Nasikia Jamaa Kichomi kweli. Anaweza akaja kwako na hati akakwambia ni Eneo langu na akaandaa mashahidi anakushinda. Huyo ni tp. Mahakama haiwezi kuamulu au kuamua kila Kitu saizi Kuna Quas Judicial Kwenye kila Wizara.

Na Maamuzi ya Wizara chini ya Quasi Judiciary yao ina maamuzi Sahihi ambayo lakini yanaweza kuwa challenged Mahakamani. Na Tp yoyote huwa anapenda Mahakamani kwasababu technicality za kimahakama kuwa na Uwezo wa kucheza nazo kufanikisha u tp tofauti na maeneo ya ukweli halisi. Waziri aendelee kukoleza Moto. Na Dar ndiko kuna huo mchezo wameuza mpaka maeneo ya wazi
 
Ukimsiliza vizur huyu wakili utajua huyo jamaa ni tapeli kweli. Sasa watu wa aina hiyo unatakiwa uende nae kiumbwambwa hivyo hivyo. Haiwezekan kila kiwanja ukiomba umiliki unakataliwa na kwa akili za kawaida kila mtu anajua mahakama zetu ni kama alivyosema Rostam.
 
Ni ubatili mtupu na uonevu. Tulisema haya mambo iachie Mahakama itoe haki. Jerry Slaa hawezi kutoa haki maana hana mamlaka ya kutoa haki. Anaweza aka-initiate process ya kupatika haki na si kutoa maamuzi kama vile yeye ni mahakama. Mfano kuvunja Ghorofa ya mtu bila amri ya Mahakama.

Sikiliza kisa cha kuhuzunisha cha ukiukwaji Mkubwa wa Haki uliofanywa na Jerry Slaa!

Verry unpleasant kwa mtu wa level ya kwake kufanya alichokifanya



View: https://youtu.be/xTWIKdgZxrQ
 

Jerry anatengeneza mazingira ya upigaji na rushwa......Huyi wakili ameweke kiporo kuhusu namba ya simu....Jerry aliomba namba ya mwenye ghorofa.
 
Hii sasa ni pattern of behaviour inayojitokeza. Watanzania wa twitter republic na wafuasi wa upinzani ni mahodari sana wa kukatisha tamaa viongozi hasa mawaziri wanaojaribu kurekebisha mambo. Same kwa wakuu wa wilaya na mikoa wanapojaribu kutatua migogoro.

Ilikuwa hivi hivi kwa Jaffo, Gwajima na sasa mnaanza kwa Slaa. Hata sijui mnataka nini, hakuna siku utaamka utakuta mambo yapo shwari tu lazima kuwe na watu wakupambana kuyaweka sawa.
 
Utapeli mtupu.
Ukichunguza sana , hao matapeli wana mtandao wa nyaraka zinazotoka huko huko wizara ya Ardhi.
Jerry Slaa asiishie kuvunja hayo maghorofa, na wale maafisa Ardhi waliohusik watiwe haiani.
 
Kabisa...anaendesha mashitaka yeye, anatoa hukumu yeye, tena siku hiyo hiyo, na siku hiyo hiyo anavunja, kwa nini asitoe hata siku 90 ili mtu ambaye hajaridhika aende kwa Waziri Mkuu, au Rais au Mahakamani?

Kuna issue ya yule mbunge Kamani, kale ka dada, only to find out ni girlfriend wake wa enzi za Uvccm, kapata uwaziri katoka mbio kwenda kumkabidhi baba mkwe wake kiwanja huko mwanza.

Mahakama imeweka mifumo rasmi, unaanza ngazi hii, hujaridhika, unaenda mbele, hujaridhika, unaenda mbele, sasa Jerry ndio Alfa na Omega, anatukana mahakama mbele ya wananchi, sasa serikali moja kwa nini mmoja anatukana taasisi ya mwenzake?

Kitendo cha kuhamasisha wananchi wasiheshimu taasisi ya kikatiba ni uhaini na anapaswa kujiuzuru mara moja. Anabaki kufanya nini wakati aliapa kuilinda katiba, katiba hiyo ndani yake ina mahakama, na yeye anahamasisha uasi wa wananchi dhidi ya mahakama?
 
Umelipwa kiasi gani na huyo tapeli wa viwanja vya watu?
 
Kwa wale ambao ni wataalama wa lugha kwa ufupi ,siasa za upinzani haswa chadema is simply a disgrace to the nation
 
Wakili anaongea taratibu sana, mb zinapotea ovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…