Sakata la Kupotea Rajab Omari Mtana na Hukumu ya Kunyongwa kwa Masheikh 10 Tanga

Umemueleza barabara!! na bayana.

Seme alishajichagulia upande so hamtoelewana.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
Mazi...
Hakuna asiyekuwa na upande.
Upande wangu ni huu kuwa historia iliyoandikwa ina makosa.

NImeandika kitabu kusahihisha makosa hayo.

Hajakuja mwandishi mwingine kusema kuwa historia niliyoandika si kweli.

Hapa nani hataki kumwelewa nani?

Ukimya huu wa kutojibu kitabu changu nini maana yake?
 
Political history inayoanza kwa ku classify wahusika kwa dini zao??? What a shame kutoka kwa mtaaluma kama wewe.
Masta....
Naam anaandika Kleist Sykes katika mswada wa kitabu alioandika kabla ya kufariki kwake 1949 anasema waasisi wa African Association wengi ni Waislam kwa kuwa wamishionari walikwakataza waumini wao wasijiingize katika siasa.

(AD Sykes "The Life of Kleist Sykes" Ref. No. JAN/HIST/143/15 1968 East Africana, University of Dar-es-Salaam).
 
Nonesense. Hao waislamu walikua watanganyika au waburundi?
 
... kila penye neno muislamu hapo nadhani ungefaa kuweka mtanzania..
...
Mkuu waislamu siyo raia wa kawaida wao wana dunia yao ndiyo maana wanaonekana kujitenga na ngano.

All in all namfikilia yule mgambo aliyefariki ambaye ndiye chanzo toka anakamata gari, kwa nini achukue maamuzi ya kwenda kwa mkulima ambaye hausike kwenye bidhaa iliyonunuliwa kwake?.

Hakika baadaye ndipo naona njia ya kifo kinavyokuja, yaani naamini kauli ya Allah kuwa 'laiti ungejua siku ya kuja mwivi usiku ungekesha'.
 
Mzee kashupaza shingo. Akiambiwa anaendekeza udini, anakimbilia kwenye historia ya TANU. Huko tukishatoka, tunataka tuishi bila haya mapazia ya dini. Kama tunavyopanda mabasi pamoja, kama tunavyoshabikia mpira pamoja, kama tunavyojitambukisha kama Watanzania pamoja, bila kuweka udini mbele, ndivyo tunavyotaka kuishi. Hizi chokochoko kwamba wengine wanaonewa kwa sababu ya dini yao, hazitujengi shehe wangu. Tumia kipawa na kalamu yako kusambaza upendo. Wanasema, ukiona unafuatwa na kundi la nzi, usiulize hawa nzi wana nini, bali jiulize wewe una nini kinachowavutia hao nzi. Wengi humu wamekuhukumu kwa kusambaza udini, lakini kwa sababu umeshupaza shingo, unahisi wote wanakosea. Inasikitisha sana mzee kukosa busara
 
Kwenye hili bila kupepesa naiona state crime hususan kwa viongozi ngazi za kijiji hadi mkoa.

Mungu awasimamie masheikh.
Mungu afunue ukwelli wa kilichomsibu Rajab Omari Mtana
 
Na hawatafanikiwa. Ukiisoma hii thread, unaona kama ukosefu wa busara. L:eo kama mtu ameuwawa, basi tunaanza kwanza kuangalia dini yake, ili tujikite katika kuhalalisha ujinga wetu, kama aliyeuwawa ni wa dini yetu.
Bila hata kujali alifanya nini
 
Vangi...
Sikimbilii historia ya TANU.

Historia ya TANU ndiyo yenye misingi ya umoja na laiti kama ungeijua historia hii ungejiuliza imekuwaje tumefika hapa nchi imegawanyika?

Kikao cha kumtia Julius Nyerere katika uongozi wa TAA kilifanyika nyumbani kwa Hamza Mwapachu (1913 - 1962) Nansio Ukerewe.

Waliokuwa katika kikao hicho ni Hamza Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).

Ndugu yangu ushajiuliza kwa nini historia hii haijulikani?

Athari ya kukosa kutambua misingi hii ndiyo haya unayoeleza wewe hapo juu.
 
Wewe ni mbilikimo wa akili pia.
Wewe jamaa inabidi ukapimwe akili kwa sababu unaonyesha kila dalili ya ukichaa. Inakuwaje unamtukana mtu kwa sababu tu hoja yake huipendi? Kwani lazima ujibu si upige kimya tu? Kama umesoma basi elimu yako haina maana yoyote na ni mzigo kwa nchi.
 
Wewe jamaa inabidi ukapimwe akili kwa sababu unaonyesha kila dalili ya ukichaa. Inakuwaje unamtukana mtu kwa sababu tu hoja yake huipendi? Kwani lazima ujibu si upige kimya tu? Kama umesoma basi elimu yako haina maana yoyote na ni mzigo kwa nchi.
Kuwa na adabu unapoona comment yangu. Kwa akili zako zilivyo ndogo unaona anachofanya Mzee Mohamed ni kitu sahihi. Unadhani machafuko yanavyotokea ni jambo la siku moja tu? Inaanza polepole na mambo kama ya huyu Mzee Mohamed.. kupandikiza chuko taratibu. Siwezi kukaa kimya pale mtu anapoichezea amani ya nchi hii.
 
Kama walitishia usalama wa nchi lazima wangeuawa
 
Wewe huna akili ndiyo maana unatumia lugha za matusi na zisizo za kistaarabu. Kama hukubaliani na hoja ya mtu tumia lugha za staha kumnasihi na siyo kumtukana. Unamwitaje binadamu mwenzio nguruwe?
 
Huyu Mzee anatabia za chuki za kidini kama yule sheikh ilunga alikuwa anahamasisha mauaji ya mapadri
 
Hawa ni waumini wa kawaida au Mashehe?
 
You really didn't get my point. Na inawezekana utaendelea kutonielewa. Binafsi, nimekiri kwenye post zangu mbili huko juu kwamba kwa suala la historia ya TANU, uko vizuri. Inawezekana nilichojifunza shule hakikuwa sahihi, ingawa hainipi madhara yoyote. Point yangu kubwa ni namna ulivyotumia kisa hiki kuonyesha kwamba madhira waliyoyapata hao Watanzania wa Handeni, yametokana na Uislamu wao. Hapa ndipo wote waliokupinga, wameparejea. Hili halihusiani na Nyerere na TANU. Hili halihusiani na nani alidai uhuru wa Tanganyika. Hapa tunaongelea Watanzania. Nilitabiri utashupaza shingo, umeshupaza. Bado nakushauri, soma maoni ya waliokukosoa kwa utulivu, bila kimue cha kutaka kuprove kuwa uko sahihi. Unaweza kujifunza kitu
 
Nasikitika kuwa Mohammed ameamua kuwa mpuuzi wa kudumu
Mjinga wa muda wote

Wapumbavu huwa na 'confidence' sana. Sijui hii inatokana na nini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…